Mapenzi, uhusiano na Imani

Mapenzi, uhusiano na Imani

iMind

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,230
Reaction score
5,525
Hapa duniani maisha yetu ya kila siku tunayaendesha kwa kufuata miongozo au mapokeo kutoka katika makabila yetu (utamaduni), dini na pia kutoka kwa jamii au watu wanaotuzunguka (utandawazi).

Swala la dini, au imani za dini zimekuwa zikitutatiza sana katika maisha yetu ya kila siku hasa ya kimapenzi na uhusiano. Mimi ni mkristo hivyo nitaongelea imani ya kikristo, kwa sababu ndo naijua. Sasa hivi kumekuwa na madhehebu mengi ya kikristo huku manabii na wachungaji wakiibuka kila siku. Kimsingi kwa mtatazo wangu jamii imekuwa confused kwa sababu kila mchungaji, nabii anahubiri kwa namna anavyojua au kwa mtazamo wako. Mimi huwa najaribu kusoma, kuwasikiliza na mwisho wa siku natafakari na kuchukua mkondo ambao naona unafaa.

Katika imani, naamimi kuwa hakuna dhambi ndogo wala kubwa. Dhambi ni dhambi tu na hukumu ya mungu iko kidigitali zaidi, yaani ni 0 au 1 hakuna katikati. Na dhambi maana yake ni kutenda kinyume ni amri za mungu. Katika biblia kuna amri 10 ambazo mungu ametupa, tuishi kwa kuzifuata. Ni amri 10 rahisi kabisa ambazo ukizifuata pepo ni halali yako. Cha ajabu binadamu tumeziongeza na kuwa na amri zaidi ya 30.

imefika hatua hadi baadhi ya wachungaji wanahubiri eti kufanya mapenzi kwa style fulani ni dhambi. Eti style ya kifo cha mende ndo halali...mweee. sijui wanayapata wapi haya.

Katika mapenzi sisi wakristo tuna masuala kadhaa ambayo tunaambiwa ni dhambi na yamekuwa yakiwafanya watu wengi kuishia kuishi kwa shida wakiogopa kutenda dhambi kama ifuatavyo;

1. Kuachana katika ndoa.
Katika amri 10 za mungu hakuna amri inayokataza watu kuachana. Lakini wakristo wengi wamekuwa wakiishi katika ndoa ambazo zimegeuka kuwa ndoano kwa sababu wanaogopa kuachana. Ndivyo walivyofundishwa kwamba kuvunja ndoa ni dhambi, ingawa mungu hakusema hivyo katika amri alizotupa. watetezi wa hoja hii wana nukuu kifungu fulani kwenye biblia mbacho yesu alitamka kuwa 'alichokiunganisha mungu, mwanadamu asikitenganishe". lakini katika biblia hiyo hiyo Yesu alimwambia mtu mmoja aliyemuuiliza afanye nini ili apate ufalme wa mungu kwani amekuwa akifuata mari zote za mungu, Yesu akamjibu 'Uza kila kitu ulichonacho halafu unifuate". Kama ni kufuata kile kitu yesu alichosema au kilichoandikwa katika biblia basi tufuate na hili. Hii ni mfano mmoja tu wa maneno ya yesu ambayo yatuyafuati, yako mengi. Wandugu, kuachana siyo dhambi kama unaona ndoa yako ina matatizo get out of it freely. Kuachana bila sababu ya msingi siyo ustaarabu. Pima na amua

2. Kuoa mke zaidi ya mmoja.
Kuoa mke zaidi ya mmoja si dhambi kwa sababu katika amri zote 10 hakuna inayokataza hivyo. Amri inasema usitamani mwanamke asiye mkeo. Mungu hapa nawaambia wanaume wasitamani wake za watu. Mungu hakuwaambia wanawake wasitamani wanaume wasio waume zao, kwa sababu alijua mwanamke anaweza kuolewa na mwanaume hata kama tayari mwanaume huyo ameoa, ila mwanamke hawezi kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja ndo maana mwanamke akishaolewa ni dhambi kumtamani achilia mbali kuzini naye. Kwa tamaduni za wa afrika wengi swala la kuoa mke zaidi ya mmoja ni halali. Lakini kwa mtazamo wangu siyo ustaarabu kuoa mke zaidi ya mmoja. Ila ni vyema ukao mke wa pili, wa tatu n.k kuliko kuwa na nyumba ndogo. Maana nyumba ndogo ni dhambi na pia siyo ustaarabu, kuoa mke zaidi ya mmoja siyo dhambi ila siyo ustaarabu. Pima na amua.

3. Mapenzi ya jinsia moja.
Kanisa la anglican linafungisha ndoa za jinsia moja. wengi walishangaa na uamuzi wa kanisa la anglican kuruhusu ndoa za jinsia moja. Wanajua siyo dhambi ndo maana wanafanya hivyo. Haikukatazwa kwenye kwenye amri 10 za mungu. Hapa watu wanaongozwa na mapokeo na utamaduni zaidi kuliko amri za mungu. Mapenzi ya jinsia moja ni ruksa kwa mujibu wa mungu.

4. Mapenzi kinyume na maumbile.
Kuna siku nilisikia dada mmoja akisema 'Huo mchezo ziwezifanya kabisa ni dhambi KUBWA SANA, yaani mungu hapendi kabisa'. sasa nikajiuliza, haogopi kuzini kitu ambacho mungu amekataza, lakini anaogopa kinyume na maumbile wakati hata mungu hajakaza. Mwee. Do it freely for your pleasure, at your own risks.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Mtoa mada, naona kuna mahali kama umekariri vile, kwanza kabisa jamii haijawa 'confused', labda wewe ndio uko confused na unachoamini.

