Mapendekezo ya sera mpya ya Habari

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,484
3,400
Ndugu,
Idara ya habari inaandaa mabadiriko ya sera ya utangazaji. Sera inapendekeza kikomo cha umiliki wa vyombo vya habbari. Ukimiliki kituo cha kurusha matangazo ya radio, basi ni radio tu, kama ni TV, basi ni TV tu, kama ni magazeti basi ni magazeti tu.

Sera hii ambayo itafuatiwa na sheria itamtaka mtu yeyote anayemiliki vyombo vyote vya habari, kuamua kuachia vyombo vingine ili abakie na kimoja tu! Atapewa muda usiozidi miaka mitano kuwa ametekeleza sera/sheria hiyo kikamilifu.
Pendekezo la Serikali limeambatishwa.
 
Attachments

  • SERA YA HABARI NA UTANGAZAJI.pdf
    231.1 KB · Views: 952
Last edited by a moderator:
that government is also there so there should be way were by it will leave some of the bodies that it is holding as of now
 
hii ndio tanzania,huu ndio uongozi wetu,haya ndio maisha yetu,tume zoe hatuoni mabadiliko,ila watumbua kuwa wao hawata ongoza hii nchi milele.
 
Kwani watanzania hatuwezi kupaaza sauti zetu tukapinga sera kandamizi kama hizi? Ambazo kwa makusudi serikali inazileta kwa lengo la kujilinda ufisadi na mizengwe yake isiumbuliwe?

But well, ni myaka mitano, naamini myaka mitano ijayo hatutakuwa hapa tulipo, sauti za walala hoi zitakuwa zimeisha anza kusikika!
 
Why Mengi tu na sio Diallo, RA, Kusaga, Mashirka ya dini et al?

Hao wote si wanamiliki vyombo kama TV, Radio, Printing nk

Kila kitu sasa Mengi, inaboa kweli!
 
2.4 UMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI[/B] (kusahihishwa)
Hivi sasa mmiliki mmoj a anaruhusiwa kuwa na zaidi ya chombo
kimoja cha habari. Aidha, baadhi ya vyombo vya habari
vimeanzishwa bila watendaji wenye taaluma. Wamiliki wengine
wa vyombo vya habari hawatoi mafunzo kazini kwa watumishi
wao. Vilevile, baadhi ya vituo vya redio na televisheni yinatumiwa
na wawekezaji na mashirika ya habari ya nje kueneza sera na
utamaduni wa mataifa ya nchi za nje na hivyo kuathiri mila na
utamaduni wetu. Baadhi ya wawekezaji hao wa nje pia
wanadhibiti maudhui ya baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini, na hivyo kuathiri mtazamo wa kizalendo wa wananchi.
2.4.1 Malengo ya Sera
•. Kuendelea kuruhusu mmiliki mmoja kuwa na zaidi ya chombo
kimoja cha habari;
•Kuvifanya vyombo vya habari vizingatie wajibu wa kutoa
huduma kwa manufaa ya umma;
•Kuhakikisha mmiliki wa chombo cha habari ana watendaji
wenyetaaluma; .
•Kuwahamasisha wamiliki wa vyonibo vya habari kuwaendeleza
watumishi wao kitaaluma;
•Kuhakikisha kwamba uendeshaji wa vyombo vya habari
unakuwa mikononi mwa Watanzania, na wageni wanaajiriwa tu
kama utaalam wao haupatikani nchini.
13
2.4.2 Maelekezo ya Sera
•Serikali iendelee kuwaruhusu wamiliki kuwa na zaidi ya
chombo kimoj a cha habari;
•Raia wa nchi za nje wanaweza kuwekeza katika chornbo cha
habari kwa ubia na raia, ill mradi hisa za M tanzania zisiwe
chini ya asilimia 51 kumwezesha kuongoza chombo hicho
wakati wote;.
•Uendeshaji wa vyombo vya habari utakuwa mikononi mwa
Watanzania;
•Wageni wataajiriwa tu kama utaalam wao unaohitajika
haupatikani nchini;
•Serikali iwahamasishe wawekezaji kuanzisha vyombo vya
habari katika maeneo ambayo hayavutii kibiashara;
•Chombo cha habari kisitumiwe kwa manufaa binafsi ya mrniliki
au mtendaji, bali kitatumiwa kwa maslahi ya umma;
•Chombo cha habari kiongozwe na maadili ya taaluma na ya
jamii hus1ka;
•Chombo cha habari kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi
wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu au kuchochea
uhasama;
•Lugha zitakazotumiwa na vyombo vya habari hapa nchini ni
Kiswahili na Kiingereza.
2.3 UMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI
Hivi sasa mmiliki mmoja anaruhusiwa kuwa na vyombo vingi vya
habari tena vya aina tofauti. Lakini athari zake zinaweza kuwa
mbaya, kwani chombo kinaweza kutumika kwa manufaa ya
mmiliki na ya biashara yake, kinaweza kuvuruga usawa katika
mashindano ya kibi kibiashara, na huweza kujiingiza ku ashara, kusaidia upande
saidia mmoja katika malumbano ya kisiasa kisiasa.
Aidha, baadhi ya vyomba vya
habari vimeanzishwa bila watendaji wenye taaluma. Wamiliki
wengine wa vyamba vya habari hawatoi mafunzo kazini kwa
watumishi wao. Vilevile, baadhi ya vitua vya redia na televisheni
vinatumiwa na wawekezaji na mashirika ya habari ya nje kueneza
sera na utamaduni wa mataifa ya nchi za nje na hivyo kuathiri
mila na utamaduni wetu. Baadhi ya wawekezaji hao wa nje pia
14
wanadhibiti maudhui ya baadhi ya vyombo vya habari hapa
nchini, na hivyo kuathiri mtazamo wa kizalendo wa wananchi.
2.3.1 Malengo ya Sera
•Kuweka kikomo cha vyombo vya haba habari mtu mmoja
ri atakavyoruhusiwa kumi kumiliki. iki.
•Kuvifanya vyombo vya habari vizingatie wajibu wa kutoa
huduma kwa manufaa ya umma;
•Kuhakikisha mmiliki wa chombo cha habari ana watendaji
wenye taaluma;
•Kuwahamasisha wamiliki wa vyombo vya habari kuwaendeleza
watumishi wao kitaaluma;
•Kuhakikisha kwamba uendeshaji wa vyombo vya habari
unakuwa mikononi mwa Watanzania, na wageni wanaajiriwa tu
kama utaalam wao haupatikani nchini.
2.3.2 Maelekezo ya Sera
elekezo •SerikaZi imruhusu mtu mmoja kumiZiki aina moja tu ya
chombo ch cha habari, kama ni magazeti, au redio au teZevisheni,
a na siyo vyote kwa wakati mmoja. (MmiZiki aZiyenavyo sasa
apewe muda wa miaka mitano kuuza hisa~za vyombo vyake
vingine).
•Mwekezaji wa nje katika chombo cha habari atawekeza
kufuatana na sera hii na shena inayoitekeleza, siyo iZe ya Kituo
cha Uwekezaji cha Tanzania (TIC).
•Raia wa nchi za nje wanaweza kuwekeza katika chombo cha
habari kwa ubia na raia, ili mradi hisa za Mtanzania zisiwe chini
ya asilimia 51 kumwezesha kuongoza chombo hicho wakati
wote; .
•Uendeshaji wa vyombo vya habari Jtakuwa mikononi mwa
Watanzania;
•Wageni wataajiriwa tu kama utaalam wao unaohitajika
haupatikani nchini;
15
•Serikali iwahamasishe wawekezaji kuanzisha vyombo vya
habari katika maeneo ambayo hayavutii kibiashara;
•Chombo cha habari kisitumiwe kwa manufaa bin.afsi ya
mmiWd au mtendaji, bali kitatumiwa kwa maslahi ya umma;
•Chombo cha habari kiongozwe na maadili ya taalurna na ya
jamii husika;
•Chombo cha habari kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi
wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu au kuchochea
uhasama;
•Lugha zitakazotumiwa na vyombo vya habari hapa nchini ni
Kiswahili na Kiingereza.
 
Inasikitisha.Tatizo siyo kuwa na Vyombo vingi vya habari. kama alivyo sema Waziri mkuu Mizengo Pinda kwamba kupambana na Mafisadi ni kazi ngumu kwani wana nguvu ya fedha na mtandao mkubwa.je wenzangu mmewahi kusikia habari za kundi la mafia lilivyo sumbua nchi huko Italy. kuja kujua ni kuwa hata baadhi ya watumishi wa serikali ya nchi hiyo walikuwa ni miongoni mwa kundi hilo.
Hivyo tusishangae kusikia Sera kama hiyo ni sehemu ya mapambano magumu ya kukomesha ufisadi kwani vyombo vya habari vinawachoma kama moto.
 
as long as the same standard applies to the government and the ruling party.. I'm fine with it.. I don't think it is targetted to Mengi.. kwani wao wakitafuta njia ya kukwepa sera hiyo na wengine nao watafanya hivyo hivyo.. kwanini wasiamue tu na kusema mfanyabiashara asiwe na biashara ya zaidi ya aina moja. Kama umeamua kuuza karanga usiuze nyanya na kama una dry cleaning usiwe na duka la nguo! One businessman, One product policy!
 
Sidhani kama haya mabadiliko yanamuhusu Mengi.
Mabadiliko haya nimeanza kuyasikia siku nyingi karibu miaka 3 hivi.
Kam utekelezaji wake umekuja wakati Mengi anagombana na Mafisadi sioni kwa nini mtu aunganishe na kusema ni sheri aya kumbana Mengi.
Hii ni sheria inayoibana mpaka serikali??
 
Ingekuwa umiliki wa biashara zote Tanzania unalazimisha Mtanzania kuwa na zaidi ya 51% sidhani kama tungekuwa tunaongelea Mabuzwagi na Mabarick hapa JF.
 
Ndugu,
Idara ya habari inaandaa mabadiriko ya sera ya utangazaji. Sera inapendekeza kikomo cha umiliki wa vyombo vya habbari. Ukimiliki kituo cha kurusha matangazo ya radio, basi ni radio tu, kama ni TV, basi ni TV tu, kama ni magazeti basi ni magazeti tu.
Sera hii ambayo itafuatiwa na sheria itamtaka Bwn. RM anayemiliki vyombo vyote vya habari, kuamua kuachia vyombo vingine ili abakie na kimoja tu! Atapewa muda usiozidi miaka mitano kuwa ametekeleza sera/sheria hiyo kikamilifu.
Pendekezo la Serikali limeambatishwa.

Kwanini lazima mtaje mengi wengine wenye vyombo vya habari vingi hawapo?

Mnachefua, mbona wenye star tv, msanii africa, radio free africa, n.k. hamuwataji?
 
Kwanini lazima mtaje mengi wengine wenye vyombo vya habari vingi hawapo?

Mnachefua, mbona wenye star tv, msanii africa, radio free africa, n.k. hamuwataji?

kwa kuwa mabadiliko haya yana mlenga Bwn.Mengi ndio maana akamtaja.
 
Masikini Soko Huria TZ. Naona wamesau sera kwa watumiaji pia,iwe ni marufuku kutumia chombo cha habari zaidi ya kimoja,Kama wewe ni msoma magazeti ni marufuku kusikiliza radio na kuangalia TV... Tatizo ni kuwa watunga sera wetu ufikiriaji wao sio endelevu,wanafikiri mara na kukoma kufikiri tena...
 
Sidhani kama haya mabadiliko yanamuhusu Mengi.
Mabadiliko haya nimeanza kuyasikia siku nyingi karibu miaka 3 hivi.
Kam utekelezaji wake umekuja wakati Mengi anagombana na Mafisadi sioni kwa nini mtu aunganishe na kusema ni sheri aya kumbana Mengi.
Hii ni sheria inayoibana mpaka serikali??

Madilu, jaribu kukumbuka sakata la Malima na Mengi miaka 3 iliyopita. Kamati ya Bunge iliyoundwa ilikusudia kutaoa tamko sawa na mapendekezo ya mabadiliko ya sasa. Kamati ilishindwa kuafikiana na huo ukawa mwisho wa njama hizo. Kuna haja ya kuunganisha matukio ndugu yangu! Mkakati wa kumnyang'anya Mengi nguvu ya vyombo vya habari ulianza 2006!
 
Watendaji wa serikali Hawakawii kujipiga risasi ya mguu kwa kutamani sana mshiko kama Changudoa ambaye hajaopolewa kwa muda wa wiki nzima.

Hivi nyie watendaji wa serikali mtaendelea kukubali kutongozwa na kudharirishwa na wenye fedha hadi lini??

Du!
 
Duh!,MWM umeniacha hoi hapa, hhahaahah!! hapa umeongea nafikiri mpaka watakapoona kuwa wameisha athirika na kujutia kuwa maharagwe ya mbeya.
 
Back
Top Bottom