Mapichapicha ya CUF Tanganyika (Mungiki)

Mapichapicha ya CUF Tanganyika (Mungiki)

CUF bara wajitathimini, Heshima ya CUF kwa kiasi kikubwa inaundwa na Zanzibar
 
Tatizo watu wanaingia kwenye vyama hivi vya siasa bila ya kuangalia Katiba za vyama hivyo zinasemaje. Kwanza kwenye CUF Zanzibar ina uwakilishi sawa kwenye vikao na Tanganyika, kwa ivo si rahisi kukwamisha mambo yao kama wanayataka kwani siku zote Akidi itatimia tu. Halafu wajumbe wengi wa Tanganyika ni wa kuokkoteza mitaani wengi wao hawatoke kwenye hiyo mikoa wala Wilaya wanazodai wanaziwakilisha.
Kama akidi inatimia ilikuwaje sharifu hamad akaja mamluki wengine 30,ambao sio wajumbe
 
Yaliyoandikwa na Abdul Kambaya aliyekuwa naibu mkurugenzi wa Habari na Uenezi cuf leo mtandaoni(FB)

"SIJAMBO GENI, HATA FIRAUN ALIPOSHINDWA KUJIBU HOJA ZA MUSSA ALITUMIA JESHI

Nimekua napigiwa simu nyingi toka kwa Wanachama wenzangu na Waandishi wa habari kuhusu Taarifa zilizozagaa kwenye Mitandao. Majibu yangu ya awali Kuhusu Taarifa hizo ni

1 Moja Baraza Kuu lina Mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na kwa kwa kufuata Katiba jinsi inavyoeleza kwenye hizo taratibu za kuchukua hatua za Kinidhamu.

2 Mimi na wenzangu tunaotajwa kwenye kadhia hiyo ikiwa ni Pamoja na Wabunge wa Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma) na Magdalena Sakaya Mbunge wa Jimbo la Kaliua na Diwani wa Kata ya Misima Wilayani Handeni,pamoja na wale ambao sikuwataja hatukuwepo wakati hukumu hiyo inatolewa na Baraza Kuu lilofanyika jana Mjini Unguja katika Visiwa vya Zanzibar.

3 Baada ya kuahirishwa kwa Mkutano Mkuu uliofanyika pale Ubungo Plaza Tarehe 21 /08 /2016 kutokana na Wajumbe 324 kutoridhishwa na ukiukwaji wa Katiba ya Chama chetu ikiwa ni pamoja na kuingizwa kwa Wajumbe wasio halali kwenye Mkutano Mkuu, mimi ni miongoni mwa Wajumbe tuliojiorodhesha na kuandika barua ya Malalamiko na kupeleka Ofisi ya Msajili wa Vyama.

Kutokana na Mambo hayo Matatu, nawaomba Wanacuf msifadhahike na wala msihuzunike waliotufukuza kabla hata ya kutoa majibu ya hoja zetu tulizowasilisha kwa Msajili, bila shaka hawana Majibu ya sahihi ya hoja zetu. Na jambo hili sio geni kwa hapa Duaniani, Firaun aliposhindwa kuthibitisha kua yeye ndie Mungu, alitumia Jeshi lake (Baraza Kuu) kutaka kumuangamiza Mussa na Wafuasi wake waliokua wanaamini katika Haki na Mungu wa kweli.

Kilichoendelea Zanzibar ni Mfano wa Firaun na Jeshi lake dhidi ya Mussa na Wafuasi wake.

Kauli yangu ya Mwisho ni kwamba hatoki mtu kwenye Cuf hii kwakua sio ya Mtu bali ni ya watu, sijambo jema kujifananisha na Firaun, jibu hoja usitumie Jeshi kujibu hoja. Hakuna kukataa Tamaa wala kukimbia Cuf. Harakati za kutafuta Uhuru ndani ya Cuf kwa Watanganyika ndio kwanza umezifungulia Geti, sasa ni hoja za Makabwela dhidi ya Vibaraka wa Mabepari wa Tanganyika."



Je?Kama Mussa ni Prof. Lipumba na Firauni ni Nani!
'Hakika Mfa Maji Aishi Kutapatapa......'

njaa mbaya....dah!!
 
Maalim awe kibaraka kwa kukataa kibaraka kuwa kiongozi wa chama alichokipigania wakati mwingine hata kuhatarisha maisha yake. Halafu huu ujinga wa kumkuza sana Lowassa hadi kufikia hadhi ya uungu mtu inawapa faida gani? Kila jambo ni Lowassa kafanya, mbona mnamuabudu sana nyie?
You are barking at the wrong tree!
Nimekutafsiria maana ya maneno ya Abdul Kambaya. Yaani nini alimaanisha aliposema kibaraka wa mabepari wa Tanganyika.
Personally, I don't care about weird parties/people.
 
Alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi sasa anafanya uenezi wake ipasavyo.
 
Hana akili huyu,anampigania Lipumba alieondoka CAF kwa akili zake timamu,watu wengine bure kabisa
Hivi nyie machadema kwa nini mnamuogopa sana Lipumba? Kwa nini msijadili uchaguzi wa mwenyekiti wenu wa maisha?
 
Tatizo dhambi ya Usaliti inamtafuna LIPUMBA na timu yake(Kambaya,sakaya +mungiki)waliyoifanya wakati wa kampeni Mwaka Jana.
Msaliti ni Lipumba aliyeyakimbia mabadiliko feki, au ni DJ aliyekuwa tayari kumpokea mtu aliyeshiriki katika kumponda kisiasa kwa miaka nane?.
 
Kama Mbowe and the team wasingebadili gear angani na kumkaribisha "mgeni" UKAWA Tifu hili lisingekuwepo,manake pale ilikuwa ndio mwanzo wa kupoteana, na yote yanayotokea CUF leo chanzo ilikuwa ni siku ile GEAR ILIPOBADILISHIWA ANGANI.
 
Weka nyama ili jamii ikuelewe
Kama Mbowe and the team wasingebadili gear angani na kumkaribisha "mgeni" UKAWA Tifu hili lisingekuwepo,manake pale ilikuwa ndio mwanzo wa kupoteana, na yote yanayotokea CUF leo chanzo ilikuwa ni siku ile GEAR ILIPOBADILISHIWA ANGANI.
 
Hivi nyie machadema kwa nini mnamuogopa sana Lipumba? Kwa nini msijadili uchaguzi wa mwenyekiti wenu wa maisha?
Unikome,mimi sio CHadema, huyo Lipumbavu aliondoka kwa akili timamu, nimeamini kusoma sio kuelimika, ina maana aliondoka bila kuwa na plan B? Hakufocus sideeffects katika maisha yake kutokana na maamuzi yake ?
 
Unikome,mimi sio CHadema, huyo Lipumbavu aliondoka kwa akili timamu, nimeamini kusoma sio kuelimika, ina maana aliondoka bila kuwa na plan B? Hakufocus sideeffects katika maisha yake kutokana na maamuzi yake ?
Unakaa Nyagwa nini? Unayemtolea lugha ya ufedhuli hapa nani? Kwenda kashikishwe UKUTA bila K.......jel.
 
Back
Top Bottom