MAPENDEKEZO: Bima ya nyumba iwe lazima kama ilivyo bima ya gari/vyombo vya moto

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Ukweli ni kwamba majanga ya moto kwenye makazi ya watu ni janga ambalo linagharimu sana maisha ya watu hapa nchini kwetu. Ajali za moto zimekuwa zikitokea na kugharimu maisha si tu ya wanafamilia lakini pia kusababisha uharibifu wa mali ya mhusika aliepata ajali na majirani zake.

Mwisho wa siku ajali hizi zikitokea kumekuwa na hasara kubwa ambayo husababisha matatizo makubwa yanayogharimu pia uhai.

Nashauri: Wabunge mpeleke pendekezo serikalini kuwe na bima ya lazima kama ya vyombo vya moto kwenye issue kama hii; au iwe bima ya maisha kuwa lazima. TIRA mnawajibika kwenye hili kuishauri Wizara ili uje muswada kulinda maisha ya jamii zetu.

279872624-H.jpg
 
Ukweli ni kwamba majanga ya moto kwenye makazi ya watu ni janga ambalo linagharimu sana maisha ya watu hapa nchini kwetu.
Kwahiyo bima inazuia kifo.

Badala ya kuongeza bajeti na vifaa pamoja na watendaji wanaojali kazi yao kwa jeshi la zimamoto na uokoaji unawaza kukusanya mapato.
 
Bima ya moto siyo ya lazima maana ni bima inayo compensate kilichopotea kwa mhusika aliyepoteza mali zake. Bima ya gari ambayo ni ya lazima ni ile third party insurance na iko hivyo kwa kuwa ajali ya vyombo vya usafiri inaweza kuleta madhara ya mtu asiyehusika kabisa kama abiria au mtembea kwa miguu asiyehusika.

Bima hiyo imewekwa kama ulinzi kwa mtu wa tatu (third party). Bima nyingine za magari kama comrehensive au bima ya moto n.k zinamnufaisha mwenye mali tu tu ambaye anaweza hata asipokata hiyo bima loss inaenda kwake peke yake na ndio maana ni za hiari.

Kuna baadhi ya mataifa haswa ya ulaya bima zingine kama bima ya afya ni lazima na ukitaka kwenda lazima ulipie bima ya afya ingawa utasema mbona inamnufaisha mwenye bima peke yake. Kwenye mataifa hayo wao kama mtu akipata tatizo la kiafya lazima walitatue kwa hali yoyote ndipo baadae watoe madai ya huduma kwa mtu yoyote hata kama si raia.

Sasa ili waepukane na kudai mtu asiyenacho wamelazimisha kila mtu aliyepo katika taifa lao lazima awe na bima ya afya.
 
Kuna moments third parties wanakuwa inflicted na janga husika kumbuka kisutu pale jengo lilianguka na kuharibu sana majengo mengine. Je, hao sio third parties. Wanafidiwa vipi kama mhusika hayuko insuranced?
 
Kila kitu tulazimishwe. Nikwambie kwa nchi hii hata kwa kukata bima nyumba yako ikiungua hutalipwa kabisaa nchi haina plan B Baada ya plan A ku fail. Kumbuka NSSF unakatwa kwenye hela yako ya mshahara halafu ukiacha kazi hupewi hela yako
 
Tumia akili yako japo kidogo tu kumuelewesha mjinga alipokosea
Tulia ujifunze kwa wenye akili. Watu wenye akili hawacrash hoja wanachangia kama alivyofanya funzadume hapo juu. Kucrash hoja ni upopoma uliotukuka. Hoja huwa inajibiwa kwa hoja sio kuicrash wala kuikimbia. Leta hoja kwa nilichopost.
 
wewe wa utopolo nini Kila kitu tulazimishwe. Nikwambie kwa nchi hii hata kwa kukata bima nyumba yako ikiungua hutalipwa kabisaa nchi haina plan B Baada ya plan A ku fail. Kumbuka NSSF unakatwa kwenye hela yako ya mshahara halafu ukiacha kazi hupewi hela yako
Tupambane.
 
Ni vizuri ungeanza kuchekecha akili yako vizuri pia. Maisha yenyewe hapa makato kama yote unataka utulete msala mwingine!! Nimekutukana tayari mkuu
Hapana hata hujatukana. Umetoa hoja vizuri sana mbona, tena hoja ya mashiko.

Sasa maisha kama yanabana na makato ni mengi tusiweke insurance?. Ina maana insurance haina maana yoyote? Wenzetu wanafanya kwanini sisi tusifanye.
 
By the way kunayo TIRA kudhibiti ujanjaujanja wa malipo ya compensation za bima.
 
Bima ya gari ambayo ni ya lazima ni ile third party insurance na iko hivyo kwa kuwa ajali ya vyombo vya usafiri inaweza kuleta madhara ya mtu asiyehusika kabisa kama abiria au mtembea kwa miguu asiyehusika.
Hivi hawa bima huwa wanawalipa kweli wahanga wa ajali za magari kama mabasi nk?
 
Hivi hawa bima huwa wanawalipa kweli wahanga wa ajali za magari kama mabasi nk?
Binafsi nishalipwa mara mbili tena kampuni za bima za baniani...sasa hivi kuna Mamlaka ya udhibiti wa bima TIRA makampuni ya bima yamepunguza urasimu. Muhimu ufuate utaratibu tu kitu ambacho wabongo huwa hatupendi tunapenda ukipata janga uletewe fidia ofisini kwako
 
Binafsi nishalipwa mara mbili tena kampuni za bima za baniani...sasa hivi kuna Mamlaka ya udhibiti wa bima TIRA makampuni ya bima yamepunguza urasimu. Muhimu ufuate utaratibu tu kitu ambacho wabongo huwa hatupendi tunapenda ukipata janga uletewe fidia ofisini kwako
Si kuletewa huduma ofisini, ila changamoto ni kwamba mashirika ya Bima yalikuwa yanazungusha sana wahanga wa majanga kiasi cha kukatia tamaa kutokana na gharama za ufuatiliaji (safari za kwenda na kurudi mijini yaliko maofisi ya bima) kuwa kubwa
 
Naunga mkono hoja ila makampuni ya bima yaliokuwa serious tu kama gari za mil 10 wanakuwa wababaishaji vipi kwa mjengo wa mil 100?
 
Tuangalie ufanisi wa hizi zilizopo kwanza mfano third part insurance je wahanga wanafaidika nayo kweli?

Siungi mkono hoja.
 
Usipende kulinganisha nchi na nchi, wakati hatuja wafikia kimaendeleo hata robo,wenzetu wapo makini kwa vitu vyao.Hapa kitu chako ila utasumbuliwa utadhani unadhurumu Serikali.
Hapana hata hujatukana. Umetoa hoja vizuri sana mbona, tena hoja ya mashiko.

Sasa maisha kama yanabana na makato ni mengi tusiweke insurance?. Ina maana insurance haina maana yoyote? Wenzetu wanafanya kwanini sisi tusifanye.
 
Usipende kulinganisha nchi na nchi, wakati hatuja wafikia kimaendeleo hata robo,wenzetu wapo makini kwa vitu vyao.Hapa kitu chako ila utasumbuliwa utadhani unadhurumu Serikali.
Naona bima ya makazi ndo suluhu kwa sababu tayari tuna makazi ambayo hayajapangiliwa hivyo kuboresha zima moto bado haitasaidia sana so tujikite kwenye bima. Ila sie ni uchumi wa kati kumbuka mkuu.
 
Back
Top Bottom