Mapenzi yanatesa

Mapenzi yanatesa

Wakati wengine tunaumiza kichwa hela ya kodi ya gheto huku kuna chali anajifunza maana ya mapenzi
 
Hodi humu ndani nakuja kwa kishindo kama [emoji233] lakini na huzuni kama [emoji212] cha kuku kilichoachwa na mamaye.
Kama kawaida nianze na hiki kitu kinachonisibu hadi sasa.

Kuna ex wangu ambaye nilimtongoza akakubali kuwa nami katika mahusiano, yapata miezi kama mitatu sahizi tupo katika mahusiano.

Japo hatujawahi kufanya mapenzi mimi na yeye, kuna wakati huwa namwambia kuhusu swala la mapenzi ananiambia nafasi ya kutoka pale nyumbani ndo ishu, vilevile anaachiwa watoto pale home.

Japo ni beki tatu anabanwa sio mchezo

KISA CHENYEWE NI HIKI

Juzi nipo matembezi na binti mmoja ambae tunajuana kama rafiki yangu, tukiwa tunapiga story nikiwa namsindikiza kwenda kwao yule binti.

Mara paap huyu ex wangu akawa kapita akatuona tukiwa pamoja japo Ilikuwa mida ya saa moja jioni kigiza kikiwa tayari kimetanda lakini alinijua.

Basi wakati huo huo nikawa nimemuaga yule sister nikarudi zangu kuja kumsubiri huyu ex wangu.

Baada ya kumuona nilimuita lakini alionyesha hali ya kutofurahia wito wangu nilimsihi asimame nimwambie kitu alisimama.

Nikamfuata nikamuongelesha lakini niliona tofauti na nilivyomzoea ndo nikamwambia au umechukia ulivyoniona na yule binti?

Akawa hatoi majibu ya kuridhisha basi mimi nikamwambia ukweli kuwa mimi wala sina mahusiano na yule binti, nilimbembeleza vya kutosha lakini hakunielewa nikaamua kumwacha.

Leo asubuhi nimemuona maeneo nikamzukia lakini cha kushangaza haniamini ninachomwambia na akaniambia eti kuwa mimi nina wapenzi wengi.

Eti wengine huwa nawasiliana nao kwenye simu ambapo si kweli, sasa mi nashindwa kuelewa ana maana gani au ndo anataka kunitema? Yaani hataki kuniamini nacho mwambia kuwa si kweli.

Aisee imeniuma sana. Msaada tafadhali waungwana. Nipo njia panda [emoji42][emoji7][emoji7]
Mkasome
 
Una miaka mingap kwanza maana mapenzi kama hayo wanayo under 20
 
Mbembeleze beki tatu ongea nae kwa upole akikuelewa mwambie akutunuku penz walau siku moja tu.
Mpe shoo ya kibabe then mwache atakuwa anakutafta mwenyewe, ikishindikana piga chini tafta kifaa kingine
 
Back
Top Bottom