Mapendekezo: Hivi ndivyo Serikali inapaswa kuwa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,318
8,228
Mawaziri na Spika: Waziri mkuu, mawaziri wa wizara, spika wa bunge na naibu spika wa bunge wanatakiwa wasiwe wabunge.

Matokeo ya uchaguzi Mkuu: Matokeo ya uchaguzi mkuu yahojiwe mahakamani.

Tume huru ya uchaguzi: Kuwepo na tume huru ya uchaguzi isiyoteuliwa.

Tume ya uchaguzi iwe ni taasisi inayohusisha watu wenye taaluma hiyo na waajiriwe kama wafanyakazi wengine wa umma mfano hakimu, dakitari mwalimu n.k na isiwe tume yenye watendaji wanaoteuliwa.

Mwanasheria mkuu, jaji mkuu na viongozi wengine wa mahakama wasiteuliwe, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na viongozi wengine wa tume wasiteuliwe, mawaziri wasiteuliwe, wakuu wa mikoa na wilaya wasiteuliwe

Mgombea binafsi: Mgombea binafsi awepo.

Kuwawajijibisha wabunge: Wananchi wawajibishe wabunge wavivu.

Uhuru wa makama: Mahakama iwe huru kazi zote za mahakama ziachwe zifanywe na mahakama kama upatikanaji kwa majaji, jaji mkuu na mwanasheria mkuu wa serikali.

Elimu ya kiongozi: Elimu ya diwani iwe kuanzia sitashahada (diploma). Elimu ya mbunge iwe kuanzia shahada (degree). Elimu ya waziri iwe kuanzia shahada ya uzamili (masters).

Muda wa kuwa kiongozi: Muda wa kuwa diwani uwe mwisho miaka 10, Muda wa kuwa mbunge uwe mwisho miaka 10. Muda wa kuwa waziri uwe mwisho miaka 10.

Waziri mkuu na mawaziri wa wizara: Waziri mkuu na mawaziri wa wizara wasiwe wabunge bali wawe wasomi wenye elimu kuanzia shahada ya uzamili wenye uzoefu na kazi za wizara husika na wapitishwe na bunge na mahakama kwa kufanyiwa vetting na kuangaliwa juu ya record zao za uko nyuma.

Mawaziri wa wizara: wawe na elimu, maarifa, uzoefu na ujuzi wa wizara watakazofanyia kazi.

Sera ya Elimu: Sera ya Elimu iwekwe kwenye katiba ili hata akija kiongozi mwingine asiweze kuibadirisha. Watanzania waweze kusoma bure elimu ya msingi na sekondani na elimu yote ibezi kwenye technical education.

Sera ya Afya na Bima: Tuwe na sera ya bima kwa watu wote ambayo iwe ni lazima kwa kila mtu. Utengenezwe mfumo wa kila raia kuwa na bima ya bei nafuu. Na tuwatambue masikini wote wanaoishi chini ya dola moja kwa siku na hao wapewe bima bure ndani ya katiba.

Wala Rushwa na Mafisadi: Ingizwe adhabu ya kifo kwa wala rushwa na Mafisadi.

Mifuko ya Hifadhi ya jamii: Mifuko ya Hifadhi ya jamii hasa sekta binafsi kama NSSF isisimamiwe na Serikali bali isimamiwe na vyama vya wafanyakazi.

Fao la kujitoa: Fao la kujitoa iwe haki ya mfanyakazi.

Karibuni kwa maoni kama unanyongeza tafadhari ongezea hapa au kama kuna kitu nimesahau au hakipo sawa ongezea.
 
Umeongea vizuri, ila eneo la siasa kwangu naona haliitaji sana elimu kubwa hasa kwa wabunge, mawaziri ni muhimu kuwa na elimu stahiki ya kile anachosimamia.

Kwasababu hawa wenye elimu leo ndio wanatufanye tuishi kama nyumbu (benders fuata upepo).

Huwa naukubali sana Mchango wa mbunge kishimba, huwa anahoja za maana sana, lakini hana hiyo elimu uliyopendekeza hapo.

Changamoto kubwa ya matokeo mabovu ya uendeshaji nchi sio elimu, bali hulka za watu na maisha ya unafiki.

Jaribu kuangalia tendency ya ishu ya uviko kwenye wizara ya afya tangu gonjwa hili kuibuka mpaka sasa,unajifunza nini kwao?!

Tanzania tukiweza kujiheshimu wenyewe,tunaweza tukaheshimu hata kile tunachokipigania.
 
Umeongea vizuri,ila eneo la siasa kwangu naona haliitaji sana elimu kubwa hasa kwa wabunge,mawaziri ni muhimu kuwa na elimu stahiki ya kile anachosimamia...
Hao wenye elimu uliowaona hawafai ni kwasababu wamesoma kwenye serikali iliyoongozwa na wasio na elimu ambao hawakuona umuhimu wa elimu wakawajaza elimu ambayo haiwezi kutatua matatizo. 😂😂😂😂😂Nadhani umenielewa mkuu
 
Hapo kwenye bima iwe bure na elimu bure itakuwa ngumu. Majority ya watanzania hawatachangia chochote hata kama uwezo watakuwa nao. Bei za bima ziwekwe kama kawaida kulingana na uwezo wa mtu, ambaye hawezi kumudu gharama za aina Fulani kuwe na kiwango atakacho mudu kununua. Yaani kuwe na vifurushi kulingana na uwezo wa mtu.
 
Hapo kwenye bima iwe bure na elimu bure itakuwa ngumu. Majority ya watanzania hawatachangia chochote hata kama uwezo watakuwa nao. Bei za bima ziwekwe kama kawaida kulingana na uwezo wa mtu, ambaye hawezi kumudu gharama za aina Fulani kuwe na kiwango atakacho mudu kununua. Yaani kuwe na vifurushi kulingana na uwezo wa mtu.
😂😂😂😂😂😂
 
Kwenye rushwa nadhani adhabu ipungue kuwekwe kipindi kifupi kama labda 20-30 yrs hii iwe kwa viongozi wa kiserikali plus kutaifishwa mali zao.

Na wale wasio viongozi yani wananchi wawe na adhabu zao za kawaida, ili kiongozi akipewa dhamana aone kwamba akiaribu kuna moto mkali unamsubiri
 
Hapo kwenye Mifuko ya hifadhi ya jamii, nitakumpinga. Bora isimamiwe na serikali lakini serikali isiweze kuzitumia kwa mambo yake binafsi, pia kuwe na sera za kuwanufaisha zaidi wachangiaji husika.
 
Tume za uchunguzi:
Nusu ya wajumbe wateuliwe na rais na nusu nyingine wateuliwe na bunge.
 
Safi Sana, Wasomi ndio hawa Sasa

NSSF isimamiwe na Vyama vya wafanyakazi...Hapo wafanyakazi wanasimamia hisa zao ...ni kama Benki binafsi hivi

FAO LA KUJITOA ni haki

Sassa hivi eti skilled people hawapati mafao. Unawanyima intellectual mafao yao, hujui wanauwezo wa kufungua makampuni na kuajiri wengine?

Kuongeza wigo wa Kodi, Bila biashara mpya?
 
WANAOPINGA FAO LAKUJITOA
Mungu awape magonjwa yasiyotibika, mfe vifo vibaya, mkachomwe moto kwa kutuibia pesa zetu.
figo zenu zifeli
mfe kwa kisukari
 
Back
Top Bottom