S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Maoni yangu kuhusu kampeni za kupinga madawa ya kulevya.
1. Mimi naunga mkono kabisa kwa asilimia 100% kwenye hii kampeni.
2. Tatizo ambalo naona si sawa kwangu ni kuwatangaza hadharani na kusema hawa wanajihusisha na dawa za kulevya. Naona si sawa kwa sababu, mosi, nchi hii ni ya utawala wa sheria kwa hiyo mwenye kuthibitisha pasipo na shaka yoyote kuwa fulani anajihusisha na dawa za kulevya ni mahakama tu. Pili, jambo ambalo lingefanyika ni kwamba; kuna watu tumewakamata kwa sababu wanatuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya bila kuwataja majina yao. Pili, tunawahoji au tutawahoji na wengine ambalo tunaona tuna ushahidi tutawapeleka mahakamani na huko wataithibishia mahakama kuwa wao hawajihusishi na dawa za kulevya na watakuwa huru.
3. Kuna kitu kinaitwa BRAND and PERSONALITY mbele ya Jamii. Ukitangazwa hadharani kwamba unajihusisha na madawa ya kulevya utakuwa umechafuka mbele ya jamii na gharama za kujisafisha ni kubwa mno. Kama wewe una biashara kubwa jua kuwa kampuni zitaanza kujitoa kabisa kujihusisha na wewe. Kwa hiyo ni jambo la msingi sana Mimi naona kulitambua hili swala.
Narudia tena, naiunga mkono serikali kwa kupambana na watumiaji wa madawa ya kulevya lakini kuna jambo la msingi sana ambalo tulijiwekea Sisi wenyewe bila kushurutishwa na mtu yoyote jambo hilo ni UTAWALA WA SHERIA
Milard Ayo; mtangazaji wa Cloud FM amemnukuu Waziri Nnape twitter akisema kwamba; "Lazima itumike busara, tusiwahukumu watu kwa tuhuma,kutengeneza brand ni kazi kubwa sana wakati kuibomoa ni jambo la sekunde".
Ni Maoni yangu kama Mwananchi huru kabisa. Nadhani mmemuelewa Nnape alivyosema na maoni yangu nilivyoyaweka hapo juu. Maana mtu ukishamtangaza halafu ikathibitika kuwa hajihusishi na madawa ya kulevya utakuwa umeharibu kabisa image yake binafsi na kibiashara.
Kwa pamoja tuyapinge madawa ya kulevya.
05/02/2017