Mapenzi na Uchawi: Wanawake mnatumaliza!

teh..teh...teh... mada zingine ngumu hata kuchangia kwa uhakika!
umalaya wa mtu kwa kiasi kikubwa unachangiwa na family history, kama mwanaume kwao malaya basi itakuwa hivyo na kama mwanamke kwao wamezoea kuchukua waume za watu itakuwa hivyo pia na kama ni uchawi ipo hivyo!
lakini hakuna anayerogwa bila ya yeye kuwa na asili ya uchawi huo na kulingana na miunganiko na michangano yetu asilimia zaidi ya 70 ya watanzania ni wachawi kwa njia moja au nyingine na hii inatokana kwa kurithi au kwa kufanya.
na mara nyingi watu uoana kwa koo zinazofanana.
na makubaliano mengi hufanywa na mizimu.
hivyo si swala la kumlaumu mwanamke kuwa mchawi bali aliyerogwa ndio mchawi zaidi hivyo ni vyema kushughulika kwanza na aliyerogwa katika asili zake yaani aache uchawi kuliko huyu aliye mroga ambaye kiukweli ni mtoa taarifa za kuwajulisha watu kuwa jamaa ni mchawi iko hivyo kwenye ulimwengu wa roho .
kama unabisha bisheni kwa mazoea.
mfano ,wengi wetu tumechanjwa chale na kunyweshwa dawa za eti kinga au kushiriki katika ibada za matambiko (japo maisha ya tamthilia yanatustiri hatuonekani kama watu wa kwa waganga)
sasa japo hatukuendelea na tamaduni hizi kwenye familia zetu lakini bado tunatambulika kuwa sisi ni wachawi.
hivyo tujipange upya.
 

Kwanini uone kosa kuroga lakini usione kosa kwa mwanaume kumsaliti mkewe...

Wakiachwa wanarudi njia kuu wadogo kama piriton... Na mpaka wakome lolest!!!!
 
Atajali vipi wakati kaishalishwa kanyama kalovundikwa ukeni masaa 12;???? Ogopa hiyo kitu.

Mimi niliwahi kulishwa hako kanyama mkuu!Ila sasa nimeshachomoa Mungu mkubwa!Maana ni hatari sana!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Mkuu... Sio kwelu kwamba uchawi wa karne hii ni wa ukoo... Kuna mada moja iko Sticky jukwaa la Biashara inazungumzia uchawi wa kununua....

Kuna watu hawana asili ya uchawi ila wamejifunza au kununua ukubwani...

Kwa hiyo usijiaminishe kuwa uchawi hufuata ukoo.....
 
Upo sahihi lkn mbona hujamgusia,mwanamke ambaye yeye katulia nyumbani lkn yy ndo anakuwa victimized kwa sababu ya mmewe?
 
Tena mh ninavoitafuta hyo dawa,yani sijapata tu wakunionyesha maana wakaka mmezid kucheza na mioyo ya watu,nikíipata ntakayemuwekea atalia maana nitahakikisha anajisahau hadi ye mwenyewe
 
Pole sana kwa tatizo. Ulilolipata. Ila inabidi iwe ni funzo kwako na kwa watu wengine. kuna watu humu watakucheka lakini nakuambia wako wengi sana wanafanya makosa kama hayo. Be careful aids kills
 
Kwanini uone kosa kuroga lakini usione kosa kwa mwanaume kumsaliti mkewe...

Wakiachwa wanarudi njia kuu wadogo kama piriton... Na mpaka wakome lolest!!!!

Kwa nini unaongea kana kwamba mke hawezi kumsaliti ama wanawake huwa hawafanyi usaliti?Mimi nimeshuhudia mke akifanya usaliti hadi jamaa akagundua naye kaamua kutoka ikawa kakamatwa nyumba ndogo.Kibaya zaidi ni kwamba mkewe huduma zikapungua na akaanza kuchakaa na jamaa zake wakamtema!Sasa anahangaika na watoto na mumewe kang'anganiwa!Rehema za Mungu tu zinatakiwa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

teh..tehe...ndo hivyo ukubali usikubali ndo hivyo hakuna jipya huyo mtu analolifanya ukoo wake haukuwahi kufanya ukichunguza katika vizazi vyake vinne kuna mtu alishafanya hivyo.
inawezekana kabisa vizazi vyako viwili havihusiki na hilo lakini cha tatu kikahusika kama unabisha anza kuchunguza kizazi chako kuanzia kwa upande wa baba na mama nenda level nne utarudi na majibu kwa nini mdogo wako mtoto wa baba yako mdogo au wa mama yako mkubwa haishi kwa waganga ili mwanaume atulie
 
Upo sahihi lkn mbona hujamgusia,mwanamke ambaye yeye katulia nyumbani lkn yy ndo anakuwa victimized kwa sababu ya mmewe?

Huyo mwanamke wakati mwingine anaweza kuwa chanzo ama wakati mwingine ni tabia tu ya mwanaume kutotulia...

Cha kufanya mwanamke awe karibu na Mungu wake katika kipindi hiko make hakuna lishindikalo kwake....
 
Mada za leo ngumu sana ngoja niwe msindikizaji
 

Fikiria wewe siku moja umefanyiwa hivyo siku mmeo akijikuta katoka nje kweli! Sawa inauma hata kwa mumeo kutoka nje lakin si afadhali arudi mzima??? Je wewe ukifariiki au kupatwa na ulemavu wanao huwahurumii? Nashauri kama tungeshirikiana kupiga vita uchawi miongoni mwa akina dada! Umeona hata hawachangii humu, maana siku hizi ndo fashion kabisa, hata vyuo vikuu ndo story.....dawa za kushika wanaume!
 
Tena mh ninavoitafuta hyo dawa,yani sijapata tu wakunionyesha maana wakaka mmezid kucheza na mioyo ya watu,nikíipata ntakayemuwekea atalia maana nitahakikisha anajisahau hadi ye mwenyewe

Jamani tabia mbaya sana, usiitafute wewe!
 
Mimi niliwahi kulishwa hako kanyama mkuu!Ila sasa nimeshachomoa Mungu mkubwa!Maana ni hatari sana!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Pole sana! Ulifanyaje nimwambie jamaa yangu aliyetelekeza watoto na mke hospitali ili arudi tena??
 
Warogwe tu mpaka watapokuwa waaminifu

Waathirika ni ninyi wanawake na watoto. Sisi wanaume tunapumbazwa kupenda tu lakini wanawake wanalogwa ili waache nafasi mahawala wamiliki!
 

utasingizia na uchawi tu zinakuwaga akili hamna tu
utasingizia na uchawi kumbe mapishi ni mazuri
utasingizia na uchawi kumbe kauri ya kuongea ni nzuri haina ukakasi
utasingizia na uchawi kumbe mwanaume anasikilizwa na siyo kutukanwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…