ki ukweli ni bora kama una tatizo uombe tu kuliko kutumia lugha ya kukopa wakati huna lengo la kulipa, na pia kama una uhakika wa kuzilipa basi mwambie akukopeshe.
Mfano:mimi nilikua na biashara zangu na mpenzi wangu alikuwa na tabia ya kuniomba pesa nimsaidie,nikawa na mpa na sichukulii kama namdai,sometymes akawa anasema nimkopeshe nikawa namkopesha pia lakini halipi anasema ntalipa mana kwa sasa kiuchumi siko fresh,baadae akawa anakopa hadi bidhaa zangu za biashara na alipopata pesa hakulipa pesa nilizomkopesha na wala pesa za bidhaa zangu alizokopa ukiachilia pesa nilizokuwa nampa tu akinililia shida mana mi nilikuwa na kazi na biashara yeye alikuwa hajapata kazi bado wala biashara.
Alipopata kazi nzuri kushinda yangu, akasema tuachane na pesa zangu hanilipi na simu nisimpigie tene! for sure niliyumba mana pesa nilizotegemea zingerudi kwenye biashara hazikurudi na biashara mtaji ulikata kabisa na yeye aliyesababisha kaniacha! nilishangaa mana mi nilifanya vile kwa kumuhurumia kumbe ye hakuwa na true love japo tulianza uhusiano kitambo na wote hatukuwa na kazi wala biashara japo baadae mi ndo nilitangulia kufanikiwa nikawa namsaidia nikijua tupo pamoja kumbe mauzauza tu! iliniuma sana.
so ukitaka kumsaidia mpenzi wako msaidie tu,mana ukimkopesha uwezekano wa kurudi hizo pesa ni mdogo sana mana lolote linaweza tokea "don't trust anybody even myself"