Mapendekezo ya wananchi: Muundo wa Baraza la Mawaziri kwa Serikali ya Awamu ya Tano

Kabla hata ya kumfikiria Mwakyembe atwambie waliopiga deal ya Mabehewa feki na hatua zilizochukuliwa dhidi yao.
 
Natambua JPM ana kazi kubwa ya kuteua baraza la mawaziri. Katika kuchangia juu ya suala hilo, kama mwananchi wa kawaida napendekeza aangalie mawazo haya pia:

1. Harrison Mwakyembe, Waziri Mkuu
2. Asha Rose Migiro, Mambo ya Nje
3. January Makamba, Afrika Mashariki
4. Sospter Muhongo, Maji, Nishati na Madini
5. William Lukuvi, Ardhi, Maliasili na Mazingira
6. Adadi Rajabu, Mambo ya Ndani
7. Kabudi Palamagamba, Katiba na Sheria (mbunge wa kuteuliwa)
8. Mwigulu Nchemba, Fedha na Uchumi
9. Luhiga Mpina, Viwanda, Biashara na Utalii
10. Stephen Wassira, Ofisi ya Rais Kazi Maalum (mbunge wa kuteuliwa)
11. Diodurus Kamala, Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi
12. Aggrey Mwanri, TAMISEMI (mbunge wa kuteuliwa)
13. Mwele Malecela, Afya (mbunge wa kuteuliwa)
14. Assumpter Mshama, Maendeleo ya Jamii
15. Mohamed Seif Khatibu , Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
16. Jumanne Maghembe, Kilimo na Misitu (inajumuisha Uvuvi na Mifugo)
17. Makame Mbarawa, Habari na Mawasiliano
18. Ramo Makani, Miundombinu na Uchukuzi
19. Sifuni Mchome, Elimu, Sayansi na Teknolojia
20. Charles Makakala, Ulinzi na JKT (mbunge wa kuteuliwa)
21. Juma Nkamia, Habari, Utamaduni na Vijana
22. Jennister Mhagama, Uratibu wa Bunge
23. Lazaro Nyalandu, Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mahusiano

24. Angela Kairuki, Naibu Ardhi, Maliasili na Mazingira
25. Kangi Lugora, Naibu TAMISEMI
26. Ummy Mwalimu, Naibu Habari, Utamaduni na Vijana
27. Janet Mbene, Naibu Viwanda, Biashara na Utalii
28. Charles Mwijage, Naibu Maji, Nishati na Madini


Haka ni ka-baraza kadogo, kalikozingatia mabadiliko ya wizara, na si kila wizara iwe na naibu. Awape hao kwanza changamoto kisha ataangalia wapi pa kurekebisha mbele ya safari kulingana na utendaji na changamoto. Kwa sasa asijali sana suala la ukabila, aangalie "kazi tu".

mbona waovu wengi unawarudisha bungeni? mambo ya Ndani Adadi Rajabu asaidiwe na Kangi Lugola, wote wanajua changamoto za polisi kwani walikuwa polisi tena wa ranks kubwa tu
 
Listi yako imejaa wale wale

Tunasubiri majina mengi ambayo hatujayazoea kuna wengi wana sifa za kuwa viongozi na ujuzi mwingi wa kubadili na kuendesha serikali.
 
Kwanini umempachika Mwakyembe uwaziri mkuu ? Kwahiyo ni kweli kwamba ' tatizo lilikuwa uwaziri mkuu ' ?
 
Siafiki baraza lako,hujafanya vetting muafaka.Nina mashaka na ufahamu wako kuhusiana na uadilifu wa uliowapendekeza.
 
haahaa akiteua hivo maghufuli atakuwa ametuangusha mno watanzania. eti wasira,mshama,ummy mwalimu dah...
 
Wabunge wenyewe ndiyo hao,,, unadhani atatoa wapi wengine!
Lakini pia lazima ajaribu ku-balamce wapya na wazoefu, vijana na wazee..lazima pia kuwe na some sort of continuity, huwezi kuanza completely na watu wapya.
Lazima uwe na watu kama Wassira kusaidia kupunguza makali ya wapinzani hasa bungeni. Katika hao 32 wa kwenye kampeni kuna baadhi hawakuwa wasaliti.

Mwakyembe nimempendekeza kwa sababu ya umahiri wa sheria na kujieleza na ufuatiliaji. Waziri Mkuu wa Tanzania
lazima awe na sifa hizo.
asali yao, huyo waziri wa Ulinzi na mjeda kamili (Maj Gen) na siyo Amos Makala kama ulivyodhani. Alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi na sasa ni Balozi kwa Comrade Mugabe alikotoka Adadi.

Najua Lugora ni kachero, hivyo atatusaidia kwenye TAMISEMI akianza kama Naibu...
 
Last edited by a moderator:
1. Wizara ya Afrika Mashariki iwekwe ndani ya wizara ya Mambo ya Nje.

2. Wizara ya 17 na ya 21 zina tofauti gani?

3. Wizara ya 23 ivunjwe, haina maana.
 
Twende kwenye serikali za MAJIMBO Nchi hii kubwa sana daima naona tuwaze juu ya kuwa na MAJIMBO kama sera ya CHADEMA ilivyokuwa ingawa inaweze kuchukua muda. Lakini pia kukosa katiba imara!
 
Asumpta mshama wa nini...atafanya nini,mtu anaetuambia kupatana marekani na cuba tz ina maslai...r u seriously
 
1. Wizara ya Afrika Mashariki iwekwe ndani ya wizara ya Mambo ya Nje.

2. Wizara ya 17 na ya 21 zina tofauti gani?

3. Wizara ya 23 ivunjwe, haina maana.

Thanks for the observations:
Hiyo ya Afrika Mashariki ni muhimu tukawa nayo ili tuweze kufuatilia kwa karibu masuala ya Utangamano (Integration) pamoja na makandokando ya jirani zetu. Ni nyeti sana, tukizubaa tutaliwa.

Hiyo Namba 17 ni kweli nimekosea: Mawasiliano tutayaingiza kwenye Miundombinu.

Hiyo Namba 23 itakuwepo kwa muda wakati tunaweka sawa masuala ya "kuvutia uwekezaji" Baadaye hiyo ajenda inaweza kuwekwa Wizara ya Fedha kama kitengo.
 
Twende kwenye serikali za MAJIMBO Nchi hii kubwa sana daima naona tuwaze juu ya kuwa na MAJIMBO kama sera ya CHADEMA ilivyokuwa ingawa inaweze kuchukua muda. Lakini pia kukosa katiba imara!

Majimbo mpaka tuwe na Katiba mpya, labda! Kwa sasa inabidi tujipange kuendesha nchi kwa katiba iliyopo...
 
Tunataka sura mpya haswa vijana kina kigwangala, shonza, gama, bashe.. Hao kina Wasira siamini bado kuna mtu anawafikiria watu walioshindwa kabla.
 
Back
Top Bottom