Mapato ya Korosho yafikia Sh Trilioni 1. 08

Mapato ya Korosho yafikia Sh Trilioni 1. 08

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,314
Reaction score
12,821
MAPATO YA KOROSHO YAFIKIA TRILIONI 1.08 HADI SASA

MAPATO kutokana na mauzo ya korosho katika msimu wa 2017/2018 katika mikoa minne ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma yamepanda na kufikia sh. trilioni 1.08 ikilinganishwa na misimu miwili iliyopita.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Bw. Hassan Jarufu alitoa taarifa hiyo jana jioni (Jumapili, Desemba 31, 2017) wakati akitoa ufafanuzi juu ya uzalishaji na mauzo ya zao la korosho nchini hadi kufikia mwisho wa mwaka 2017.

“Ukiangalia msimu wa mwaka 2015/2016, utaona kuwa korosho zilizozalishwa zilikuwa kidogo zaidi. Msimu huo ziliuzwa kilo 155,244,645 zikiwa na thamani ya sh. 388,474,530,906.00 ikilinganisha na msimu wa 2016/2017 ambapo jumla ya kilo 265,237,845.00 ziliuzwa zikiwa na thamani ya sh. 871,462,989,284.00,” alisema.

Alisema katika minada 10 ya msimu wa 2017/2018, mauzo ya korosho yamefikia kilo 285,828,205 zenye thamani ya sh. 1,082,200,383,581.00. “Mnada wa 10 ulikuwa tarehe 21 Desemba, 2017 na minada bado inaendelea kwa msimu wa 2017/2018,” alisema.

Akitoa ufafanuzi wa mauzo hayo kwa kila mikoa hadi kufikia mnada wa 10, Bw. Jarufu alisema Mkoa wa Mtwara umeongoza kwa kuuza tani 178,165.741 zenye thamani ya sh. 701,674,466,366.00 ukifuatiwa na mkoa wa Lindi ambao umeuza tani 68,687.504 zenye thamani ya sh. 247,163,294,296.00.

“Mkoa wa Ruvuma umeuza tani 19,545.613 zenye thamani ya sh. 76,173,400,063.00 na mkoa wa Pwani umeuza tani 19,429.347 zenye thamani ya sh. 57,189,224,856.00 na kufanya mapato yote kwa mwaka huu kufikia sh. trilioni 1.082,” alisema.

Bw. Jarufu alitoa ufafanuzi huo mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 kwa msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni: “Korosho ni dhahabu ya kijani, tuitunze, itutunze”.

Bw. Jarufu alimweleza Waziri Mkuu kwamba Bodi ya Korosho Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za wilaya, imeendelea kutekeleza mpango wa miaka mitatu wa kupanda mikorosho 10,000,000 kila mwaka.

“Katika mpango huu, wastani wa mikorosho 5,000 inatarajiwa kupandwa katika kila kijiji au mikorosho 30 kwa kaya kwa mwaka, sawa na ekari 330,000 kwa mwaka kwa nchi mzima. Lengo la mpango huu ni kuongeza kiasi cha korosho kinachozalishwa nchini kwa kuongeza wigo wa halmashauri zinazozalisha korosho na kupanda miche inayotokana na mbegu bora zenye uzalishaji mkubwa na zenye ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu,” alisema.

Alisema katika msimu wa 2017/2018, Bodi ya korosho inaratibu uzalishaji wa jumla ya miche 14,001,820 ambayo imetokana na tani 100 (kilo100, 000) zilizozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele.

“Mchanganuo wake ni kama ifuatavyo: kilo 31,170 za mbegu zitapandwa shambani moja kwa moja ambazo zitatoa jumla ya miche 2,181,900; kilo 68,830 zitazalisha jumla ya miche 11,819,920 kati ya miche hiyo isiyobebeshwa ni 9,636,200 na miche itakayobebeshwa ni 2,183,720.

“Ni matumaini yetu kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Februari 2018, miche yote itakuwa tayari imezalishwa, kugawanywa na kupandwa katika mashamba ya wakulima,” aliongeza.

Mkurugenzi huyo alisema, katika msimu huu eneo la utekelezaji wa mradi limeongezeka kutoka Halmashauri 51 za msimu uliopita 2016/2017 hadi kufikia Halmashauri 90 nchi nzima ikiwemo mikoa mipya iliyothibitishwa kustawi zao la korosho hapa nchini.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya, baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele walishiriki uzinduzi huo.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
 
MAPATO kutokana na mauzo ya korosho katika msimu wa 2017/2018 katika mikoa minne ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma, yamepanda na kufi kia Sh trilioni 1.08 ikilinganishwa na misimu miwili iliyopita.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Hassan Jarufu, wakati akifafanua juu ya uzalishaji na mauzo ya zao la korosho nchini hadi kufikia mwisho wa mwaka 2017.

Korosho ni zao la biashara linaloongozwa kwa Tanzania. Inaiingizia Tanzania takribani asilimia 15 za fedha za kigeni. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), kwa Afrika, Tanzania inashika nafasi ya nne kwa uzalishaji wa korosho ikizalisha asilimia 20 ya korosho zote, lakini kwa duniani, inashika nafasi ya nane.

Kwa Afrika inazidiwa na Nigeria, Ivory Coast na Guinea- Bissau. Zao la korosho linalimwa na kustawi zaidi katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Ruvuma. Jarufu, katika taarifa yake juzi alisema; “Ukiangalia msimu wa mwaka 2015/2016, utaona kuwa korosho zilizozalishwa zilikuwa kidogo zaidi.

Msimu huo ziliuzwa kilo 155,244,645 zikiwa na thamani ya shilingi 388,474,530,906 ikilinganisha na msimu wa 2016/2017 ambapo jumla ya kilo 265,237,845 ziliuzwa zikiwa na thamani ya shilingi 871,462,989,284,” alisema.

Alisema katika minada 10 ya msimu wa 2017/2018, mauzo ya korosho yamefikia kilo 285,828,205 zenye thamani ya Sh 1,082,200,383,581. “Mnada wa 10 ulikuwa Desemba 21, 2017 na minada bado inaendelea kwa msimu wa 2017/2018,” alisema.

Akidadanua mauzo hayo kwa kila mikoa hadi kufikia mnada wa 10, Jarufu alisema Mtwara umeongoza kwa kuuza tani 178,165.741 zenye thamani ya Sh 701,674,466,366 ukifuatiwa na mkoa wa Lindi ambao umeuza tani 68,687.504 zenye thamani ya Sh 247,163,294,296.

“Mkoa wa Ruvuma umeuza tani 19,545.613 zenye thamani ya shilingi 76,173,400,063 na mkoa wa Pwani umeuza tani 19,429.347 zenye thamani ya shilingi 57,189,224,856 na kufanya mapato yote kwa mwaka huu kufikia shilingi trilioni 1.082,” alisema.

Jarufu alitoa ufafanuzi huo baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 kwa msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni: “Korosho ni dhahabu ya kijani, tuitunze, itutunze”. Alimweleza Waziri Mkuu kuwa, Bodi ya Korosho Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele iliyopo Mtwara, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za wilaya, imeendelea kutekeleza mpango wa miaka mitatu wa kupanda mikorosho 10,000,000 kila mwaka.

“Katika mpango huu, wastani wa mikorosho 5,000 inatarajiwa kupandwa katika kila kijiji au mikorosho 30 kwa kaya kwa mwaka, sawa na ekari 330,000 kwa mwaka kwa nchi mzima.

Lengo la mpango huu ni kuongeza kiasi cha korosho kinachozalishwa nchini kwa kuongeza wigo wa halmashauri zinazozalisha korosho na kupanda miche inayotokana na mbegu bora zenye uzalishaji mkubwa na zenye ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu,” alisema.

Alisema katika msimu wa 2017/2018, Bodi ya korosho inaratibu uzalishaji wa jumla ya miche 14,001,820 ambayo imetokana na tani 100 (kilo 100,000) zilizozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele.
 
Kwa mwaka ulioishia sekta ya kilimo katika zao la korosho imezidi kuimarika kulinganisha na pato la mwaka 2016.

