TEMILUGODA
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 1,389
- 285
1.Unyonge kitu kibaya,hushindwa kudai haki, Mengi aliona wabaya,papa kuhodhi haki, Mola akishalipanga,muda huja muafaka, kasa wameshakazana,papa wanachinjwachinjwa. 2.papa walikula noti,mvuvi alipozama, Madawa yale kulevya,papa wamelindalinda. Meno ya tembo yaisha,papa wanaangamiza, Kasa wameshakazana,papa wanachinjwachinwa.