Tetra
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 1,526
- 771
::
Rafiki anamsaliti rafiki yake,
Shost anamsaliti kwa shost wake,
Mume anamsaliti mkewe,
Mke analipiza kwa alivyosalitiwa,
Mapenzi uwanja wa fujo Kama huwezi kaa pembeni.
::
Kijana anampenda binti,
Anamweleza wanakubaliana,
Bosi anamtamani binti huyo huyo,
Pesa inatumika binti anabadili mawazo,
Kijana anashinda analaumu Analia wee!
Unalia nini sasa ee? Kama kizuri huli peke yako,,unasikia kijana
Mapenzi uwanja wa fujo kama huwezi kaa pembeni.
::
Binti anampenda kijana kwa dhati kabisa,
Kila anachoomba anapewa,
Kijana kuona anapendwa bichwaa hiloo!
Anafanya anavyotaka,
Anamsaliti maana anaona amekolea.
Baadae binti anamwagwa tena kwa kashifa,
Binti analia eti anataka kujiua.Wee! Binti wee! Nani kakuambia huyo ni Mungu wako?

House girl analilia ka kibarua,ametoka bush,
Akipewa ka blue band na chai ya moto,anaanza nenepa na kupendeza.
Lakini anamtamani Baba mwenye nyumba
Ili kurahisisha mambo anamtafutia mizizi,
dozi 7 kutwa mara 3
Baba anauingia mkenge,Mama anatimuliwa Housegirl ndiye Mama wa amamu mpya,
We Mama wewe uliyepoteza ndoa,
akili kumkichwa! Ohoo!

Huyu ametendwa,,
Amemfumania mwenzi wake Mara gesti,Mara home,
Alishatendwa mpaka kawa sugu! Ana uzoefu wa kutendwa,
We nae kichwa kichwa! Unamvaa,,Anakutenda Anakutenda hadi hasira zimuishie! We nae kutwa unalia tu,,oo! Amerogwa! Ni wivu wa watu.
Kaa kimya wewe Unajua background yake?
Mapenzi uwanja wa fujo kama huwezi Kaa pembeni.
::
Ona huyu nae! Kakutana na mwenzake,amempenda hasikii wala haelewi,Mbio mbio hata bila kufikiri..ndoa
Mara Kumbe mwenzake ana watoto Na kila mtoto ana baba au mama yake.Anaanza kulia "mbona hukuniambia" akuambie ye mjinga!
Mapenzi uwanja wa fujo Kama huwezi kaa pembeni
::
Huyu nae Kutwa analilia ee Mungu nipe mwaminifu.
Oo! Kapata binti mrembo wa haja,
Kazama haswaa, watu wanaomjua wanamshangaa! Ye katoka town kaja bush Ye mjuaji,,
Kumbe mrembo mwenyewe kashatoa mimba 9 na anaishi kwa matumaini

Haka nako Kila mwanaume Kanamvulia,
Kana dhani real love ni ngono.
Akiambiwa anapendwa hajui kukataa,Mara Mimba hiyoo! Anaachwa Maana vijana nao wakijua binti ni wa wote,,wanamshughulikia hadi thamani inaisha.
Subiri utaolewa na asiyekujua tena bora uhame,
Shukuru umepata mimba ungepata Li Ukimwi?

=