Mapenzi ni maigizo na mwenye script ndefu huachwa

Mapenzi ni maigizo na mwenye script ndefu huachwa

Analyse

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
17,639
Reaction score
47,716
Hivi ushawahi kujiuliza kwanini ulivyoachwa uliumia? "Nilimpenda sana yule kaka" Najua jibu litakuwa ilo au kufanana na ilo. Ila ukweli ni kwamba unajipenda wewe ndio maana unaumia kwa kukosa hitaji la moyo wako.

Nnavyojua tuwapendao huwa tunahakikisha wanapata vitu wavipendavyo, sa wewe unaumia nini kwa yule demu kumpata ampendae? 😀 😀 😀 😀 😀

Back to the topic. Tofauti ya movie ya mapenzi na movie zingine ni kwamba hii washiriki ni wawili tu alafu kila mmoja anakuwa na script yake kichwani. Na kati ya hao wawili mwenye script ndefu ndio atapigwa chini.

Unatongozwa leo, after a week unalegeza na kumkubalia, mnadate for 3 months jamaa anaamua kuamsha, huku nyuma unaanza kulia full kulaani kwamba amekuchezea.

Unasahau kuwa kosa sio lake, ukweli ni kwamba katika igizo lake script yake ilikuwa scenes ambazo ni za miezi mitatu tu, bahati mbaya yako ilikuwa ndefu sana na haukupanga iishe hivyo (hiyo ni yako sio yake).

Wengine scripts zao huwa ndefu kweli kiasi kwamba kuna scenes zinahusu ndoa, wanafika hadi church. Wanafunga ndoa. Few years after marriage kuna mmoja script yake inafika mwisho, scenes zinaisha. Hapo ndio ndoa huanza kuwa na mifarakano, ugomvi wa hapa na pale hatimae divorce.

Ila wale wachache ambao scripts zao ni ndefu kuliko ISIDINGO ndio huwa tunasikia wamehadhimisha jubilei ya miaka 10,15,50 n.k ya ndoa. Na hao sio kwamba huwa hawagombani, wanatibuana sana sema kila mmoja akiangalia number of scenes zilizobaki kwenye script yake anaamua kuwa mpole, wanasolve mambo yao.

Ukitaka kujua kuwa mapenzi ni maigizo kwa asilimia kubwa, we angalia watu wakitengana/ kuachana hapo ndio utaona ni jinsi gani moyo wa mtu ulivyo msitu. Chukulia mfano kina Mbasha au huyu DC anayesema anajishangaa kwanini alimpendaga yule mwanamuziki.

Humu kila siku watu wanalia hadi unawaonea huruma, wengine wanafikia hata stage wanasomesha wapenzi wao. Yani wanachukua majukumu ya wakwe zao ili mradi kuonesha mapenzi, ila at the end of the day story zao tunaziskia mara kwa mara humu. Yani hata umpeleke chuo, siku script yake ikifika mwisho what you have done to her won't stop her from leaving.

Au hujawahi kusikia ile story ya yule professor wa UDSM ambae after few years of marriage alimpeleka mkewe USA kujiendeleza kielimu, mke baada ya kumaliza masomo anasema mimi Tanzania sirudi, kama unanipenda njoo huku tuendeleze familia.

Yani hapo ulipo wewe na huyo mpenzi wako haijalishi anasema anakupenda kiasi gani au wewe ni jinsi gani unajitahidi kumuonesha kuwa unampenda, siku scenes zake zikiisha tu broh jipange.

MSISEME HAMKUAMBIWA.

Analyse
 
Mkuu, wanawake wana thamani zao, hapa thamani namaanisha tabia, mwenendo na vitu kama hivyo. Kuna wale ambao thamani yao ni kama saa ya mchina ya sh. 500 na wapo ambao thamani yake ni sawa na Seiko 5 ambayo ni saa ya gharama kubwa sana.

Ukimpata huyo wa Seiko 5, hata aje mtu ana nguvu kiasi gani za kifedha au ushawishi hawezi kumchukua, ila ukimpata huyo wa saa ya mchina, kwa ushawishi kidogo tu watu wanalala naye. Huyo wa Seiko 5, ndo somewhere kwenye maandiko anaitwa mke mwema, unaweza kufuatilia zaidi sifa zake
 
Mkuu, wanawake wana thamani zao, hapa thamani namaanisha tabia, mwenendo na vitu kama hivyo. Kuna wale ambao thamani yao ni kama saa ya mchina ya sh. 500 na wapo ambao thamani yake ni sawa na Seiko 5 ambayo ni saa ya gharama kubwa sana. Ukimpata huyo wa Seiko 5, hata aje mtu ana nguvu kiasi gani za kifedha au ushawishi hawezi kumchukua, ila ukimpata huyo wa saa ya mchina, kwa ushawishi kidogo tu watu wanalala naye. Huyo wa Seiko 5, ndo somewhere kwenye maandiko anaitwa mke mwema, unaweza kufuatilia zaidi sifa zake
Mkuu hapa sizungumzii wanawake tu, hii ni kwa wote. Unaweza ukapata dem mwenye thamani ya Seiko 5 alafu wewe ukawa na thamani ya mchina wa Tsh 500. At the end you will dump her when your script is done and u have played all your scenes.
 
Mkuu hapa sizungumzii wanawake tu, hii ni kwa wote. Unaweza ukapata dem mwenye thamani ya Seiko 5 alafu wewe ukawa na thamani ya mchina wa Tsh 500. At the end you will dump her when your script is done and u have played all your scenes.
Mkuu, hizo quality zinaongelewa kwa mwanamke. Usawa wa kijinsia ni fikra ya kibinadamu, kwa Mungu hakuna kitu kinaitwa usawa wa kijinsia.
 
mi yangu script hii imekwama sijui itaishia wapi kuna dalili za kuachwa hivi coz ya past history ila ngoja nione
 
Kuna mmoja hata hatudate ila nampenda mpaka nikiona message yake nato mchozi. Nikimuona ndo najisikia kuzimia kabisa. Umenifanya niwaze tukianza kudate ukite script yake ni ya scene za week 3 si nitakufa mimi
Usijali,script yangu ina uhai kama saa ya seiko.
 
Kuna mmoja hata hatudate ila nampenda mpaka nikiona message yake nato mchozi. Nikimuona ndo najisikia kuzimia kabisa. Umenifanya niwaze tukianza kudate ukite script yake ni ya scene za week 3 si nitakufa mimi
Jiandae tu kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom