Mapenzi au kazi kipi kitangulie?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Chochote kinaweza kutangulia hasa Kwa wale Watu Exceptional, wateule, wenye bahati zao. Ambao Watu hao Duniani ni wachache yaani mmoja mmoja. Watu hao ndio wanaovunja Kanuni za Asili na kuwafanya Watu wengine waseme Maisha hayana Formula. Ni kweli Maisha hayana Formula lakini ni Kwa Watu Exceptional ambao ni mmoja mmoja. Lakini waliobaoi wote Maisha Yana Kanuni na formula zake.

Kikawaida maji hufuata mkondo, hiyo ni formula ya Maisha lakini yapo maji exceptional ambayo yasiyofuata mkondo. Taikon sitaki leo kuwachosha, nirudi kwenye mada.

Je kijana ambaye ndio Kwanza anaanza kujitegemea, Mbele yake anakabiliwa na mambo makubwa mawili, KAZI au MAPENZI. Kila kimoja ni nyeti na kitaathiri Maisha yake iwe positive au negative.
Swali; Kipi kijana achague Kati ya Mapenzi au Kazi? Marà anapoyaanza Maisha yake.

Haya ndio maelekezo nitakayokupa ambayo utayafanya na bila ya Shaka yatakusaidia;

1. Jitambue wewe ni wakawaida au Exceptional.
Ukianza kujitegemea jiulize wewe ni mtu wa Aina gani, je ni MTU kama walivyowatu wengi wengine, au je wewe ni mtu ambaye mfano wako mpo wachache?

Kujibu swali hilo itakupasa ujiulize maswali mengine madogo ili kujijua wewe ni mtu wa aina gani.
a) Je ukifanya mambo yako yanaenda kiurahisi au ni mpaka uparangane?

b) Je ukifika sehemu Watu wanakukubali na kukupenda bila hata wewe kufanya jitihada?

c) Je unaposema Jambo Watu wanakuamini na hawakutilii mashaka?

d) Je uliwahi kutongozwa na Wanawake ikiwezekana kuhongwa kabisa na hao Wanawake? Hata kama ni mmoja?. Licha ya kuwa hauna muonekano wenye kuvutia na hauna Pesa lakini Wanawake wanajigonga, je uliwahi kujiuliza hiyo inasababishwa na nini? Wanawake hupenda Watu Exceptional, na huvutiwa na watu wa namna hiyo. Iwe Kwa kujua au Kwa kutokujua.

e) licha ya kuwa unajiweka nyumanyuma na hujipendekezi lakini unashangaa viongozi, maboss wako wanakuchagua na kukuheshimu. Ukishajijua wewe ni mtu wa Aina gani itakusaida katika hatua zinazofuata.

Kama Wewe ni binadamu wa kawaida kama walivyowengi ambao Kula Yao ni yajasho mpaka watumie nguvu nyingi. Basi unapaswa uchague KAZI ndipo baadaye uchague MAPENZI.

1. Usichague Mapenzi kama chagua la Kwanza kama unajijua wewe ni binadamu wa kawaida. Yaani bahati yako ni mpaka uitolee jasho. Utaumia, utasagika, utapasuka.

2. Chagua KAZI, ipende, ifanye Kwa Moyo wako wote, ujipatie riziki kupitia kazi hiyo, utumie Akili kuitumia Riziki hiyo ili uweze kuyaweka Maisha yako yawe mazuri. Kisha ukishajijenga, na kuwa na makazi, au uwezo wa kulipia makazi, na uwezo wa kulisha Watu angalau watano. Basi hatua ya pili ingia kwenye Mapenzi.

3. Pamoja na kuwa unakazi, isikufanye ukakosa utulivu, umakini katika kuchagua Nani WA kumpenda. Hakikisha unachagua pia anayekupenda. Zingatia kuwa, wewe ni binadamu wa kawaida hivyo shida ni zinakuandama hata ukiwa na Furaha. Tofauti na watu exceptional ambao furaha inawaandama hata wakiwa na shida.

Kupata kwako kazi na Pesa haitamaanisha kuwa mapenzi yatakuwa rahisi, hapana. Kazi Ipo kwaajili ya kupunguza Kani ya gravitational inayolazimisha mambo yako kuanguka.

4. Iheshimu kazi na kila senti tano ilinde na kuiwekeza sehemu sahihi. Usiwekeze kwenye mapenzi hasa ukishajitambua kuwa wewe ni binadamu wa kawaida.

Mapenzi hayatakulipa ukiwekeza Huko ikiwa wewe ni binadamu wa kawaida, lakini Kwa Watu Exceptional Mapenzi kwao lazima yawalipe na wanabahati nayo.

Watu exceptional huyashinda mambo yaliyowashinda Watu wa kawaida (wenzangu na miye)

5. Ni kosa kubwa la kiufundi Kwako kijana kuoa Mwanamke Kabla hujaweka mambo yako Sawa ilihali unajua kabisa wewe sio mtu maalumu (exceptional).

6. Ukishaoa na kuzaa Watoto na tayari unajijua wewe ni mtu wa kawaida ni vizuri uhakikishe na ujithibitishie hao Watoto no wako.

Ni kawaida watu wa kawaida kubebeshewa mizigo, kubambikiziwa Watoto, na wao Kwa vile sio Watu wenye bahati njema hujikuta wakiteseka Maisha Yao alafu mwisho wa siku wanakuja kuumia. Najaribu kusema, ukishajijua wewe sio Exceptional ni lazima uwe makini na MTU wa tahadhari nyingi Mno.

7. Kikawaida Watu wasio Exceptional hufa mapema Kabla ya Wake zao. Hii ni tofauti na wale Exceptional. Wanaume exceptional ni nadra Sana Kufa Kabla ya Wake zao. Chunguzi zangu zinaonyesha hivyo.

Nimezungumzia mambo ya Kifo Kwa sababu vifo vingi sababu kubwa inatokana na Masuala makuu mawili ambayo ni KAZI(utafutaji) na MAPENZI (mahusiano). Kama ni MTU wa kawaida ili uishi Maisha mazuri ni lazima uwe mwingi wa ujanjaujanja katika Mapenzi na katika utafutaji (kazi).

Hivyo ni ushauri wangu Kwa Watu kuwa Kwa vile wengi wao ni Watu wa kawaida basi ni vizuri wachague Kwanza KAZI ndipo yafuate Mapenzi. Kwa sababu kwao mapenzi bila ya kazi(kipato) hayawezekaniki. Hii ni tofauti na wale Exceptional ambao wanaweza na kazi na bado mapenzi wakawa wanayamudu na wake zao wakawa wanawaheshimu.

Zingatia: Ukiwa MTU wa kawaida heshima yako haitokani na kazi au pesa pekee Bali inatokana na jinsi inavyotumia Akili yake kuendesha kazi na Pesa yako Hekima ukijua kuwa bila hiyo kazi na Pesa wanaokuzunguka wasingekuwa karibu yako. Hivyo karibu wote ni Wanafiki. Ndipo Ile kauli ya Trust no one inapotokea Kwa sababu hiyo ni universal Law Kwa Watu wa kawaida.

Lakini Watu exceptional hiyo Kanuni haina matumizi kwao Kwa sababu wao nature imewapa upendeleo wa kuishinda gravitational force. Yaani Mtu exceptional anaweza kulala na Mwanamke mwenye ukimwi na asiupate huo ukimwi.

Mtu exceptional anaweza kukutana na Tapeli au jambazi na akamuachia Pesa zake akaenda chooni na Yule jambazi au Tapeli asipate wazo la kuzichukua zile Pesa.

Zingatia Watu exceptional ni wachache na Wakati mwingine hawajitambui kama ni exceptional Ila wanasikia wakiambiwa na watu Wengine kuwa Fulani anabahati Sana. Au jamaa anakizizi.

Acha nipumzike sasa, nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
"Mtu exceptional anaweza kulala na mwanamke mwenye Ukimwi na asipate huo Ukimwi"🤔
 
Watu exceptional unamaanisha magenius na talented?

Au watu wa kiroho sana?
 
Back
Top Bottom