Mwaka uliomalizika wa 2017 sekta hii imeshuhudia kipato cha sh trilioni 1.1 kulinganisha na bilioni kama 800 hivi za mwaka 2016.

Korosho ni zao linaloweza kuwainua watu wa pwani na kusini kama likiendelea kuwekewa msisitizo.

Kwa wale wanaolialia mtandaoni eti vyuma vimekaza basi waende pwani na kusini wakaone wanaume wa kazi wanavyolainisha vyuma.

SIASA MWISHO 2015 HAPA NA SASA NI KAZI TU.


Farmers pocket over 1.08 trn/- in cashew sales


HERI YA MWAKA MPYA!
 
Zungumzia sekta ya KILIMO nchini sio kuzungumzia zao moja la korosho Ebo!
sekta ya Kilimo IPO uvunguni mwa kitanda cha plastiki.

Agrarian Revolution in Europe haikutokana na zao moja tu, bali mazao mengi ya kilimo. Sasa wewe unatuletea hadaa na mbwembwe za ajabu ajabu na kutupotezea malengo kama Taifa. Huu uchumia tumbo ni hatari kwa vizazi vya aina yako!
 
Utashangazwa zaidi ukifika kwa hao wakulima wanaoitwa wa KOROSHO hali zao duni kupitiliza
 
Huu ni mwelekeo mzuri sana kwa maendeleo ya taifa.
 
Zungumzia sekta ya KILIMO nchini sio kuzungumzia zao moja la korosho Ebo!
sekta ya Kilimo IPO uvunguni mwa kitanda cha plastiki.

Agrarian Revolution in Europe haikutokana na zao moja tu, bali mazao mengi ya kilimo. Sasa wewe unatuletea hadaa na mbwembwe za ajabu ajabu na kutupotezea malengo kama Taifa. Huu uchumia tumbo ni hatari kwa vizazi vya aina yako!
Mahindi yapo wala wala mchele ndio usiseme ndio maana hatuna njaa.

Wewe na roho yako ya korosho nieleze eneo la kilimo lisilofanya vyema kwa sasa.
 
Kwa mwaka ulioishia sekta ya kilimo katika zao la korosho imezidi kuimarika kulinganisha na pato la mwaka 2016.

Mwaka uliomalizika wa 2017 sekta hii imeshuhudia kipato cha sh trilioni 1.1 kulinganisha na bilioni kama 800 hivi za mwaka 2016.

Korosho ni zao linaloweza kuwainua watu wa pwani na kusini kama likiendelea kuwekewa msisitizo.

Kwa wale wanaolialia mtandaoni eti vyuma vimekaza basi waende pwani na kusini wakaone wanaume wa kazi wanavyolainisha vyuma.

SIASA MWISHO 2015 HAPA NA SASA NI KAZI TU.


HERI YA MWAKA MPYA!
Umesema vizuri mkuu,Korosho sasa hivi ni green Gold..
 
Kumbe hela wanazo lakini hawataki kunilioa hela zangu? Mm mbona sujalipwa mpaka sasa?
 
Mahindi yapo wala wala mchele ndio usiseme ndio maana hatuna njaa.

Wewe na roho yako ya korosho nieleze eneo la kilimo lisilofanya vyema kwa sasa.
Acha siasa wewe leta uchambuzi wa sekta ya kilimo kwa ujumla wake acha kuja na zao moja tenà linalolimwa kusini mwa nchi tu!
 
Acha siasa wewe leta uchambuzi wa sekta ya kilimo kwa ujumla wake acha kuja na zao moja tenà linalolimwa kusini mwa nchi tu!
Wewe usiyefanya siasa lete uchambuzi wako.!
 
Jambo jema

Kwa wazelendo wa kweli kama mimi

Ila kwa wasaliti, vibaraka wa wazungu na wasaka madaraka kwa nguvu (Zito, Mgonjwa Tindu, DJ Mboe, Fisadi Luwasa) kwao habari kama hiyo si jambo jema kwani huwapunguzia ajenda za kupigia kelele
 
Back
Top Bottom