Mapenzi Na Mafanikio Ya Mwanamke


tathimini zako nashindwa kuzipa 100% hazinipi majibu fasaha !
 
Thanks Mkuu, sina wasiwasi kabisaa na hilo, ni mambo ya muda na nafasi lakini jitihada tayari wasiwasi wangu ni watu wanaosema ukimsomesha anakukimbia!!!

halafu na naona kama kuna kaukweli fulani mazee

You must be genius!!!!!!!!!!!!!
 
Mimi nafikiri kuna mengi yanayochangia hapa si elimu peke yake. Ninamfahamu mama ambae ameachana na mume wake baada ya kuhitimu elimu yake na kwa ukaribu ni kuwa huyu mama alikuwa ananyanyaswa sana na mume wake (unfortunately huyo mume alikuwa ni msomi mzuri tu). Mama alipoona manyanyaso yamezidi akaamua kutafuta elimu (hakusomeshwa na mume wake- alipata mkopo huku akisaidiwa na dada yake). Na elimu yake hakuipata kirahisi including kero na frustrations kibao toka kwa Mr. akiwa na lengo la kumkatisha tamaa lakini alifanikiwa kumaliza salama.


Baada ya kumaliza (yeye ilikuwa Masters) gubu na kero toka kwa mume hazikukoma ndio kwanza zikaongezeka. Mama akiargue kidogo/akitoa ushauri ambao unapingana na wa mzee anaambiwa anajifanya kasoma. Akitaka kutafuta kazi ili apractice elimu yake anazuia huyo mmoja akatafuta kwa siri kazi akamwambia mumewe alipopata na hata alipokatazwa akaanza kinguvu. Matokeo yake ugomvi kila kukicha na mume akamtafutia mwenza kisa anaambiwa ana kiburi. Mamam akaamua kutafuta nyumba akaondoka na kichanga chake. Mtaani yameenea maneno oh mke kasoma kamtelekeza mume!!

What I want to write here ni kuwa it takes a lot kwa mwanamke kufikia uamuzi wa kumwacha mume. So tusiangalie klijuu juu tu. Kuta zinaficha mengi
 
MJ1
Huu ni mfano halisi wa kile nilichosema kwenye bandiko langu.Mke akiendelea kuliko mume mara nyingi huleta balaa kwenye ndoa.Lakini haimaanishi ni kila ndoa hukumbwa na balaa hili.Kero za masimango kama haya ndizo humpa mke msukumo kutoka na kutafuta amani bila kujali jirani, rafiki, ndugu , adui atasema nini.

Ndugu zangu akina kaka, mjue kuwa katika ulimwengu wa sasa, ni vigumu kuwafunika au kuwa suffocate wake zenu.Jiandae na mpokee kuwa wake zenu wana kila potential kuwa sawa na nanyi kielemu au kipato au hata kuwazidi. MKILIPOKEA NA KULIKUBALI NA MKATAMBUA KUWA YATASEMWA MENGI, NYIE KAZANENI KUWAPENDA WAKE ZENU HALAFU MTAKUJA KUTUPA USHUHUDA WA MAISHA YANAVYOKUWA MATAMU.

SISI WANAWAKE KWANZA TUNAWAPENDENI SANA, TUNAWAJALI NA TUKO TAYARI KUWAFANYIA MAKUBWA SANA HAMJUI TU.Tupeni ushirikiano, tupeni nafasi .......
 
What I want to write here ni kuwa it takes a lot kwa mwanamke kufikia uamuzi wa kumwacha mume. So tusiangalie klijuu juu tu. Kuta zinaficha mengi



MJ1 na WoS,

Mbona mi natamani jamani my wife wangu angesoma hadi kile kibao cha 'no more education'....

lakini si hivyo tu, nadhani kama mwanaume UKIJIAMINI mwanamke anakukabidhi kila kilicho chake, ni juu yetu kukitunza kama lulu! Hapo ndo utamu unapokuja wa kitu kinachoitwa NDOA.

I aprreciate, WoS, kuwa mnatupenda, tena sana. Niseme tu kuwa kuna baadhi ya wanawake kutokana na mfumo wtu wa kijamii ulivotulea kwa karne na karne, wakipata zaidi basi ni kweli wataanza manyanyaso ya namna fulani. Hapo itahitaji awe amepata mume wenye busara ili aweze kumwongoza katika njia ifaayo ili kukwepa mitafaruku isiyo ya lazima.
 
Hili suala la kuelimisha wake zetu,ndo linaananza kuchukua kasi kwenye jamii yetu, na siku zote kitu kikipokelewa ujue kuna watakao kipokea sivyo ndivyo,chukua mfano; mtu kaolewa ili ajikomboe(kufanikiwa) kimaisha kisha ukamsomesha akagundua elimu aliyonayo inaweza kumkomboa kimaisha zaidi ya kuwa na wewe,nn kitakachotokea? lakini kama mna upendo wa dhati mbona poa tu,kwasababu upendo wa dhati acha elimu hata pesa na ndugu hawawezi kuuvuruga,ila kumsomesha mkeo ni sehemu ya wajibu wako mwanaume,kwa maendeleo bora ya vizazi vyenu, hasa kipindi hiki cha utandawazi
 

Hapo penye red hapo..... patamu

angalizzo si wajibu tu wa mume kumsomesha mke bali hata mke kumsomesha mume ndo mwake wapenzi
 
 
Hivi unasema kweli PJ ..nina mpango wa kuendelea na elimu mpaka nimzidi mme wangu kabisaaaaaaaaaaa ..sijui na mie nitabadilika ??

.......Soma mpenzi wangu, hata ukimpita poa tu. Elimu ndio ukombozi wa mwanamke.
 
Hata kama hajakuacha physically, ukisikia anasimulia na kutoa sifa kem kem kwa wanaume, Oh tulisaidiana sana, ni mstaarabu sana, anajali sana, anajiheshimu sana, ni mpole sana, tulidiscuss pamoja kwa karibu sana, nk. Kisha simu zikipigwa hataki kuongea nawewe ukiwapo karibu, ujue akilini mwako umechujuka na anao wengine kichwani mwake na huwakumbuka. Tena akiwakumbuka hufarijika sana. Ukiwa shambani kulima unageuzwa screen, kichwani kwake anayelima ni yuleee. Siku moja atakuambia "Hapo hapo John!" kumbe kajisahau kwambawewe n Juma wala sio John. Usiku akiweweseka atalembulia jina la John ilhalin wewe umemzungushia mkono wako juu ya nanii yake.

Misahafu yote inasema usimwamini mwanamke asilimia zote, kuna siri zako zingine ambazo hata mkeo hapaswi kuzifahamu. Hujasikia kuna mwanasiasa waziri Bongo anayemsotesha mumewe msomi na mhadhiri chuo kikuu kimojawapo Bongoland? Yeye na mizunguko tu, shamba hulimwa pale anapojisikia ndio hulipeleka likalimwe, lakini vinginevyo linalimwa huohuko mizungukoni. Ila akisikia kwamba umelipeleka jembe kulima kwa jirani anapagawa kwa hasira, ati hataki jembe lake lichezewe, lakini wakati huo huo hataki kulikalisha shamba lako mahali jembe lilipo ili ulime kwa nafasi.

Hiyo ndiy Kilimo kwanza Bongoland. Huo ni mfano tu. Mkeo akifanikiwa kisiasa na ikapigwa simu usiku wa manane kwamba anatakiwa mara moja sehemu fulani kikazi inakuwaje na shangingi linakuja kumchukuwa? Ukitaka uishi siku nyingi katika mazinbgira kama hayo, wewe jifanye *****. Atalipeleka shamba lako huko, watafanyia majaribio na atalirudisha tena. Omba Mungu tu wasiweke sumu shambani humo ukadhurika na wewe Wengine hawavai buti wanapofanya majaribio katika mashamba yasiyokuwa yao, maana wamezoea na kuyafanya kama vile ni ya kwao.

