Nalendwa
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 7,466
- 13,031
Baadhi ya waathirika wa mapenzi ya uonevu wengi wao wakiwa wanawake, huwa na tabia ya kuwarudia wapenzi wao waliowapiga au hata kuwaumiza kabisa bila kujali matokeo ya mahusiano hayo mabovu. Ni suala ambalo wengine tumekutana nalo katika maisha.
Hawa ni baadhi ya wanawake wa jinsi hiyo. (Majina yamebadilishwa)
Kate.
Ameishi na boyfriend wake kwa miaka 5 na wana mtoto mmoja. Boyfriend kamchapa mara kadhaa na hata kumuumiza lakini Kate anashindwa kumwacha. Kila akijaribu kumwacha, boyfriend huja na maneno matamu na Kate huingia kingi na kuamua kuendelea nae.
Hawako pamoja sasa baada ya boyfriend kumkasirikia Kate na kuondoka, kisa Kate kabeba mimba ya pili. Na baada ya boyfriend kuondoka Kate kaanza kumtafuta..
Hollo.
Hollo ameolewa na mumewe karibu miaka 10 na watoto 3. Mume ni mpigaji haswa akilewa, lakini Hollo pamoja na kupigwa mara kadhaa, kati ya hizo mojawapo akiwa mjamzito mpaka kulazwa, hataki kumwacha mume pamoja na kushauriwa mara kadhaa.
Baada ya kujifungua mtoto wa pili Hollo alivyorudi nyumbani toka hospitali, mume alimlazimisha Hollo kufanya tendo la ndoa, kitu kilipelekea Hollo maumivu makubwa na kuchelewa kupona kizazi. Hollo ndo kwanza anajiachia facebook na mumewe kipenzi.
Wenye kujua tatizo na wana Saikolojia, nini kinapelekea Victims hawa kurudi kwa Abusers wao?