Mapato ya Zanzibar yafikia shilingi bilioni 2874, sawa na trilioni 2.874 kwa mwaka. Tanzania Bara tunayo ya kujifunza kutoka Zanzibar

Mkuu huyo akili yake ni nyepesi sana. Hivi kweli Unaweza sema uchumi wa mikoa Kama Dar na Mwanza upande kwa asilimia 7 Kama uchumi wa Rwanda kisa idadi ya watu na ukubwa vinakaribiana kulingana?
Kwani haiwezekani?! Nakumbuka miaka michache iliyopita uchumi wa California ulikuwa ni sawa na uchumi wa Ufaransa huku uchumi wa Los Angeles peke yake, ukiwiana na uchumi wa nchi mzima ya Malaysia! Na kwa sasa, nadhani California imeshaiacha Ufaransa including many other developed European countries.

Dar es salaam kwa mfano, kama haiizidi Zanzibar basi nitashangaa sana.
 
Taarifa yako inaukweli sehemu ya Zanzibar kukusanya Tsh2T+ kwa mwaka basi. Ila kwenye kulinganisha mikoa ya Tz bara na Zanzibar hapo taarifa imejaa unafiki na upotoshaji. Huwezi ukasema mkoa kama wa kigoma,Geita,Simiyu na n.k idadi ya watu kila mkoa heti ni sawa na idadi ya watu wote Zanzibar.

Harafu kitu kingine umeshindwa kutambua vitu vinavyochangia mapato kuongezeka. Nikutoe tu ushamba kuwa idadi ya watu haichangii Sana kuongezeka kwa mapato Bali vyanzo vya uchumi ndo vinafanya uchumi kuongezeka.

Taarifa yako Ni nyepesi Sana haina hoja za kiuchumi kabisaa.
Sasa kama mshindi wa kiti cha urais anapatikana kwa kura chini ya 300000 huo si sawa na mkoa mmoja wa bara?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbuka znz ni nchi hivyo inakusanya mapato yote ya kodi na yasiyo ya kodi, import duties, ports,domestic revenues,tozo za serikali na taasisi zake, na mgao, tofauti na mikoa, haikusanyi kodi zaidi ya tozo za kawaida za serikali za mtaa.kama kungekuwa na mfumo wa znz mkoa kama Dar ungekuwa na asilimia zaidi sitini ya. mapato, Arusha $ za utalii zote etc
 
Taarifa yako inaukweli sehemu ya Zanzibar kukusanya Tsh2T+ kwa mwaka basi. Ila kwenye kulinganisha mikoa ya Tz bara na Zanzibar hapo taarifa imejaa unafiki na upotoshaji. Huwezi ukasema mkoa kama wa kigoma,Geita,Simiyu na n.k idadi ya watu kila mkoa heti ni sawa na idadi ya watu wote Zanzibar.

Harafu kitu kingine umeshindwa kutambua vitu vinavyochangia mapato kuongezeka. Nikutoe tu ushamba kuwa idadi ya watu haichangii Sana kuongezeka kwa mapato Bali vyanzo vya uchumi ndo vinafanya uchumi kuongezeka.

Taarifa yako Ni nyepesi Sana haina hoja za kiuchumi kabisaa.
Nakubaliana na wewe juu ya kutaja vyanzo vya mapato.
Ukiacha vyanzo vya Customs, mikoa ya Tanzania Bara ina vyanzo vingi sana vya mapato ambavyo havipati msukumo stahiki kutoka Serikalini
 
Mkuu huyo akili yake ni nyepesi sana. Hivi kweli Unaweza sema uchumi wa mikoa Kama Dar na Mwanza upande kwa asilimia 7 Kama uchumi wa Rwanda kisa idadi ya watu na ukubwa vinakaribiana kulingana?
Lengo letu kama ni kujifunza kutoka Zanzibar, naamini yapo yenye manufaa.
Nimewahi kusoma kuwa mapato ya Jimbo la California, nchini Marekani, ni makubwa kuliko nchi kadhaa duniani.
Tanzania imejaliwa mito, maziwa, ardhi na maliasili kadha wa kadha.
Tukijipanga kuimarisha uzalishaji katika nyanja mbalimbali katika mikoa yetu, mapato yataboreka.
 