Kwa hiyo, maendeleo ya mwanamke is a disastre to her company. Mwalimu wangu mmoja alipropose kwamba ni bora na sahihi zaid mke akae ndani akilea watoto na kutunza mji, wakatimzee anachakalika kutafuta maisha, akirudi akute mwili laini na afarijike. Kuliko wote kuchakalika na kuwa musculine. Mkitoka shambani mtafute kujikanda maumivu.

Leka
 

Leka, nashukuru kwa kuwa detailed na kuweka wazi mtazamo wako;
cha maana ni kukumbuka kwamba haya mambo ya mapenzi ni siri kubwa sana iliyopo moyoni na ndio maana watu wanasema "laiti ningekufungulia moyo uone"

Ukweli ni kwamba kuna aina mbili kubwa za "life partners"

  • moja ni yule mwaminifu atakayestick na wewe to the last drop - hawa ni rare gems na kwasbabu hiyo mifano yao ni michache sana
  • ya pili ni ile ya "circumstantial" partnerships - hii ni wengi na wanakuwa entrepreneurs kwenye kila kitu, hadi mapenzi wanayafungulia ledgers... hao ndio nuksi lakini ndo majority!!! huwa wansubiri triggers (sababu tu!), wakuache baada ya kuchupa toka daraja moja la maisha kwenda jingine
Cha maana ni kuwa positive mda wote wa mahusiano kwani unakuwa unavunja zile dark forces zake maana mara nyingi zinapandikizwa utotoni na ndio maana wazazi huangalia watoto wanaoa au kuolewa wapi!

the bottom line is, lets support them and if they benfit ujue kwamba ndugu, jamaa na marafiki watafaidika...
 


Leka..umenichekasha sana!
Sina la kusema maana unajua unaowasema labda kuna visa kama hivi unavijua. Lakini usifananishe wote na huu mfano.Pia kwamba samaki mmoja akioza ni wote..sidhani utakuwa sahihi kuuweka katika maisha binafsi ya watu.
All the same..thank u for the anecdote.
 

Hata mawe hubadilika. Mengine huwa vito, mengine huwa takataka!!!!!!!!!!!!!!
 
 
 

hapo bolded ndipo penye determination,lakini tatizo linakuja ni wachache sana wenye hiyo kitu MAPENZI YA DHATI, wengi ni matapeli tu wa mapenzi,nawaongelea jinsia ya SHE hapa, hawa ndio huwa wanaingia kwenye ndoa kwa sababu fulani fulani na sio mapenzi ya dhati
 

Mkuu, hata hao ma HE nao kuna matapeli wa ndoa aisee... hujawahi kusikia wanaume kama mabinti?

eniwei, kusomesha au kutosomesha ni suala la ntu na ntu!!
 
hapa naona kuna maswali ya kujiuliza; huyu mwanamke anasomeshwa kwa faida ya nani? na huyu mwanaume anasomesha kwa faida ya nani? tukigundua sababu ndio tutatenda haki kwenye mjadala
 
Kaka zangu mlio humu ndani kumsomesha mke ni jambo zuri sana, ila mimi kwa maisha ya sasa hivi siwezi hata kumshauri kaka yangu kufanya hivyo. Kwa sababu kuna kaka yangu alimsomesha mke wake akaacha kumsomesha mdogo wake, baada ya wifi kumaliza chuo, tulishangaa kaka akiacha kila kitu, gari na kila kitu na kuondoka personal things tu na ndoa ikaishia hapo. Ukimsomesha msomeshe kwa faida ya wanao kwa sababu ht mkiachana watoto wataendelea kupata msaada kwa mama yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…