masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,894
- 15,116
KAMA NDO HIVYO NITAENDAJE HUKO NA VEROSSA YANGU SI ITAHARIBIKA KWA HIZO BARABARA MBOVU NDAN YA UWANJA?
CC😡Ntuzu
ni kwenda kwa ngondi tu huko!
Yap yap! Tutaenda!
Nimetembelea leo viwanja vya Saba Saba.
Naleo vilikuwa vinatembelewa na kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais Zanzibar.
Tatizo nililoliona ni lile lile la miaka yote.
Vumbi na uchafu.
Vumbi kutokana na barabara za ndani kuwa na mashimo, na vile vile vumbi kutokana na vifusi.
Cha kushangaza ni kuwa TANTRADE wanakuwa na mwaka mzima wa kujiamdaa, lakini shughuli zinaanza mwezi wa tano au sita.
Mbaya zaidi ni sehemu ya barabara inyopakana na jeshi.
Barabara ni mbaya mno na leo kulikuwa na tope kabisa, hata kupiga grader hakuna.Akili inasema hii barabara pamoja na parking yake vingewekwa lami ili hata tozo ya shillingi elfu nne iwe na maana.
Kule ndani , vibanda vingi sana wala havijakamilika, hasa mndani ya PTA, na lile banda la waonyeshaji wengi.
Hata hivyo kilichonifurahisha mwaka huu ni kuwa na exhibitors wengi wa ndani hasa bidhaa za ngozi-viatu, mikanda mabegi n.k. Hapo nimejipatia pair mbili za viatu pure leather!!
TANTRADE wanatakiwa kubadilika na kufikiri kidogo.
Maonyesho ya mwakani waanze sasa kwa kuweka lami ndani ya kiwanja kizima.
Sijui kama Waziri Kigoda analielewa hilo?
Mkuu kwa kweli viatu nilivyoninia ni fashionable, Travolta, na ni ngozi pure.pinda anasema maonesho yasifanyike mwaka mmoja patengezwe, sijui wanataka kujenga shopping mall?!! btw, kama umevipenda viatu vya nyumbani ni vyema ukaongelea kidogo kuhusu kampuni inayotengeza viatu hivyo, au hata ubandike kipeperushi chao na picha za viatu hata ulivyonunua, ndiyo hasa lengo la maonesho mkuu, tuungane mkono!
Miafrika Ndivyo Tulivyo - Nyani Ngabu.
Watanzania ni wazi akili zetu zimejifunga na ndio maana tumeshindwa kubadilisha jinsi ya kufikiri.
Hebu fikiria hizo enzi tangia mji una watu laki nane na kampuni zikiwa RTC na NMC, leo hii mji una wakaazi zaidi ya million tano na na uchumi wenye makampuni zaidi ya laki moja lakini kakiwanja ni kale kale na hakuna hata mwenye wazo la kusogea mbele kutafuta walau heka hamsini na kujenga maeneo mapya!
Watasema 'pesa za kufanya hayo hamna' wakati yakiteketea mabilioni ya kufanya vitu hivyo hivyo hata mara mia.
Hapafai kwenda kabisa, ikiwa umeshaina Trade Fair za wenzetu wa nje ya Tanzania, hapo hurudi tena, ni kujitesa tu.
Ndiyo maana hata exhibitors wanakuwa siyo wale wa maana sana, ni hivi vikampuni uchwara tu vya nje vinavyokuja kuuza vibiashara uchwara. Weka exhibition waje akina Boeing, waje akina Raytheon, Waje akina Hyundai. Waoneshe maajabu ya dunia.
Nilienda mwaka juzi, baada ya nusu saa nikaondoka mbio. Fujo tupu, barabara mbovu, hakuna mpangilio wa maana, makelele utafikiri upo uwanja wa fisi (hata Uwanja wa Fisi siku hizi wamestaarabika).
Kwa kweli inasikitisha kuona watu walioajiriwa hawajui kufikiri vitu vipya!
Na kwa bahati mwaka huu kuna mabanda ya Wamarekani, India , Indonesia ,Kenya na hata Japan.
Kwa uozo nilouona pale viwanja vya Sabasaba , yaani miundombinu mibovu sana, sidhanii kama watarudi mwakani!
Yaani ni vumbi, vumbi tupu watu wa TANTRADE utafikiri hawaendi Trade Shows nchi za nje, ukweli ni kwamba wanaenda lakini they cant themselves think outside the box.
They lack innovative ideas.
Hapafai kwenda kabisa, ikiwa umeshaina Trade Fair za wenzetu wa nje ya Tanzania, hapo hurudi tena, ni kujitesa tu. Ndiyo maana hata exhibitors wanakuwa siyo wale wa maana sana, ni hivi vikampuni uchwara tu vya nje vinavyokuja kuuza vibiashara uchwara. Weka exhibition waje akina Boeing, waje akina Raytheon, Waje akina Hyundai. Waoneshe maajabu ya dunia. Nilienda mwaka juzi, baada ya nusu saa nikaondoka mbio. Fujo tupu, barabara mbovu, hakuna mpangilio wa maana, makelele utafikiri upo uwanja wa fisi (hata Uwanja wa Fisi siku hizi wamestaarabika).