Mapigano dhidi yako mwenyewe 💪

Mapigano dhidi yako mwenyewe 💪

Ninawi na Nabii Yona – Muhtasari

Ninawi ulikuwa mji mkuu wa Dola ya Ashuru, uliosifika kwa utajiri, nguvu za kijeshi na uovu mkubwa. Kwa sababu ya maovu yao, Mungu alimtuma Nabii Yona kwenda kuwaonya kwamba mji ungeangamizwa ndani ya siku 40 ikiwa hawangetubu.

Mwanzoni Yona alikataa kwenda na akajaribu kukimbia. Baada ya kupitia tukio la kumezwa na samaki mkubwa kwa siku tatu na usiku tatu, alitii agizo la Mungu na kwenda Ninawi.
Kumbe kisa cha Yona kumezwa na samaki sababu ilikua kukataa agizo la Mungu😳
Alipofika, alitangaza ujumbe wa toba. Cha kushangaza, kuanzia mfalme hadi watu wa kawaida walitubu, wakafunga na kubadili mwenendo wao. Mungu akaona toba yao na akaahirisha adhabu aliyokuwa ametangaza.
Ooh asante mkuu
 
Jonah Alikaidi amri Ya Mungu, Kisha Akapanda merikebu kupelekea Tarshish instead of Nineveh (Ninawi)

Wakiwa katikati ya bahari Chombo likapata dhoruba, Waliokuwa mke ndani wakapiga kura/Ramli/wakafikiri kwa kina Ya kubwa huyu huenda Kwa hakika na yakini kubwa ndiye aliyetuletea Zahama yote hiyo kisha wakatupa baharini ...

Napendekeza ukisoma kitabu cha Jonah kwenye biblia kwa uelewa zaidi
Asante ni tasoma nikikumbuka nitakuletea mrejesho
 
Natoa angalizo kwa wale wa unashinda JF full-time
Huu ni kama ushauri tu kwamba hii mada inakuhusu isome yote ili uanze leo kupigana na hiyo tabia isiyopendeza ya kufatilia ni nani anaingia online sa ngapi na anatoka saa ngapi

Sisi wengine kuandika ni moja wapo ya enjoyment 😊

Na hii platform sio kama hizo zingine za kupost makalio au kutafuta attention hapa tulio wengi hatufahamiani

na hii inatupa uhuru wa ku share kujifunza kupiga story na kufurahia maisha kwa mtindo huo

kwa wale wote wanaovutiwa na nyuzi zangu guys nipo in love kwenu 🥰 nawapenda sana😊😊

Twende zetu sasa 👇

Mapigano yapo ya aina nyingi Umewahi kusikia nchi fulani ikiwa vitani?
Watu husema nchi A inapigana na nchi B. Hayo huitwa mapigano

Pia kuna mapigano kati ya watu wawili, mtu A na mtu B, kama vile yanavyotokea ulingoni( mtu anapigwa hata kwa TKO)

Hata wanyama nao hupigana mfano kuku, mbuzi na wengine

Lakini je, umewahi kujiuliza kama inawezekana mtu kupigana dhidi ya yeye mwenyewe?

Jibu ni ndiyo, inawezekana kuwa na vita au mapigano dhidi yako mwenyewe

Haya ni mapigano ambayo hayapiganwi kwa ngumi wala silaha, bali ni mapambano ya ndani ya nafsi

Ni pale unapogundua kuna kitu ndani yako ambacho hakikufanyi kuwa mtu unayetaka kuwa, hivyo unaamua kukikabili

Mfano unaweza kujijua kabisa una tabia fulani kama wivu, hasira au kutokuwa na subira

Baada ya muda unagundua tabia hiyo haikusaidii wewe wala jamii inayokuzunguka

Hapo ndipo vita vinaanza siyo dhidi ya mtu mwingine, bali dhidi ya hiyo tabia iliyopo ndani yako

Unaanza kujifunza kujizuia kujirekebisha na kuikataa ile hali ambayo haikupi thamani

Kwa mfano, kama zamani ulikuwa huwezi kukaa nyumbani na kila mara ulitamani kutoka, siku moja hamu hiyo inapokuja unaweza kujikuta ukisema

Hapana, siendi leo(unakaza)

Hapo unakuwa umeanza kupigana dhidi yako mwenyewe unayashinda matamanio yako kwa ajili ya lengo kubwa zaidi

Sasa swali la mjadala👇

Wewe umewahi kuwa na vita au mapigano dhidi yako mwenyewe?
Ni nini kilishinda wewe au kile ulichokuwa unapambana nacho?

Ulipigana kwa muda gani, na ulitumia njia gani kushinda?

Nyongeza👇
Kabla hujaanza mapambano hayo, ni muhimu kujifanyia utafiti wa nafsi yako Jifahamu, tambua tabia zako, haiba yako na vitu vinavyokufanya uwe wewe

Baada ya hapo utaweza kuona kama kuna mambo ndani yako unayoyapenda au kuna mengine ambayo yanahitaji kubadilishwa

Kwa sababu wakati mwingine ushindi mkubwa wa mtu siyo kumshinda mwingine, bali ni kujishinda mwenyewe na kuwa yule mtu ambaye anatamani kuwa

Happy weekend 🔥
ShesRise_1 ✋️
Uzi wako huu unatufundisha nini dada?
 
That's the issue with you, huku soma vizuri comment yangu?

Sikusema wewe ni mtoto nilisema zinakufanya uonekane kama mtoto zingatia hilo next time

Ni kweli ila unatakiwa kupunguza au kujaribu kupunguza Misconception au kudhani mtu anaku attack kila wakati.
ephen_ nimethibisha kumbe de gunner ndio Elevenn 🙌🙌🙌

Aisee niko hoi 🤣🤣🤣
 
A
1

Mkuu, kitu cha kwanza ni kujikubali mwenyewe

Amini kwamba una uwezo wa kuzungumza na watu na kwamba mawazo yako yana thamani

Acha kujiuliza sana Watanichukuliaje nikiongea

Ukweli ni kwamba hakuna mtu mkamilifu

Kila mtu ana changamoto zake na kila mtu hujifunza kwa kupitia makosa

Wewe kama ni kuongea ongea ukikosea kesho utajifunza kupitia makosa yako ya leo

Anza kuongea taratibu bila kuogopa kuhukumiwa maana challenge utakutanazo na ni kawaida

Wengine watakuelewa, wengine watakosoa, lakini hata maneno mabaya yakitokea yachukulie kama changamoto ya kukufanya uwe bora zaidi

Ujue kabisa hata iweje huwezi kukubalika na wote haiwezekani ukijua hivyo utakua huru kufanya unavyopenda bila kujali matokeo hasi dhidi yako
Asante sana mkuu
 
Mapigano ya kuacha kubet duh! miaka miwili napigana tu since niko form two hapo, form three ndo ikawa balaa maana nilidrop hadi kimasomo, form four nikaongeza jeshi la kiroho nikatumia silaha nzito inayoitwa prayer mapema tu nikashinda uraibu na necta nikapata grade nzuri tu!
 
Mapigano ya kuacha kubet duh! miaka miwili napigana tu since niko form two hapo, form three ndo ikawa balaa maana nilidrop hadi kimasomo, form four nikaongeza jeshi la kiroho nikatumia silaha nzito inayoitwa prayer mapema tu nikashinda uraibu na necta nikapata grade nzuri tu!
Hongera sana sana
 
Back
Top Bottom