Pili, kutumia biblia kama wakristu haimaanishi tunaamini katika kitu kimoja, na kinachotutofautisha ni tafsiri ya biblia hiyo. Naona unasema ni sawa watu kuachana kwa ndoa za kikristu, inaweza kuwa sawa kwako kulingana na tafsiri ya ndoa ya dhehebu lako, lakaini haimaanishi wakristu wote wanaona hilo katika mtizamo mmoja.

Tatu, hii mada iende jukwaa la dini, maana imejikita katika mtizamo wa mahusiani na ukristu, waislam watachangia nini? Vinginevyo ungeweka general tu kuonesha nafasi ya dini katika mahusiano.
 
Kwa hiyo mwandishi unamaansha kuwa fundisho kuu katika biblia ni amri za Mungu tu? Nazidi kuamini wakristu tunaamini vitu tofauti sana, anyway kama inatusaidia kuishi kwa amani zaidi hakuna mbaya.
 
kutumia fake id raha sana mtu unaongea lolote unalojisikia.
 
hahahahahaha....mkuu, na wewe ni nabii nin?? Maana skuhzi mnaibuka wengi kweli.
 
Hebu fikiria kama watu wafanyapo mapenzi kila bao lingekuwa na mlio kama wa risasi paaaa! Je usiku tungelala kweli?,Si ingekuwa kelele tu kwenye mapaa ya nyumba zetu. Huku paaa! Kule paaa!,paaa! Mhh, bora hii ya kimya kimya...Maana kwenye gesti ingekuwa kama Libya enzi za Kanali Gadaffi....!
 
Kwa hiyo mwandishi unamaansha kuwa fundisho kuu katika biblia ni amri za Mungu tu? Nazidi kuamini wakristu tunaamini vitu tofauti sana, anyway kama inatusaidia kuishi kwa amani zaidi hakuna mbaya.
Nachosema kutenda dhambi ni kutenda kinyume na amri za mungu. ambazo ziko 10. Haya mengine yote kama mungu angetaka tusifanye pia yangekuwa kwenye amri 10.
 
Mtoa mada, naona kuna mahali kama umekariri vile, kwanza kabisa jamii haijawa 'confused', labda wewe ndio uko confused na unachoamini.

Pili, kutumia biblia kama wakristu haimaanishi tunaamini katika kitu kimoja, na kinachotutofautisha ni tafsiri ya biblia hiyo. Naona unasema ni sawa watu kuachana kwa ndoa za kikristu, inaweza kuwa sawa kwako kulingana na tafsiri ya ndoa ya dhehebu lako, lakaini haimaanishi wakristu wote wanaona hilo katika mtizamo mmoja.
.
Wakristo wote tuna aamini kitu kimoja. Ingawa tunatofautiana katika taratibu za uendeshaji wa ibada zetu, taratibu za maisha na miiko mbalimbali. Ni seme tu, ni utaratibu wa kawaida kwa jamii fulani kujitengeezea miiko na masharti na kujiwekea utaratibu wa kuwaongoza katika masulua mbalimbali ya kimaisha. Ila hiyo miiko, utaratibu na masharti ni lazima usivunje sheria kuu (Katiba) au kwa wakristo Biblia.

So my point is, hivi vitu nilivyoviongelea viko kwenye miiko ya jamii mbalimbali na dini mbalimbali na siyo amri ya mungu. Kwenda kinyume na miiko ni kosa lakini siyo dhambi.
 
Ndugu mleta mada.

Tatizo lako ni kubwa sana kwa sababu umekariri badala ya kujikita kwenye uhalisia wa kile kinachozungumzwa kwenye biblia.Isome vizuri biblia na utagundua kuwa pamoja na Musa kupewa amri kumi,lakini biblia hiyo hiyo inatuambia kwamba,amri kuu kuliko zote ni upendo.Je,upendo imetajwa kwenye amri kumi?,bila shaka hapana.La msingi tunahitaji kuwa na tafsiri pana sana kuhusu amri za Mungu.Ukisoma maandiko,miji ya Sodoma na Gomora iliteketezwa na kuangamia kwa sababu ya matendo maovu likiwemo la matendo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.Mungu hakuwa -------- kuumba mwanadamu na kumpa njia ya haja kubwa na ndogo,matumizi ya kila kiungo yameanishwa.Kuhusu suala la wake wengi,si kweli kwamba ni ruhusa,amri zinataja mke na wala si wake.Usipende kusoma biblia na kuwa na gramatical interpretation.U need to apply liberal approach na kuyaangalia mazingira tuliyonayo.Nani kakuambia mwenye wake wengi hatoki nje ya ndoa??!!
 
Prove this

Sawa mimi nimekariri. Je wewe ambaye hujakariri unawweza kuniambia ni kigezo gani kanisa la England walitumia kuruhusu ndoa za jinsia moja? Au wewe ndo unajua sana biblia kuliko wao?
 
Mi namuunga mkono mtoa mada.

Hivi vinabii feki vinatuchanganya tu.

Katika amri za Mungu hakuna alipotuambia tusinywe Guiness beer au tusikamate makalio ya wahudumu kama Joyce na Rehema. Chapchap sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom