Mapendekezo kwa serikali kuhusu namna ya kuondoa omba omba

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061
2,000
Nashauri viongozi wafanye yafuatayo kuondoa omba omba kwenye miji mikubwa, si ungi mkono kuwa na omba omba lakini kuna omba omba wa aina mbili, Omba omba wa kweli na wa uongo. Wa kweli ni wale ambao unakuta mtu kweli anamatatizo na hana namna ya kujikimu, kama ugonjwa na uzee, lakini wa uongo ni wale ambao wamefanya kuwa njia ya kujikimu na wananguvu za kufanya kazi lakini hawataki kufanya kazi.

Watanzania kwa umoja wetu na upendo tukiamua tunaweza kuwasaidia hawa ndugu zetu na kubadilisha hali zao za kimaisha.

Watanzania tupo milioni 45 na kila mtanzania akatoa shilingi elfu 1 tu yaani 45,000,000 x 1,000 = 45,000,000,000. Ambazo ni fedha nyingi sana, nimesema kila mtu elfu 1 tu, kuna wengine ni watoto siyo wote watatoa, lakini kuna wengine watatoa milioni 1 hapo anakuwa amewatolea watu elfu 1. Hii elfu moja kwa kila mtu ni wastani. Hizi fedha zikagawanywa kwa kila kanda 4 billion 8 = billion 32 baki billion 13 kwa ajili ya kanda ya pwani sababu ina omba omba wengi.

Hizi fedha zikifanya yafuatavyo:-

i. Kununua hekari 200 kwa kila kanda (Kaskazini, Ziwa Victoria, Kati, Kusini na Pwani) yaani hekari 1,000 x 2,000,000 = 2,000,000,000

ii. Kujenga mabweni ya kisasa kwa ajili ya kulala watu, kuchimba visima na wale ombaomba wenye nguvu kutumika kufanya kazi hapo kambini.(skim za umwagiliaji)n.k

iii. Kujenga shule kwa ajili ya watoto wa omba omba na wa mazingira magumu.

iv. Kujenga zahanati kwa ajili ya kuwahudumia.

v. Kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi (walimu, wataalamu wa afya, wataalamu wa kilimo, uvuvi, walinzi na wengineo).

vi. Kununua trecta za kisasa kwa kila kanda kwa ajili ya kilimo.

vii. Kununua mifungo(Ng’ombe, Mbuzi, Kuku, samaki, nyuki nk).

Fedha hizi zikisimamiwa vizuri omba omba watapata mazingira bora na watafundishwa kujitengemea na wazee wasiojiweza watahamishiwa huko hatimaye tutakuwa na taifa lenye maadili mazuri.


Hapa tutakuwa tumewawezesha kujitegemea kupitia miradi yao wenyewe.

Viongozi wakizisimamia hasa kwa utawala huu wa hapa kazi tu, mambo yataenda vizuri badala ya kuwafukunza tu mjini na hawajui wanaenda wapi.

Viongozi wakifanya kampeni/kuhamasisha fedha hizi zitapatikana, mimi nitalipia watu 30 yaani elfu 30 nitatoa kwa kuanza. Tunaweza kuchangia kupitia Vodacom, tigo pesa, Airtel money nk.

Kampeni hii inaweza kufanyika ndani ya mwezi mmoja tu.


Angalizo

Fedha zisimamiwe na Raisi au Waziri Mkuu.

Mambo yapo mengi lakini nimeamua kuandika machache kulingana na muda naamini kuna wachumi wazuri Tanzania wanaweza kuandika andiko zuri zaidi yangu.


Naomba kuwasilisha kutoka Babati Manyara.


Tuwasiliane

0715-163816

Isack

Babati – Manyara.
 

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,487
2,000
wewe ni great thinker, unastahili pongezi. kimsingi tunahitaji ubunifu sio kuomba. Hata hao omba omba wamekosa ubunifu, vijijini kuna maeneo mengi sana yalio wazi, vijiji vinaweza kuwa na mpango wa kuwasaidia wasio weza, kwa kuweka mipango bunifu
 

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,448
2,000
Ndugu umejitahidi saana kuwaza. Lakini je, mahitaji ya hao ombaomba ni kukaa mashambani? Kila mtu ana sababu iliyomfanya afikie hali ile. Sidhani kama ni ardhi au kuishi kama kundi. Maana huko walipotoka kuna ardhi, shule na hospitali. Kifupi ni kwamba huwezi kuwalazimisha binadam kuwa na mfumo mmoja. Hao watu wana matatizo na yana tofautiana. Wengine watashamiri katika mazingira hayo na wengine watatokomoea. Athari zaidi ni kwamba zoezi hilo litawachukua hata wale wasiostahili
 

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,448
2,000
Hapo kama ni usaidizi ni target approach. Kuna wengine huo ndio mfumo wa maisha tangu mababu. Lengo kuu lianze na watoto na kina mama. Hawa wasikilizwe na waonekane watu. Huko nyuma hawa walishawahi kubebwa kwenye malori na kupelekwa mikoani. Hapa ni kutarget kundi maalum kupitia idara ya ustawi wa jamii, kuwapa ushauri nasaha na muelekeo kimaisha. Wengine wamekimbia ubakaji au kupigwa na manyanyaso. Wanaona vyema hali ile na si kudundwa kila siku. Watoto nao wengine ni yatima, watukutu, wamekimbia unyanyasaji.
Narudia tena, ufumbuzi wa matatizo haya hauwezi kufanana.
 

Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,488
2,000
achen mambo ya ajabu...mnazuia watu kuomba wakati ninyi kama nchi ni ombaomba maarufu duniani.......achien ombaomba...kwa sababu mwombaji yupo kwa sababu mtoaji yupo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom