Mapenzi yashanikera

Status
Not open for further replies.

mdau mpya

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
474
651
Wasalamu wana MMU!

Ningependa kushare nanyi hii mambo mana hata siielewi kabisa.Ni hivi kuna binti mmoja nilikuwa na uhusiano nae mwaka 2014 wote tukiwa chuo. Sasa baada ya sintofahamu nyingi sana uhusiano wetu ukakata mara baada ya kujilidhisha kuwa ana mpenzi mwingine. Ishu ilikuja baada ya takribani miezi minne mara baada ya kuachana akanijulisha eti ana mimba yangu na kulia sana kwamba haitoi ila nijue hilo. Aisee alinichanganya kichwa sana, nikajitafakari nikarudiana nae kwa ajili ya kunusuru mtoto asijepata shida ila cha ajabu nilipekua simu yake na kuona anachart na mwanaume mwingine kuhusu hiyo mimba, to be honesty from there nilimuona kama sio mtu mzuri kwangu nikamwambia siyo mimba yangu na haiwezekani awe na mimba yangu at the same time anachati na mtu mwingine kuhusu huyo mtoto atakae zaliwa.

Baada ya muda wa takribani mwaka hivi nimekuja kuonana nae hamadi bin vuuu, akaniletea fujo sana kuwa nilimtelekeza yeye kajifungua bila msaada wangu, niliishia kumuangalia tu. kibaya zaidi alichukua begi langu na laptop kapeleka kwao eti nikachukue nimuone na mtoto nikatia mgomo hata sikwenda. Baada ya masuluhisho mengi sana, ndug zangu wakakubali kuwa watamlea mtoto japo mimi nilitia ngumu simchukui mpaka nipime DNA.

Sasa hii juzi kamaliza mitihani, tukakutana kujadili hili pamoja na ndugu zake na wangu, na muafaka ulikuwa nisaidie kumlea mtoto ili asipate shida na masomo, kishingo upande nikakubali. Sasa nilienda kwake kama baba mtoto, sasa unajua haya mambo hayaishagi hivihivi nikajiona nalala hukohuko.

Asubuhi wakati naamuka nikachukua simu yake, hapa ndio maluelue yalipo anza..kumbe yule jamaa aliyavunja uhusiano ndio mwenye mtoto na anamuhudumia kila kitu kutoka pango mpaka chakula cha mtoto. nikasema isiwe shida nikachukua # yake nilipomcheki alidai huyo mtoto ni wake na ana mupa kila kitu ila kwa kificho mkewe asijue, niliishiwa nguvu aisee. Nikarudi tena mchana pale getoni kwake nikamkuta jamaa kampakata mtoto, sikuamini ikabidi nivunge mi kama rafiki ake huyo mama mtoto wake kama intelijensia nikachukua document za mtoto hapa ndo niligundua ninapressure mbaya sana.

Sikuwa na namna nikaondoka kuitafuta bar yoyote nipate hata ka castle lager kabaridi kanipunguzie pressure. Nikamtumia text asinijue kamwe, sina haja ya DNA alivojifanya mjuaji kanidanganya kuwa eti yule ni classmate wake.

Nahisi Dunia sio yangu nashindwa hata la kufanya, sihitaji ushauri nawashirikisheni tu nimeandika kwa akili za Dompo, kama nimeikosea nitaiedit kesho.

Jamani usiku mwema.
 
Nimeipenda 'Disclaimer' yako kua umeandika kwa akili za Dompo.

Haya,pombe njema. Ukiamka kesho nenda kasali then mpigie simu mwambie ashike adabu yake na wewe shika adabu yako uwe na misimamo kama kidume. Huu sio ushauri (hukutaka ushauri), hii ni amri nikiwa kama kaka yako!
 
historia yako inafanana na jamaa mmoja hv hko homblo Dodoma,,,ila pole sana
 
Nimeipenda 'Disclaimer' yako kua umeandika kwa akili za Dompo.

Haya,pombe njema. Ukiamka kesho nenda kasali then mpigie simu mwambie ashike adabu yake na wewe shika adabu yako uwe na misimamo kama kidume. Huu sio ushauri (hukutaka ushauri), hii ni amri nikiwa kama kaka yako!
Ha haaa... Kaka mkali
 
Siku hizi kuambiwa mimba yako iz very simple kumbe ana mgegedo kwa pembeni, pole mkuu kunywa maji mengi uwe kama Ray ili usisingiziwe mimba tena.
 
mie mwenyewe yaliwahhi ntokea .......omba Mungu usahau .................. ila jua life goes no matter what
 
Haujakosea mkuu, lakin nafurahi kuona mapenz hayajakutawala, you are still strong no matter what.
 
Daaah!! Hii stori kidogo ifabnane na yangu, nakumnuka 2014 niko mwaka wa mwisho chuoni milikuwa na demu ambaye kwa mda wa miezi mitatu hatukuwa pamoja, yeye alisafiri kwenda kwao, halafu alivyorudi dar hakunijulisha, siku moja nikapiga simu akapokea na nikagundua kuwa huyu hayuko mkoani atakiluwa hapa dar, nilpomuulza kama yuko dar akakubali akadai kaja ghafla kwa usafiri wa mjomba wake.

Basi nikamwambia njoo basi kwangu, akaja duuu!! Mtoto kapendeza balaa, anatia viwalo ile mbaya na nikampenda zaidi kwani awali hakuwa hivyo.

Basi mda wa usiku umefika mi nacheki naona kama kanenepa kweli maana alikuwa na shepu matata.

Kabla ya kugegedana akaniambia ni mjamzito wa miezi minne, babake niliwaza balaa kumuuliza akasema eti hakujua kwani alikuwa anaendelea kupata siku zake kama kawaida so hakutambua mapema.

Nilimfukuzia.mbali nikamwambia mimi na wewe tena basi nenda kwa huyo alokupa mimba. Aliondoka kama baada ya miezi saba hivi alinipigia eti kajifungua mtoto wa kiume nikampogeza tu simu nikakata na namba nikafuta tena.

Hadi leo mwaka na nusu sasa hajanitafuta tena.

Nilijaribu kuikubali ile mimba lkn nikashindwa
 
MKUU NIMEFURAHI INAONEKANA HII ISHU WENGI TUWAHANGA..
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom