Mapendekezo: Liwepo jukwaa la hadithi na story

Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
4,817
6,442
Mods hongereni kwa kazi kubwa mnayoifanya humu JF. Napendekeza liwepo jukwaa au kipengele cha hadithi na story kama zile za kikosi cha kisasi, Njama, Ntakupata tu, na zingine. Mimi ni mpenzi mzuri sana wa hadithi na story mbali mbali ila napata shida sana humu kuzisoma hizo hadithi katika jukwaa la entertainment. Hadithi zote zimewekwa na thread zingine ambazo hazihusiani na hadithi kwenye jukwaa la Entertainment. Ukiingia kwenye hili jukwaa unakutana na thread nyingi sana mpaka unachanganyikiwa. Napendekeza hizi hadithi ziwe katika kipengele chake au jukwaa lake ili ukiingia tu ni mwendo hadithi tu mpaka mwisho. Fanyeni kama kwenye jukwaa la Jamii intellegence (Ukiingia humo wala haupotei na haujuti unakutana na the Bold na wengine ni mwendo wa kusoma tu ambapo ni tofauti ukiingia kwenye jukwaa la Entertainment ambapo hadithi ni za kutafuta kama umendondosha nati ya saa kwenye majani)
Kazi njema
 
Itakuwa poa

Sent from my HUAWEI LUA-L21 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom