Mapenzi hayalazimishwi

Mapenzi hayalazimishwi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,639
Reaction score
220,421
Kuna dada mmoja Arusha alimpata kijana mgeni anafanya kazi kwenye bank moja hapo mjini. Walianza dating, lakini kaka inaelekea moyo haukua kwa dada wakati dada anapiga picha ya gauni la harusi. Kaka alianza kumpiga matukio lakini dada alikua mbishi kuelewa.

Alikwenda J’mosi kufanya usafi wa nyumba, kufua, kupiga pasi na kupika. Sikunyingine anaambiwa usije nitakua safarini, dada akizuka anamkuta kaka anaangalia mpira.

Mara mkaka amepata uhamisho, sifahamu kama huu uhamisho ulikuja kama bahati au kaka aliuomba lakini alisoma misa ya shukran. Alihamia Dar makao makuu ya bank yao. Dada aliifahamu namba ya kazini akawa anapiga simu.

Siku moja alimwambia ninakuja Dar kukuona. Mdada amefika Ubungo kaka alimpokea na kumpiga tukio la mwisho, mdada alielewa somo kuwa hatakiwi.
 
Ushauri wako kwa wadada ni UPI aswa?
 
Tukio la mwisho ni lipi?
Ilikua J’mosi jioni, dada alitoka Arusha asubuhi hivyo alikua na uchovu wa safari. Mkaka alijua akimpeleka nyumbani amekwisha.

Alimwambia wachukue guest mjini. Baada ya shughuli mkaka alimwambia anatoka mara moja atarudi. Hakurudi tena na simu dada aliyoifahamu ilikua ya ofisini. Alilala J2 asubuhi alilielewa somo na kwenda Ubungo kuwahi mabasi ya Arusha.
 
Ilikua J’mosi jioni, dada alitoka Arusha asubuhi hivyo alikua na uchovu wa safari. Mkaka alijua akimpeleka nyumbani amekwisha.
Alimwambia wachukue guest mjini. Baada ya shughuli mkaka alimwambia anatoka mara moja atarudi. Hakurudi tena na simu dada aliyoifahamu ilikua ya ofisini. Alilala J2 asubuhi alilielewa somo na kwenda Ubungo kuwaji mabasi ya Arusha.
That man was still a big boy with childish mentality. Anamsumbua bibie bila aibu na adabu.Kwa nini usimueleze mtu jambo kwa uwazi ili uiache nafasi yake iumeng'enye ukweli huo?
 
Kuna wengine hawaelewi hata ukiwaeleza.
 
Kuna dada mmoja Arusha alimpata kijana mgeni anafanya kazi kwenye bank moja hapo mjini. Walianza dating, lakini kaka inaelekea moyo haukua kwa dada wakati dada anapiga picha ya gauni la harusi. Kaka alianza kumpiga matukio lakini dada alikua mbishi kuelewa.

Alikwenda J’mosi kufanya usafi wa nyumba, kufua, kupiga pasi na kupika. Sikunyingine anaambiwa usije nitakua safarini, dada akizuka anamkuta kaka anaangalia mpira.

Mara mkaka amepata uhamisho, sifahamu kama huu uhamisho ulikuja kama bahati au kaka aliuomba lakini alisoma misa ya shukran. Alihamia Dar makao makuu ya bank yao. Dada aliifahamu namba ya kazini akawa anapiga simu.

Siku moja alimwambia ninakuja Dar kukuona. Mdada amefika Ubungo kaka alimpokea na kumpiga tukio la mwisho, mdada alielewa somo kuwa hatakiwi.
Hivi kitabu chako cha haya mambo kinatoka lini? Ukichelewesha kitakuwa kikubwa sana ni bora ukatoa volumes tofauti na sio editions.
Fedha nje nje, halafu mnasema vyuma vimekaza.
 
Kuna dada mmoja Arusha alimpata kijana mgeni anafanya kazi kwenye bank moja hapo mjini. Walianza dating, lakini kaka inaelekea moyo haukua kwa dada wakati dada anapiga picha ya gauni la harusi. Kaka alianza kumpiga matukio lakini dada alikua mbishi kuelewa.

Alikwenda J’mosi kufanya usafi wa nyumba, kufua, kupiga pasi na kupika. Sikunyingine anaambiwa usije nitakua safarini, dada akizuka anamkuta kaka anaangalia mpira.

Mara mkaka amepata uhamisho, sifahamu kama huu uhamisho ulikuja kama bahati au kaka aliuomba lakini alisoma misa ya shukran. Alihamia Dar makao makuu ya bank yao. Dada aliifahamu namba ya kazini akawa anapiga simu.

Siku moja alimwambia ninakuja Dar kukuona. Mdada amefika Ubungo kaka alimpokea na kumpiga tukio la mwisho, mdada alielewa somo kuwa hatakiwi.

Kuna muda wanaume wanakutongoza kwa lengo la kuona tu kuwa bado wanauwezo wa kutongoza na kukubalika. Na anaweza kabisa akasema anataka kukuoa , ni vizuri mwanamke kutokuwa na papara, hakuna mwamume ambaye anataka kuoa lakini wewe mwanamke uwe una m drive hivyo, hilo ni tukio kubwa , mwanaume angetaka yeye awe driver, huwa inakera kwakweli maana kuna wanawake wako jujuu kama moshi wa kifuu, yaani anakufika kooni mpaka unamchoka.
 
Bibi kuna watu wengine wakishapenda wanakua vipofu, viziwi na pia mabubu.
Hua wanashindwa hata kusoma mabadiliko ya tabia nchi, hao dawa yao ni kupiga tu matukio mpaka dedi seli zao zinafufuka.
Ndiyo maana nimeshikilia kwa babu Asprin kule sijawahi wala sitawahi kupigwa matukio.
 
Hahahaaaa ngoja siku moja babu akutandike dhoruba moja ya tsunami.
Ila nyie upendo wenu ni wa agape maana hata shetani anaogopa kutia mguu wake.
 
Back
Top Bottom