Mapenzi ni maigizo na mwenye script ndefu huachwa

Mapenzi ni maigizo na mwenye script ndefu huachwa

Hivi ushawahi kujiuliza kwanini ulivyoachwa uliumia? "Nilimpenda sana yule kaka" Najua jibu litakuwa ilo au kufanana na ilo. Ila ukweli ni kwamba unajipenda wewe ndio maana unaumia kwa kukosa hitaji la moyo wako.

Nnavyojua tuwapendao huwa tunahakikisha wanapata vitu wavipendavyo, sa wewe unaumia nini kwa yule demu kumpata ampendae? 😀 😀 😀 😀 😀

Back to the topic. Tofauti ya movie ya mapenzi na movie zingine ni kwamba hii washiriki ni wawili tu alafu kila mmoja anakuwa na script yake kichwani. Na kati ya hao wawili mwenye script ndefu ndio atapigwa chini.

Unatongozwa leo, after a week unalegeza na kumkubalia, mnadate for 3 months jamaa anaamua kuamsha, huku nyuma unaanza kulia full kulaani kwamba amekuchezea.

Unasahau kuwa kosa sio lake, ukweli ni kwamba katika igizo lake script yake ilikuwa scenes ambazo ni za miezi mitatu tu, bahati mbaya yako ilikuwa ndefu sana na haukupanga iishe hivyo (hiyo ni yako sio yake).

Wengine scripts zao huwa ndefu kweli kiasi kwamba kuna scenes zinahusu ndoa, wanafika hadi church. Wanafunga ndoa. Few years after marriage kuna mmoja script yake inafika mwisho, scenes zinaisha. Hapo ndio ndoa huanza kuwa na mifarakano, ugomvi wa hapa na pale hatimae divorce.

Ila wale wachache ambao scripts zao ni ndefu kuliko ISIDINGO ndio huwa tunasikia wamehadhimisha jubilei ya miaka 10,15,50 n.k ya ndoa. Na hao sio kwamba huwa hawagombani, wanatibuana sana sema kila mmoja akiangalia number of scenes zilizobaki kwenye script yake anaamua kuwa mpole, wanasolve mambo yao.

Ukitaka kujua kuwa mapenzi ni maigizo kwa asilimia kubwa, we angalia watu wakitengana/ kuachana hapo ndio utaona ni jinsi gani moyo wa mtu ulivyo msitu. Chukulia mfano kina Mbasha au huyu DC anayesema anajishangaa kwanini alimpendaga yule mwanamuziki.

Humu kila siku watu wanalia hadi unawaonea huruma, wengine wanafikia hata stage wanasomesha wapenzi wao. Yani wanachukua majukumu ya wakwe zao ili mradi kuonesha mapenzi, ila at the end of the day story zao tunaziskia mara kwa mara humu. Yani hata umpeleke chuo, siku script yake ikifika mwisho what you have done to her won't stop her from leaving.

Au hujawahi kusikia ile story ya yule professor wa UDSM ambae after few years of marriage alimpeleka mkewe USA kujiendeleza kielimu, mke baada ya kumaliza masomo anasema mimi Tanzania sirudi, kama unanipenda njoo huku tuendeleze familia.

Yani hapo ulipo wewe na huyo mpenzi wako haijalishi anasema anakupenda kiasi gani au wewe ni jinsi gani unajitahidi kumuonesha kuwa unampenda, siku scenes zake zikiisha tu broh jipange.

MSISEME HAMKUAMBIWA.

Analyse
Hio akili ya mke wa Proffessor ni sawa na akili ya mke wangu kabisa. Najua siku ntakayompeleka ulaya tu harudi wacha aendelee kusoma humu humu kwenye vyo vya kata.😅😅😅
 
Hio akili ya mke wa Proffessor ni sawa na akili ya mke wangu kabisa. Najua siku ntakayompeleka ulaya tu harudi wacha aendelee kusoma humu humu kwenye vyo vya kata.[emoji28][emoji28][emoji28]
Wakishavuka boda hawataki kurudi [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Kuna mmoja hata hatudate ila nampenda mpaka nikiona message yake nato mchozi. Nikimuona ndo najisikia kuzimia kabisa. Umenifanya niwaze tukianza kudate ukite script yake ni ya scene za week 3 si nitakufa mimi
Hahahah week 3 nyingi! Siku 7 tu 😅😅😅 bora hata mimi yangu miaka 50!
 
Ndio maana siku hizi najitahidi script zangu ziwe fupi kama mizengwe!
 
Script yangu ilikua ya mpaka kifo wakati mwenzangu ana script ya miaka mitano tu[emoji23]
 
Back
Top Bottom