Mapenzi ya kweli bado yapo.

Mapenzi ya kweli bado yapo.

Simara

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
7,561
Reaction score
23,991
Habari wanabodi, leo nilikua nasoma uzi flani hivi ukanikumbusha miaka kadhaa nyuma.

Kipindi tupo chuo mwaka wa pili, room mate alikutana na mkaka mmoja hivi katika kuelezana unakaa wapi na unafanya kazi gani, yule kaka akasema yeye ni boda boda....basi bibie baada ya muda flani wakaanza date na yule kaka.

Basi kama kawaida ya wadada tukawa tunashangaa tu mbona kakutana na watu wengi wenye wadhifa lakini kawakataa kamkubali bodaboda ila msimamo wake ilikua ni anampenda yule kaka.

Baada ya miezi 6 yule kaka akaja kumuambia ukweli yeye sio boda boda ni mhasibu mkuu ofisi flani hivi ya serikali, na alimuambia vile ili kumtega kama kweli anampenda.

Now wameoana na wana watoto 2 na wanaishi kwa furaha na amani kwenye ndoa yao.

Kaka zangu wanawake wenye mapenzi ya dhati bado wapo, huwa nikisoma humu comments mbali mbali naona wanaume wengi hawaamini kama bado kuna wanawake ambao fedha kwao sio kipaumbele.
 
Mhu...Dada aliona mbali.Siamini kama walikutana barabarani pengine mahali wamekaa hivi.Kijana kapendeza,wallet imejaa ana maneno mazuri,akili na busara yani output yake ukilinganisha na ya bodaboda unaona hapanaaa...atakuwa ananitania.
 
Mhu...Dada aliona mbali.Simini kama walikutana barabarani pengine mahali wamekaa hivi.Kijana kapendeza,wallet imejaa ana maneno mazuri,akili na busara yani output yake ukilinganisha na ya bodaboda unaona hapanaaa...atakuwa ananitania.
Ilikua njiani tunatoka kula, halafu yule kaka yupo simple mnoooo. Hata akitokea sasa hivi akikuambia yeye ni konda utaamini.
 
Nakwambia sio rahisi.Pengine kwa bahati tu aliona japo kitambulisho.
Kwani alitongozwa dakika hiyo hiyo akakubali dakika hiyo hiyo?
Mapenzi hayachagui lakini
Hapana hakuona, kwanza huyu binti mwenyewe ni wale wasio na makuu mambo ya simu za gharama huyu kaka ndiyo alimuanzishia yeye kumnunulia, unajua kuna watu wana hela ila jinsi wanavyojiweka huwezi kuwajua... ndiyo huyu kaka alivyo.
 
Kaka zangu wanawake wenye mapenzi ya dhati bado wapo, huwa nikisoma humu comments mbali mbali naona wanaume wengi hawaamini kama bado kuna wanawake ambao fedha kwao sio kipaumbele.

Hadi leo naamini hivyo maana sijawahi kuona wanawake wa mapenzi ya dhati.

Kila wanapoona pesa hawachoki kusumbua na kurukwa akili.



Acha tuendelee kuzitafuta aiseeh
 
Hapana hakuona, kwanza huyu binti mwenyewe ni wale wasio na makuu mambo ya simu za gharama huyu kaka ndiyo alimuanzishia yeye kumnunulia, unajua kuna watu wana hela ila jinsi wanavyojiweka huwezi kuwajua... ndiyo huyu kaka alivyo.
Kumbe na yeye ndo walewale wa kununuliwa!
 
Probability hiyo.

Hata huyo mdada nahisi alishtukia mchezo mapema kuwa anadanganywa jamaa ni boda boda.


Pua ya mwanamke inanusa harufu ya pesa hata ukijificha.
Kweli watu hamna imani na kwa style hii mtakua hampati hao wanawake wenye mapenzi ya kweli wasioangalia pesa...sababu hata nyie hamjiamini
 
Hata mimi nilikuwa siamini ila sasa hivi kidoogo naanza kuamini...
*siombei mabaya ila huyu akiendelea hivi basi atakuwa mke wangu wa ndoa hasa, she is simple and real.

ananifanya hata mm niwe real na nijiamini zaidi...
Wapo mkuu, Mungu awasimamie
 
Back
Top Bottom