Mapambano ya kutengeneza Mashuja wapya wa kupinga ukoloni mpya.

Mapambano ya kutengeneza Mashuja wapya wa kupinga ukoloni mpya.

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,619
Kwanini wizara mpya ya uwekezaji imepelekwa ikulu? Kwanini isingeachwa huko nje ya ikulu...?

Tundu Lissu aliwahilalamika takriban mwezi 1 nyuma akihoji kwanini idara ile nyeti (jiongeze kujuwa ni ipi hiyo) imepelekwa ikulu?

Hizi ni hatua za dhahir shahir kuthibitisha kuwa dhamiri za warasimu (Madalali na Mawakala) zipo za kulinda ukoloni mpya.

Taifa (bila kujuwa) linajiandaa kutengeneza mashujaa wapya wa mapambano dhidi ya ukoloni mpya.

Vizazi vyetu vitasoma kwenye historia mashujaa wa kizazi cha pili cha kupambana na ukoloni wa pili.

Nani watakuwa front kujiumba Mashujaa Mkwawa, Abushiri, Songea, Chabruma, Mirambo, Isike, Mangi Meli, Mangi Meza, Kidaha, Mkwavinyika Mwinyigumba Mwamuyinga, Mukama, Kinjikitile Ngwale wa kizazi hiki kipya?

Tanzania inapokea harakati hizi toka kwa mataifa mengine yaliyoanza kama Afrika Kusini, Kenya, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, DR Congo, Nigeria, Afrika Kaskazini mwa Sahara.

Zipo nchi zilizofanikiwa na zipo zilizozama jumla kwenye mapambano haya bila tija.

Angalia GDP (Nominal) za Afrika 2022.

Nigeria (16.87%)
Egypt (15.70%)
South Africa (13.77%)
Algeria (6.26%)
Morocco (4.78%)
Kenya (4.18%)
Ethiopia (3.72%)
Tanzania (2.56%)
Ghana (2.54%)
Other Countries (25.78%)

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom