Mapigano ya ardhi Tanzania yanachochewa na umiliki wa silaha kinyume cha sheria

Uhuru n Umoja

JF-Expert Member
May 25, 2016
684
1,000
Kwa ardhi kubwa tuliiyonayo mapigano ya ardhi ni ya lazima kweli ama uzembe wa serikali?

Mimi sio mtu wa kunzisha uzi or kukomenti ila nlichokiona leo kimeniuma. Iwaje mtu mapigwe mkuki mpaka utokee upande wa pili?

Kisa wanasema eti ardhi, ardhi? Swala sio ardhi. Wamasai waliompiga jamaa mkuki wanamiliki ardhi ipi?

Tanzania tunatatizo kubwa la umiliki wa silaha kinyume cha sheria. Wamasai wanatembea na silaha kila mahala watakavyo na lakini wengine wakifanya hivyo wanachkuliwa hatua za sheria.

Wamasai wako juu ya sheria? Maana wanatembea na silaha, na wanavunja sheria kwa kuharibu mashamba ya watu na pindi watu wasio na silaha, wanapojaribu kulinda mashamba yao wanashambuliwa na silaha za Wamasai wanazobeba.

Hili swala ni la miaka mingi zaidi ya 30.

Na kwa muda sasa Serikali imekua kimya juu ya mauaji na majeraha jamii hii ya wabeba silaha kisheria ya Kimasai imekua ikifanya.

Ni kwanini waruhusiwe kuendelea kubeba silaha? ama ni ishara kwa wengine kubeba silaha na kujichukulia sheria mikononi?
 
stemcell

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
677
1,000
Mtakatifu anaona aibu kuwatetea wakulima kwani moja katika jamii inayosumbua wakulima ni kutoka kwao,kiukweli kama una mifugo wa kutosha kwanini usioteshe majani yenu kuliko kutegemea ya mungu?hii nchi haiwezi kuendelea kama mabadiliko yanalenga ukilima wa kisasa pekee bila kuwa na sera ya ufugaji wa kisasa,ardhi aslimia 35 ni hifadhi na mbuga za wanyama na msitu,ukichanganya na milima na mabonde ardhi haitoshi kwa ufugaji wa kuzurura,lazima tubadilike na tusioneane aibu.

SmartSelectImage_2016-02-15-16-20-32.png
 
Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,792
1,500
Kuna jamaa yangu aliwahi kusema serikali ingekua makini na land management: mikoa ya Morogoro, Pwani, Ruvuma, Mbeya, na Rukwa haikupaswa kuwa na mifugo inayotembea .. Ni zero grazing tu.
 
JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,760
2,000
Nimeishi na wamasai ni watu wenye inferiority complex, hata kama amesomaje. Hivyo wamekuwa wakatili wasio na utu. Kifupi, Masai ni tatizo.

Kwa upande wa mwingine, pia kumekuwa na tabia ya kilimo holela. Wakulima wanaanzisha mashamba kiholela. Mimi maranyingi nasafiri kwa mabasi na nimeweza kusafiri sehemu nyingi za nchi yetu, huko njiani nashuhudia uharibifu wa misitu ya asili kunakofanywa na watu wanaotafuta ardhi ya kilimo. Kilimo kinaambatana na kufyeka miti na kuchoma mikaa na kupunguza maeneo ya malisho. Ukulima wa namna hiyo pia ni tatizo.
Kwa kifupi bila kuwa na mipango ya uhifadhi wa misitu, kilimo na ufugaji endelevu, mapigano ya wakulima na wafugaji hayatakoma.
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,174
2,000
Swala la matumizi ya ARDHI hapa kwetu bado ni kitendawili. Bila serekale kuchukua hatua za makusudi kuweka mipango ya matumizi bora ya ARDHI migogoro haitakwisha! Tunaweza kuwaona wafugaji ni wakorofi kumbe hata wakulima wenyewe nao ndo wakotofi. Mara nyingi wafugaji wanapohamia mikoa fulani huenda kukaa ndani kabisa ambako hata wakulima walikuwa hawana habari napo. Hapa nazungumzia uzoefu wangu wa maeneo ya KASULU, Mpanda, Ulanga, Kilombero na Urambo. Kuna vijiji vingi vimeanzishwa na wafugaji matokeo yake wakulima waliamua nao kuhamia huko na kuanzisha vijishamba vyao, huu kwangu ni ukorofi! Kama yunavyofahamu Wasukuma ni agropastoralists wakifika mahali kama kuna ARDHI na mvua basi tegemea mavuno ya hatari kabisa, sasa hii imekuwa ikiwachochea wakulima kuwafuata Wasukuma huko waliko na kuanzisha vijishamba! Serikali iwasaidie wafugaji kuweka mipango ya matumizi bora ya ARDHI. Mkulima asiruhusiwe kuingia kwenye eneo la machunga na mfugaji asiruhusiwe kuingiza MIFUGO kwenye eneo la KILIMO. Ng'ombe akikutwa huko ataifishwe na serikali na kupelekwa kwenye ranch za Taifa "kama mbwai na iwe mbwai" mkulima naye akikutwa kule tumkute Ukonga, Keko, Segerea, Butimba au Kisongo!
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,135

