Mapenzi uwanja mpana,
Ya sasa tofauti na ya jana,
Wakati ule mimi kijana,
Vijana wakipendana,
Huishia kuoana.[/SIZE]
Pesa haikuwa kitu cha maana,
Starehe na mapenzi wala havikulandana,
si lazima mrembo awe msichana,
Ili apate bwana,
wala pesa awenazo mvulana,
Mapenzi yapate kufana.
Namkumbuka Rumi Mavlana,
alisema mapenzi si kubaguana,
na wala si nani wa maana,
Hakuana aliye bora sana,
Na ndivyo ilivyo mbinguni kule kwa Bwana.
siku hizi ni kurumbana,
Uvumilivu hakuna,
kubembelezana sio tena,
Ohh!!! Mapenzi hayana maana,
Ndivyo msemavyo vijana.
Namkumbuka mzee Kenyatta na yule mama Ngina,
Nyerere na mama Maria kweli walipendana,
Mlima na mabonde vyote vya ujana,
Mapenzi yakawazidia,ishia rekebishana,
Wakapata elewana, Uzeeni kuzikana.
Siku hivi mwabomoa kila kona,
Nauliuliza sababu, eti kuzinguana,
Mapenzi hamana tena, Eti mnamegana,
Mmeacha kupendana, na sasa mnarumbana,
Mna nini nyie vijana??????
mwinjuma na Asha walishachumbiana,
Uchumba mwaka wa tatu,kila siku wagombana,
Wazazi wanataka ndoa, tena itakayofana,
Majibu wazazi wakawapa, huku wakizozana,
Bado tupo tupo sana, ...................................
Tena tunasomana,....................................
Itaendelea.
By Domokaya lisilo changua neno.
........Inaonekana kama haya mapenzi yanaendelea bado DOMO lete vitu.........
Naona umejaribu kuleta yaliyopita na kizazi kipya pamoja Bravo.
Kama kijana yule wa Clauds FM na kpindi chake cha top 20 ananikumbusha wakati ule wa RTD na MISAKATO (kama sikosei) nyimbo zinatengeneza stori nzuri ya kupendeza,mjanja sana kijana lkn ni nzuri kutukumbusha tulipotoka
Mwaka watatu mwasomana,mapenzi mnatia doa.
Elimu kwenu ilishindikana,masomo yaliwaboa.
Sasa mna tatizana,hakuna mnacho jua.
Mapenzi kuyafanya somo,huo kweli ni ujuha.
Labda yawe hisabati,mapenzi kuya kokotoa.
Mapenzi yana majedwari,kujumlisha na kutoa.
Sufwa namba witiri,kipenyo kuyatafutia.
Mabanoni mtayari,hakuna wa kuwafungua.
Mapenzi yana thamani,hata kwenye Biologia.
Hutoa viumbe hai,na vile msivyo vijua.
Kushavishana mimeani,ndege wana totoa.
Ni kuutafuta muhari,mapenzi kuyasomea.
Mapenzi yana ukweli,hata kwenye fizikia.
Myapime kwenye mizani,majibu yata wajia.
Umeme ule mapenzini,wala hauku somewa.
Ford,Newton wametii,hawa kuweza vumbua.
Kemia imesha feli,majibu haita toa.
Nyekundu kua kijani,ndio kazi jaliwa.
Nyie mwaleta utani,madawa mwachanganyia.
Wala si maabarani,au mganga kilingeni.
Mapenzi hayana ramani,kuyawakea mipaka.
Milimani na mabondini,huko kote yamefika.
Angani na aridhini,nusu kwa nusu kama ikweta.
Hiyo wote mnajua .
Jogolafia
Itaendelea
Nakaribisha maoni

Uko kamili ...
Umeona eeh........Inaonekana kama haya mapenzi yanaendelea bado DOMO lete vitu.........