Sawa haina shida. Mapato ni Mali ya muungano.
Vipi deni letu la tanesco ameshalipa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi, naamini lilikuwa jambo la aibu kulitangaza sana deni la Serikali ya Zanzibar kudaiwa na Tanesco.
Sote tunafahamu kuwa Taasisi nyingi za Serikali ya Muungano zinadaiwa sana na Tanesco.
Utangazaji wa madeni ya umeme ya Serikali na Taasisi zake kutoka kwenye Taasisi nyingine ya Serikali ilikuwa ukosefu wa nidhamu.
 
Kasomee uchumi kwanza ndo uje uanze kupuyanga hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninaheshimu sana elimu pamoja na Wasomi.
Lakini ukweli ni kwamba wazalishaji wa mazao na bidhaa hapa kwetu Tanzania siyo Wasomi.
Angalia Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wachimba madini, na Wamachinga.
Kama kada hizi zitasaidiwa na hao Wachumi, kwa kupewa elimu halisi ya vitendo, hakika huo 'Uchumi unaosomwa Vyuo Vikuu' utaongezeka na kuimarisha Uchumi wa Nchi.
 
Mkuu unaweza kuwa na hoja lakini zanzibar ina sovereignty yake tofauti na mikoa ya Tanzania bara hasa halmashauri. Mikoa kama Geita ikivuna rasilimali zote zinaenda dodoma kwanza ndio zinapangiwa kazi ya kufanya ila zanzibar licha ya udogo wa eneo au idadi sawa na mikoa yetu ila inajitegemea kiutawala hivyo ni rahisi kuretain mapato yake unayoona makubwa.

Mfano Halmashauri za huku bara ziliporwa kodi ya majengo ikaenda serikali kuu..... Gesi ya mtwara ni ya serikali sio halmashauri ya Mtwara n.k. kule kigoma ujiji halmashauri ilitaka kuingia MoU na mashirika ya nje kuwekeza miradi mbalimbali ya maendeleo ila yalitaka wasaini OGI ambayo serikali ya Tanzania ilijitoa. Mwisho wa siku mradi ukafa ila ingekua zanzibar jambo lingeamuliwa mara moja na baraza la wawakilishi na wangevuna hiyo miradi kuboost mapato ya ndani ila bara mpaka dodoma ndio iamue kwa niaba ya Halmashauri.

Suluhisho ili tuwe sawa ungesema sera ya ugatuzi wa majimbo Mtwara ijikamulie gesi yake na korosho.... Geita wavune dhahabu zao etc trust me kuna mikoa ingekua na mapato ya ndani makubwa kuliko hata hyo zanzibar kwa mbali sana ila ingekua na cost zake kwa mikoa ambayo bado haijawa na rasilimali za kutosha.
Bandiko lako lina hoja nzito na za msingi.
Wazo langu mimi ni jepesi.
Mathalani, mazao ya michikichi yakiongezeka mara mbili au mara tano, Uchumi wa nchi si utaimarika?
Nchi inaagiza mafuta mengi ya kula toka nje, kwa nini Mikoa yetu isiweke mkazo kwenye kilimo cha Michikichi huko Kigoma, Alizeti katika mikoa ya Kati na ya Kusini, na kadhalika.
Tunaona jinsi Rais Dr. Shein anavyofuatilia kilimo cha Karafuu, Mpunga, Mboga za Majani na kadhalika huko Zanzibar.
Huku kwetu ufuatiliaji unakuwa kama wa kufuata mkumbo.
Mwaka juzi kulikuwa na mkazo wa kilimo cha Mikorosho. Nani anafuatilia kama miche ile iliyogawiwa inaendelea kukua?
Zanzibar ufuatiliaji upo mpaka wakati wa mavuno.
 
Back
Top Bottom