Sitaki kupingana na wewe ila ume generalize mno, kasulu hakuna mahali popote penye pori lisilo na mwenyewe, nitajie kijiji
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,975

You might be having a point but this won't make a permanent solution. We need more than that! How? Let us debate. (mimi naishia hapa, sitachangia possible solution)
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,174
2,000
You might be having a point but this won't make a permanent solution. We need more than that! How? Let us debate. (mimi naishia hapa, sitachangia possible solution)
How then can we debate kama huchangii unaishia hapo? Mipango ya matumizi bora ya ARDHI ndiyo suluhisho kuna ushahidi kule Kiteto ambako kuna ARDHI imesajiliwa kwa ajili ya wafugaji na kwa kiasi kikubwa imepunguza sana misuguano kati ya wakulima na wafugaji! Kama nakumbuka vizuri inaitwa OLENGAPA ni muungano wa vijiji kama 6 hivi vya wafugaji! Bila kuigawa ARDHI tutaendelea kupigana kila siku!
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,174
2,000
Sitaki kupingana na wewe ila ume generalize mno, kasulu hakuna mahali popote penye pori lisilo na mwenyewe, nitajie kijiji
Mkuu unafahamu kijiji cha Malalo kilianzaje? Unafahamu Asante Nyerere kilianzaje? Pale Basanza Wasukuma wameenda kukaa 26 km kutoka kijiji cha wakulima lakini Waha wamewafuata mpaka huko ndani baada ya kuwaona Wasukuma wanafuga na kulima mpunga! Hivyo ni vichache nilivyokutajia!
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,975
2,000
How then can we debate kama huchangii unaishia hapo? Mipango ya matumizi bora ya ARDHI ndiyo suluhisho kuna ushahidi kule Kiteto ambako kuna ARDHI imesajiliwa kwa ajili ya wafugaji na kwa kiasi kikubwa imepunguza sana misuguano kati ya wakulima na wafugaji! Kama nakumbuka vizuri inaitwa OLENGAPA ni muungano wa vijiji kama 6 hivi vya wafugaji! Bila kuigawa ARDHI tutaendelea kupigana kila siku!
Hiyo ni solution mojawapo. Tunaanzia na kutenga kama unavyosema. Lakini ngombe/mifugo ni mingi sana. Ardhi isipotosha tunafanyaje? Kupunguza mifugo???? Wafugaji hilo hawataki kulisikia!
Labda kwa kuanza tuanze na hilo la kutenga ardhi kwa wakulima na wafugaji.
 
papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,625
2,000
kwenye hili sakata la wakulima na wafugaji kuna mambo mengi tuu chini ya 'kapeti' jamii haitaki kuyatatua
mfano, wamasai wamefukuzwa kwenye ardhi zao za asili kule kwao kwa kisingizio cha uwekezaji, kubwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa 'population' & 'other human activities' maeneo mengi yaliyo kuwa yametengwa kwa ajili ya wafugaji yamegeuzwa kuwa mashamba, mashule, mahosipitali, makanisa, makazi, nk, hivyo jamani wafugaji waende wapi? wakienda kwenye forest reserves wanafukuzwa, wakirudi kwenye maeneo yao ya asili wanatimuliwa, si kama na watetea lakini kuna namna inatakiwa ifanyike na hasa upande wa wafugaji ili kumaliza tatizo hili
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
11,135
2,000
Mkuu unafahamu kijiji cha Malalo kilianzaje? Unafahamu Asante Nyerere kilianzaje? Pale Basanza Wasukuma wameenda kukaa 26 km kutoka kijiji cha wakulima lakini Waha wamewafuata mpaka huko ndani baada ya kuwaona Wasukuma wanafuga na kulima mpunga! Hivyo ni vichache nilivyokutajia!
Asante nyerere ilikuwa general land, ilipimwa mashamba 400 yenye ekari 100 kwa plot na kugawiwa kwa wananchi nao wakasajiri ushirika wao, basanza ndo kijiji rasmi na kwa sasa hakina pori na wamepungukiwa ardhi kuyokana na ongezeko la watu, mzindakaya alipokuwa rc alianzisha vijiji vingi akihimiza Kilimo cha kufa na kupona
 
jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,917
2,000
Nimekuwa nikisikia haya mapigano na mauaji kati ya wakulima na wafugaji tangu kipindi cha Mkapa.
1.Kilosa hili ni eneo sugu na ni aidha serikali imeshindwa kudhibiti au inadharau maisha ya wanaokufa miaka na miaka(nipo tayari kupewa sababu nyingine kama hiyo ya kushindwa na kudharau maisha ya raia sio sahihi) Jirani yangu Mwigulu analijua hili vizuri maana ni mwaka huu tu alikwenda na kushuhudia mauaji ya wanyama na uharibifu wa mali.
2. Rufiji huku kuliwahi kutokea mapigano miaka kadhaa nyuma. Napo hali si shwari kwani kwa sasa ni swala la muda tu.

Waliopewa dhamana ya kusimamia mambo haya wafanye kazi yao. Inawezekana kuepusha mapigano na mauaji
 
Dr. Msafiri

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
471
250
Nimefanya kazi (ugani & uchunguzi / utafiti) tangu mwaka 1976 katika maeneo mbalimbali hapa nchini (Mikoa ya Mwanza, Singida, Mbeya, Manyara, Arusha, Rukwa, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Dodoma, na Tabora! Kinachokosekana hapa nchini ni programu, mipango na shughuli endelevu za uhifadhi & matumizi ya misitu / maliasili, kilimo na ufugaji tangu tupate uhuru kutoka kwa wakoloni. Bado tunaendesha kilimo duni & holela pia ufugaji (uchungaji) duni & holela: kwa mfano - mkulima kuhodhi ekari tatu za kulima mahindi na kuvuna gunia 10 ambapo kwa kuzingatia maarifa na juhudi kiasi hiki kingevunwa kwenye ½ ekari tu! Kwa hatua jamii ilipofika sasa, panahitajika mjadala wa muda mfupi lakini yakinifu yakianzia kuwepo kwa katiba mwafaka kisha makubaliano ya jinsi ya kutumia ardhi yetu _ master plan! Vinginevyo mapigano kati ya wakulima, wafugaji na watumiaji ardhi wengineo hayatakoma!
 
Dr. Msafiri

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
471
250
Ni ajabu pia kwamba kunatokea ugomvi (tena unaochukua muda mrefu na rasilmali) wa mipaka kati ya vijiji au wilaya au mikoa! Kwamba Serikali inayoweka mipaka hii inakataa kuona hii aibu!
 
Bei Mbaya

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
2,263
1,250
Manjagata. Retired

ule mpango wa upimaji nchi hautasaidia?

kuna makampuni 58 waliambiwa washirikiane na ofisi/ viongozi wa Halmashauri wapange matumizi na upimaji nchi nzima
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom