Mapendekeko: Namna sahihi ya kuwasherekhea mashujaa wote waliopeteza maisha Mo29

Mapendekeko: Namna sahihi ya kuwasherekhea mashujaa wote waliopeteza maisha Mo29

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
1,413
Reaction score
5,150
Wakati tukiwa njiani kuindea D9 , nivyema tukawakumbuka mashujaa wote walioanguka kwa ajili ya Tanganyika kuanzia Siku ya 29.10.2025 nakuendelea.
Binafsi nitapenda machache yafuatayo yafanyike kuwaenzi wenzetu na sisi wengine tulioko njiani kuwafuata huko waliko kuanzia Siku ya D9 nakuendelea.

1) Pasipo kujali Imani zetu tufanye sala na maombi kuwaombea wapendwa wetu bila kusahau kuomba haki ya Kila marehemu ilipwe kwa matendo yake🙏

2) tusiwashe umeme Siku hiyo usiku , bali tuwashe mishumaa majumbani mwetu mpaka asubuhi , sababu adui yetu alituvizia tukiwa gizani na kututendea mabaya kwa ukatili mkubwa.

3) Zipigwe baruti zaheshima kulingana na Kila mmoja wetu atakavyowiwa kulingana na eneo Siku hiyo itakapo mkuta.

4) Sisi kama waTanganyika nyama iwe haramu kwetu kwa Siku tatu kuanzia tarehe 29/10 mpaka tarehe 02/10 Kila mwaka ili kuwaenzi wenzetu.!

Yangu ni hayo machache ila ninaimani wenye hekima ni wengi humu kuniliko Mimi mwehu , mnakaribishwa kuchangia namna sahihi ya kuwaenzi wenzetu na sisi maana tu njiani
 
Kama ikiwezekana iandaliwe orodha ya wahanga wote nchi nzima [ kutoka kila mkoa] na iweze kutunzwa kwenye National archives kama ukumbusho kwa vizazi vijavyo.
 
9 december tunakwenda kuwaheshimisha wale wote waliopoteza uhai, kujeruhuliwa na kupewa ulemavu 🔥
 
Wazo zuri japo hilo la kuzima taa lifanyike kwa dakika chache tu.

Ni kama nilishawahi kuona sehemu kuna nchi hua inafanya hvyo, kama kumbukumbu zangu zipo sawa ni American hua wanazima taa zote zisizo za muhimu sana kwa dakika moja kama ishara ya kumpa heshima mgunduzi wa kwanza wa light bulb 💡 Thomas Edison.
 
Back
Top Bottom