Mapigano ya wamasai na waarusha: Watu wengi wameumizwa na maboma yamechomwa moto

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,575
523
kwa taarifa kutoka ITV kunamapigano kati ya waarusha na wamasai kwenye eneo la Longindo kutokana na malisho ya mifungo tunaomba walio karibu wazidi kutuhabarisha
 
Watu 12 wamejeruhiwa na nyumba kuchomwa moto! Serikali itatue migogoro ya ardhi kabla ya madhara makubwa
 
kwa taarifa kutoka ITV kunamapigano kati ya waarusha na wamasai kwenye eneo la Longindo kutokana na malisho ya mifungo tunaomba walio karibu wazidi kutuhabarisha

unaomba kupewa habari badala kuiomba mamlaka kuingilia kati kunusuru maisha ya watu!!!!! Wewe wa ajabu kweli kweli.
 
sasa hawa jamaa wakipigana....si watapigana sana.......
 
habari kamili utaipata wakitulia,idadi ya ng`ombe zitakazotozwa kama fine kwa walikufa na kujeruhiwa .Wanaongea lugha moja na wote wanalipa uhai kwa ng`ombe ila wanatabia nyingine tofauti sana.
 
Ndo matatizo ya kuwa na serikali DHAIFU. bado napata taabu kujua ukweli wa nini hasa kazi za wakuu wa wilaya na mikoa. Kuna mahali nilisoma eti ni wenyeviti wa kamati za usalama kwenye maeneo husika. Hizo kamati zina husika na usalama wa nani??? wa ccm au wa wananchi??? Kwa nini sheria zetu tulizonazo hazitumiki kushughulikia hii migogoro kwa haki tukaepusha huku kuchinjana wenyewe kwa wenyewe??? mimi bado naamini kinga ni bora kuliko tiba. Hii inaonyesha kushindwa kwa kamati za usalama zote za wilaya na mkoa katika eneo husika.
 
Haya ndio matatizo ya kutoshughulikia overgrazing. Ardhi haiongezeki bandugu, shughulizetu ndio huongezeka, na tusipoangalia vitaibuka vita vya kugombea si tu maeneo ya kulisha bali maeneo ya kunywesha. Tuelimishe wafugaji ufugaji wa kisasa na wakulima ukulima wa kisasa. Mambo ya kuhamahama kutafuta malisho yamepitwa na wakati.
 
Wacha wapigane wauane hawa jamaa wameuza mpaka mifereji kwa tamaa ya kuuza viwanja!:frusty:
 
Back
Top Bottom