Mapenzi yetu katika siasa yanatuondolea hata uwezo wa kufikiri

Beauty Eva

Senior Member
Jul 22, 2016
131
374
Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana, hasa linapokuja suala la siasa.

Mapenzi yetu katika siasa yanatuondolea hata uwezo wa kufikiri.

Tazama jambo hili:-
Majuzi, serikali ilizuia mikutano ya vyama vya siasa katika maeneo ambayo vyama hivyo havikushinda. Wapo watu wamefurahia sana jambo hilo ingawa wao wenyewe wanakosa haki yao ya kupata habari na haki yao ya kukusanyika.

Jana, tumesikia Tundu Lissu kakamatwa na Polisi. Baadhi ya vijana, wamefurahia jambo hilo kwa kuwa tu Tundu Lissu amekuwa mwiba kwa Chama chao.

Kijana wa Kitanzania yupo tayari kupoteza maslahi yake, kwa ajili ya Chama chake. Si Taifa lake

Kijana wa Kitanzania, yupo tayari na anaombea vyama vya upinzani vife au viwe dhaifu bila kujua kifo au udhaifu wa vyama vya upinzani kutapelekea nchi kusinyaa ktk uchumi, maendeleo n.k

Kijana wa Kitanzania hajui kuwa Upinzani wenye nguvu, huifanya serikali iliyopo madarakani isilale. Na kutokulala kwa serikali ni faida kwa wananchi.

Wakati wenye hekima na ufahamu bora, kila wakilala wanaombea Upinzani uzidi kuimarika, vijana wa Kitanzania waliorogwa na siasa, wanaombea upinzani ufifie, ufubae au ufe kabisa, ingawa kufifia kwa upinzani kutamuathiri katika maisha yake.

Kijana wa Kitanzania anasahau kabisa kuwa, Uhuru anaouona (wa vyombo vya habari, Uhuru wa kuongea), uwazi wa Uendeshaji serikali, uwazi wa mikataba, mgawanyo sawa wa rasilimali za Taifa vyote ni matokeo ya Uwepo wa vyama vingi.

Ndo maana ninajiuliza: Tumelaaniwa au ni umbumbumbu?
 
Kosa lako ni kuwa; Unasema "Vijana wa Kitanzania". Hivi, mtu ka yule mpayukaji wa chama, "Ole nanihii" naye ni kijana?? Sema, wanachama wa chama flani wanadhani kuwa bila upinzani hata wao watakuwepo kwenye hicho chama chao.

Naamini, chama kinaimarika zaidi kutokana na upinzani kuwepo wala si vinginevyo.

Tumuombe Mungu upinzani uimarike wala tusiufanye upinzani kuwa dhambi ya asili ambayo kila mtu ati huzaliwa nayo.
 
Mkuu ila wachunguze sana vijana ambao wanikishabikia sana ccm utagundua kati ya haya;
  1. Upeo wao kielimu ni mdogo sana na wenye uwezo mdogo mno wa kufikiri na kuchambua mambo.
  2. Kwa wale wenye 'ka-upeo' kdg wana vijimaslahi ndani ya ccm (kama vile wale wanaolipwa elfu 10)
  3. Wapo wale wanaoishi kwa matumaini kuwa watapata vyeo hasa U - DC
Watu kama hawa kwa kuwa hawana mbele wala nyuma ni sisi wanamageuzi kuwapigania ili waje waishi maisha huru na wajifahamu labda watakuja kujutia Upumbavu wao,
 
Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana, hasa linapokuja suala la siasa.

Mapenzi yetu katika siasa yanatuondolea hata uwezo wa kufikiri.

Tazama jambo hili:-
Majuzi, serikali ilizuia mikutano ya vyama vya siasa katika maeneo ambayo vyama hivyo havikushinda. Wapo watu wamefurahia sana jambo hilo ingawa wao wenyewe wanakosa haki yao ya kupata habari na haki yao ya kukusanyika.

Jana, tumesikia Tundu Lissu kakamatwa na Polisi. Baadhi ya vijana, wamefurahia jambo hilo kwa kuwa tu Tundu Lissu amekuwa mwiba kwa Chama chao.

Kijana wa Kitanzania yupo tayari kupoteza maslahi yake, kwa ajili ya Chama chake. Si Taifa lake

Kijana wa Kitanzania, yupo tayari na anaombea vyama vya upinzani vife au viwe dhaifu bila kujua kifo au udhaifu wa vyama vya upinzani kutapelekea nchi kusinyaa ktk uchumi, maendeleo n.k

Kijana wa Kitanzania hajui kuwa Upinzani wenye nguvu, huifanya serikali iliyopo madarakani isilale. Na kutokulala kwa serikali ni faida kwa wananchi.

Wakati wenye hekima na ufahamu bora, kila wakilala wanaombea Upinzani uzidi kuimarika, vijana wa Kitanzania waliorogwa na siasa, wanaombea upinzani ufifie, ufubae au ufe kabisa, ingawa kufifia kwa upinzani kutamuathiri katika maisha yake.

Kijana wa Kitanzania anasahau kabisa kuwa, Uhuru anaouona (wa vyombo vya habari, Uhuru wa kuongea), uwazi wa Uendeshaji serikali, uwazi wa mikataba, mgawanyo sawa wa rasilimali za Taifa vyote ni matokeo ya Uwepo wa vyama vingi.

Ndo maana ninajiuliza: Tumelaaniwa au ni umbumbumbu?
Kama nimemuelewa vizuri mleta uzi, ni kwamba tupo watu ambao tupo tayari kulikata tawi la mti linalotupa support. Au pia tupo tayari kuking'ata kidole kinachotulisha.
 
Alionya mwalimu nyerere katiba yetu inaruhusu udikteta kama angetaka kuwa dikteta angeweza. Kosa tulilolifanya ni kuiacha itumike mpaka sasa imekutana na dikteta halisi.
Ngoja tuisome namba kwanza tupate akili ya kuibadilisha. Tulikuwa hatujui madhara yake sasa tujionee wenyewe kisha tuseme HAPANA.
 
upinzani si matusi, siasa si hasira za kufutiwa posho na kuzuhiliwa bungeni uanze kutumia lugha za kejeri, kudharau serikali, tukuchekeee tu.

Serikali kama ikikubali shenzi ya leo basi ikubali na pumbavu ya kesho. Ni Tanzania pekee ndo watu uchwara kama Lissu wanatoa matusi hadharani, na wahuni wenzao wakawasapoti
 
Hakuna cha kulaaniwa wala kurogwa!

Kunyimwa elimu nzuri ndo kunasababisha haya yote, eti kusoma na kuandika ndo elimu ya msingi? Msingi gani huo? Hakuna sehemu ambapo Mtanzania anafundishwa kuwa mzalendo na kuipenda nchi yake. Sisi tuliosoma zamani tulikuwa tunakaririshwa mambo ya ajabu kwenye somo la Siasa.
Mtu yeyote asiyekuwa na msingi mzuri wa elimu hata siku moja hawezi kutafakari lolote na kutoa majibu sahihi. Mbinu hii ya kuwanyima watanzania elimu bora ndo msingi wa CCM kwani wanaamini kwamba majority hawajitambui, wanaojitambua ndo wanabughudhiwa hili wale wasiojitambua waogope kujitambua na kudai haki zao.
 
Back
Top Bottom