Mapenzi ni fadhila?

Mapenzi ni fadhila?

mapenzi si fadhila, ila japo kuna watu wakike kwa wakiume wanafanya kuwa ni fadhila, sasa ukiyafanya nifadhila hadi kufikia kuoana mwishowe unakuwa sio mzuri naamini hivyo.....
tupo pamoja brodah!!
But unamwonaje yul;e mtu anayetaka hadi kutenda unyama juu ya mtu kisa tu hajalipwa fadhila ya penzi alokuwa analitaka??
 
Mapenzi hayawezi kuwa fadhila. Inategemea nyinyi 2 mawasiliano yenu yapoje, wanaume mara nyingi ni watu wa kupima au kujaribu, sasa yale majibu yako wakati huo wa kupimwa au kujaribiwa ndiyo huleta muafaka upande wa mwanaume na wakati huu ukianza kuleta misimamo yako ndiyo majanga hutokea.
 
Mapenzi sio fadhila, mapenzi ni utayari na hiari ya mtu kuingia katika mahusiano na mtu mwingine, bila kujali anapata/atapata nini kutoka kwa mwenzake...hayo yalikuwa mapenzi ya miaka iliyopita.

Mapenzi (kwa asilimia kubwa) ya sasa yapo kwa kulipana fadhila. Fikiria wapenzi wengi wanasomeshana, wanapeana vito vya thamani, huku wakitegemea kupata kitu baadae. Wengine husema kabisa, simpendi ila namuoa/ananioa kwa sababu fulani, maana yake nini...kwamba huyo mwenza asingefanya hivyo asingepata nafasi kwenye moyo wake.

Ndio maana mtizamo wangu ni kuwa, ukiwa na mpenzi, kama umeamua kufanya kitu kwa ajili yake, iwe kumpeleka shule au kumnunulia kito cha thamani, ufanye hivyo kwa vile umependa na si kwa kutegemea kulipwa fadhila (kuoa/kuolewa)
 
sasa kama wanaume ni watu wa kupima kwann wao ndio0 wahanga wa kulia kila siku kwamba wamepigwa chini na waliowafadhili?
 
same dear!!
umenikumbusha msemo wa wahenga kwamba wema haulipwi.

Mtu anawezaje kulipa wema mamii? Achana na material help mtu apatayo, ule moyo wa mtu kujitolea kwaajili yako, kukufikiria na kufurahia kuwa msaada kwako ..yaani huwezi kabisa zaidi ya kushukuru na upande wa pili uelewe hivyo pia, kuwa si lazima itokee kama wanavyo tarajia.
 
Hapana,mapenzi sio fadhila

Nasema hayo kwasababu kwanza mapenzi ni kitendo cha kukubaliana kati ya watu wawili wa jinsia tofauti,wanakubaliana kuyafanya hayo mapenzi [sio ngono pekee] yaani mambo yanayohusiana na mapenzi kama vile kutoka out,kununuliana zawadi,kufanya ngono,kushare masuala ya kimaisha [kiuchumi] n.k

Watu au mtu hulalamika kwasababu ule ni mkataba ambao wanakuwa wamekubaliana na mmoja anaukiuka

Tatizo huanzia hapo!!
 
zamani wakati tunaolewa ilikuwa tunaangalia zaidi utayari ama wa kwako binti ama wa wazazi wako.......
siku hizi maisha yamebadilika sana tunaangalia incentives mtu kama hana basi hawez kupata wa kuoa/kuolewa.

kuna boda boda leo asbh nimepishana nayo kwa nyuma pale kwenye ile mad guard pameandikwa
'BILA PESA DEMU MZURI HUOI'............japo nilicheka lkn nilisikitika
 
Hapana,mapenzi sio fadhila

Nasema hayo kwasababu kwanza mapenzi ni kitendo cha kukubaliana kati ya watu wawili wa jinsia tofauti,wanakubaliana kuyafanya hayo mapenzi [sio ngono pekee] yaani mambo yanayohusiana na mapenzi kama vile kutoka out,kununuliana zawadi,kufanya ngono,kushare masuala ya kimaisha [kiuchumi] n.k

Watu au mtu hulalamika kwasababu ule ni mkataba ambao wanakuwa wamekubaliana na mmoja anaukiuka

Tatizo huanzia hapo!!
ina maana mdogo wangu Eiyer kuna mikataba ambayo watu wengine hujiwekea ili waweze kuwa na mahusiano??
 
Last edited by a moderator:
Mapenzi ni muunganiko wa hisia na pia ni makubaliano ya kutimiza jambo au kitu fulani katika maisha,na endapo mmoja wenu hakutimiza makubaliano basi kunakuwa na malalamiko ya kutotendewa haki.

Cha msingi unapoingia kwenye mapenzi na mtu yeyote especially kwa sisi wanawake usijiaminishe kuwa lazima huyo jamaa yako atakuoa,Subiri wakati utasema kama ikitokea basi ni kheri,isipotokea maisha yanasonga mbele.

Hiyo ndio principle ambayo naitumia siku zote,na hata kama nikihisi sijatendewa haki huwa najipa moyo kuwa pengine it wasn't meant to be na ni hatua ya kujifunza na kukomaa kihisia.
 
Mtu anawezaje kulipa wema mamii? Achana na material help mtu apatayo, ule moyo wa mtu kujitolea kwaajili yako, kukufikiria na kufurahia kuwa msaada kwako ..yaani huwezi kabisa zaidi ya kushukuru na upande wa pili uelewe hivyo pia, kuwa si lazima itokee kama wanavyo tarajia.
ni kweli mpendwa wangu wema halipiki.
Maisha yangu yote huwa namwomba Mungu sana anipe moyo wa kushukuru kwa kila wema ninaotendewa manake najua siwez kuulipa. Lakini anizidishie zaidi moyo wa kutendea wengine mema kuliko kiasi cha wema ninachotendewa na wengine.
 
Mapenzi ni muunganiko wa hisia na pia ni makubaliano ya kutimiza jambo au kitu fulani katika maisha,na endapo mmoja wenu hakutimiza makubaliano basi kunakuwa na malalamiko ya kutotendewa haki.

Cha msingi unapoingia kwenye mapenzi na mtu yeyote especially kwa sisi wanawake usijiaminishe kuwa lazima huyo jamaa yako atakuoa,Subiri wakati utasema kama ikitokea basi ni kheri,isipotokea maisha yanasonga mbele.

Hiyo ndio principle ambayo naitumia siku zote,na hata kama nikihisi sijatendewa haki huwa najipa moyo kuwa pengine it wasn't meant to be na ni hatua ya kujifunza na kukomaa kihisia.
wewe unaonekana kukomaa na kukua kiakili zaid.
Lakini unaonaje/ama utajiskiaje pale makubaliano mliyokuba-LIANA YASIPOTEKELEZEKA??
 
sasa kama wanaume ni watu wa kupima kwann wao ndio0 wahanga wa kulia kila siku kwamba wamepigwa chini na waliowafadhili?

Wanaume wengi sasa wala hawapimi, wengi wanatumia uwezo wao kifedha kuteka mioyo ya wanawake huku wakijua kuwa wadada wanarubuniwa kirahisi kwa pesa. Hii imesababisha wanaume wengi sana kuumizwa kwenye mahusiano. Nashindwa kuelewa kwa nini utumie uwezo wako wa Mali na fedha kumshawishi mtu kuishi na wewe maisha yako yote?
 
ina maana mdogo wangu Eiyer kuna mikataba ambayo watu wengine hujiwekea ili waweze kuwa na mahusiano??
Inaonekana neno mkataba limekustua sana

Basi ngoja nikuambie hivi:

Mapenzi ni makubaliano ambayo watu wanakubaliana na kuoana ni mojawapo ya makubaliano hayo,kitendo cha kwenda kuolewa/oa mwingine ni kwenda kinyume cha makubaliano

Na hapo ndipo kulialia kunaanzia!
 
sasa kama wanaume ni watu wa kupima kwann wao ndio0 wahanga wa kulia kila siku kwamba wamepigwa chini na waliowafadhili?

Atakupigaje mtu chini? kusoma hujuwi hata picha huoni?, atapigwa chini yeye wakati ule anaanza tu kuwaza kunipiga chini mimi.
 
Msingi wa ndoa sio fadhila ni upendo ndoa inayojengwa kwa kulipa fadhila inamfanya mmoja au wanandoa wote kuwa kifungoni tu maana unakaa na mtu sababu tu alikuchangia damu ulipokuwa mgonjwa n.k
 
wewe unaonekana kukomaa na kukua kiakili zaid.
Lakini unaonaje/ama utajiskiaje pale makubaliano mliyokuba-LIANA YASIPOTEKELEZEKA??

Makubaliano yasipotekelezeka piga moyo konde japo sio kitu rahisi,Time will heal everything jipange upya,

Usiendekeze hisia zako muda mwingi jaribu kushirikisha na akili yako,kwa sababu hisia mara nyingi hudanganya,

Usimgharamie mtu kwa kuwa unategemea kupata kitu fulani,kama umeamua kumsaidia fanya tu ila baadaye usije kutaka malipo ya fadhila kwa kisingizio cha mapenzi,

Hisia za mtu hubadilika kadiri muda unavyozidi kwenda,don't invest a lot kwasababu itakucost baadaye.
 
Back
Top Bottom