Mapenzi na Uchawi: Wanawake mnatumaliza!

Acuity

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
391
Reaction score
118
Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, wanawake wanazidi kukata tamaa ya kuolewa. Silaha yao imebakia uchawi. Mfano, binti akitongozwa na kijana au mwanaume ambaye tayari yumo kwenye ndoa (inapotokea kwa bahati mbaya, amejikwaa kwa huyo binti), msichana atahakikisha huyo mwanaume anahama kwake, anakwenda kuishi na msichana huku katerekeza familia yake. Kama aliyependwa ni kijana ambaye hajaoa, basi huyo ataahirisha mipango yote na kufanya anayoelekezwa na msichana, kama alikuwa akilipa karo ya wadogo zake, inakuwa ndo mwisho. Kama alipendwa mume wa mtu, basi huyo mke wake anaugua na kufariki au anachanganyikiwa! Hii nimeishuhudia katika familia mbili. Huu ni uchawi. Wanawake, mmezidi, muache kupenda kwa ndumba, mtapendeka tu kwa kuonesha mapenzi natural ambayo si matokeo ya mitishamba!!
 
1174773_505327519538024_1934316671_n.jpg
Waganga2.jpg
 
Yaani Mkuu hii habari inaharibu kabisa. Mimi nimeshuhudia jamaa alikuwa family freind wa familia yangu, mara kajichanganya kwa kabinti, amehama kwake, tumemtoa juzi tukiwa team ya watu 6, karudi na begi. Baada ya siku mbili tu, mkewe kaanguka bafuni, kavunjika mguu kabisa, hivi sasa yupo Bugando. Mbaya zaidi huyo shemeji yangu, ananyonyesha mtoto wa miezi 4. The man wala hajali kama mkewe yupo hospitali! It pains alot!
 
Mkuu kama una ndoa kwanini usibaki njia kuu? Acheni kusingizia wadada kila kitu mana hamfungwi kamba kuamishwa kwenye ndoa zenu.

Nakubaliana na wewe lakini inapotokea mtu amejikwaa kidogo, tunatarajia arejee nyumbani kwake salama. Lakini siku hizi ni tofauti maana kurudi majaliwa. Hii tabia waiache akina dada! Wakubali ku-share hasa pale wanapojikuta wamependa waume za watu!
 
sasa kwanini musimpeleke kuombewa huyo rafikiyo na mkewe kama unajua uchawi ndo umemfanya hivyo?
 
Nashangaa kawa huna malengo na mwanamke unamfatia nini? Au kama umeoa si utulie na ndoa yako kwa nini umtumie bint wa watu kisha umuache ndio maana wanawakomesha nyie msiotaka kutulia
 
Munkari unaweza kuombea mtu aliyevunjika mguu?? Yupo hospitali labda akirudi tutafanya hivyo.
 
Nakubaliana na wewe lakini inapotokea mtu amejikwaa kidogo, tunatarajia arejee nyumbani kwake salama. Lakini siku hizi ni tofauti maana kurudi majaliwa. Hii tabia waiache akina dada! Wakubali ku-share hasa pale wanapojikuta wamependa waume za watu!
mtu unafanya jambo kwa makusudi unajua una ndoa na huna mpango wa kuongeza mke then unasema umejikwaa basi na huyo binti atakuwa kajikwaa kukuroga anyway siungi mkono ushirikina but wanaume na nyie mtulie
 
Nashangaa kawa huna malengo na mwanamke unamfatia nini? Au kama umeoa si utulie na ndoa yako kwa nini umtumie bint wa watu kisha umuache ndio maana wanawakomesha nyie msiotaka kutulia

Nakubaliana na wewe, lakini unadhani suluhisho ni uchawi? kwanini usikubaliane na hali ukakubali kushare kama kweli kweli unahisi unapendwa na ukamwacha mke mwenzio na hawala yako huyo waendelee kuishi salama ndani ya familia yao?? Nakubali kwamba wanaume tuna tamaa lakini wasichana wa siku hizi wanatamaa zaidi, hata za kupeleka roho za watu kuzimuni!
 
in the spiritual world, the devil is very powerful
 
mtu unafanya jambo kwa makusudi unajua una ndoa na huna mpango wa kuongeza mke then unasema umejikwaa basi na huyo binti atakuwa kajikwaa kukuroga anyway siungi mkono ushirikina but wanaume na nyie mtulie

Crstal Clear; na mimi siungi mkono wanaume kwenda nje ya ndoa. Lakini katika mazingira ya sasa, ni nadra mwanaume kutulia na mke wake, walau aende nje hata mara moja kwa mwaka. But, unaonaje tabia ya ushirikina, inafaa kutumika ili kupata mume??
 
Back
Top Bottom