Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Nimeisoma habari juu ya _"tuhuma za wizi wa kifaru cha Jeshi"_ kwenye gazeti la Dira ya Mtanzania la jana tarehe 20 mwezi June 2016, kisha nikamsikiliza msemaji wa jeshi la wananchi akitoa taarifa kuhusu tuhuma hizo. Ningependa kutoa maoni yafuatayo;
*Kuhusu Mwandishi*
Ukisoma content ya habari hiyo (sio headline) utaona mwandishi ameandika _"very objective"_. Haikua habari ya uchunguzi, ilikua habari ya mahakama. Yani mwandishi alienda mahakamani na kuripoti kile alichokiona na kusikia. Ukisoma habari utagundua kuwa mwandishi hakuweka maoni yake. Yeye aliripoti kitu kilichotokea.
Mwandishi angeweza kuwa hatiani kama kesi hiyo ilikua ya ndani na isiyoruhusu waandishi (In-camera) halafu yeye akairipoti.
Kuna namna mbili za kusikiliza kesi.
*_NamnaYaKwanza; (TRIAL OPEN COURT)._*
Katika utaratibu huu kesi husikiliza kwa uwazi ambapo waandishi huruhusiwa kuingia mahakamani na kuripoti wanayoyaona na kuyasikia. Utaratibu huu kisheria huitwa *_"Trial in open court"._* Member of Public huruhusiwa kuingia chumba cha mahakama na mawakili wa pande zote hubishana kisheria kwa hoja _(arguments with facts &evidence)_ huku umma uliopo mahakamani ukishuhudia.
*_NamnaYaPili; (IN-CAMERA)_*
Katika utaratibu huu, kesi husikilizwa katika mazingira ya siri kutokana na unyeti wake. Umma, wala waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia ktk chumba cha mahakama _(court premises)._ Hairuhusiwi kusikiliza yanayoendelea, kurekodi, wala kushuhudia mwenendo wa kesi au sehemu ya kesi inayosikilizwa. Utaratibu huu kisheria huitwa *_"In-Camera"_*
Kwa kawaida mwandishi au mtu yeyote akiripoti kesi yoyote ambayo inasikilizwa _"In-camera"_ anakuwa amefanya kosa la jinai na anaweza kushtakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi na akipatikana na hatia akaadhibiwa.
Swali la kujiuliza je kesi ya kuhusiana na kifaru ilikuwa inasikilizwa "In-camera??". Jibu ni HAPANA. Ilikua inasikilizwa kwa uwazi (Open court) na waandishi walikua wakiruhusiwa kuingia na kuripoti.
Labda ilitakiwa iendeshwe "In-camera" kutokana na kuhusisha vyombo vya usalama. Lakini je ni kosa la nani kesi hii kuendeshwa openely? Kama kesi hiyo kuendeshwa kwa uwazi ni kosa basi mahakama ndio ilikosea sio mwandishi. Kwahiyo hapa inapaswa kuwajibishwa mahakama ya Mwanzo Kibaha iliyokua inasikiliza kesi hiyo.
*Kuhusu kauli ya JWTZ*
Nimemsikiliza msemaji wa Jeshi la Wananchi Kanali Ngemela Lubinga nimenukuu mambo kadhaa kwake. Amesema Waandishi wajifunze kutafuta habari ktk vyanzo vya kuaminika _(credible sources),_ ameshauri waandishi wapende kusoma, ameshauri waandishi wawe na weledi, ameshauri waandishi wajifunze kwenda beyond the story.
Akahusisha suala na mgogoro wa ardhi, akimtaka mwandishi angekwenda beyond angeweza kujua mengi kuhusu suala hilo. Akashauri waandishi wajue mipaka ya kazi yao. Akashauri waandishi wawe _"evidence based"_ yani wasijiandikie tu bila kuona. Na hapa akatolea mfano wa kifaru kinachodaiwa kuibiwa kuwa hakikua kifaru bali _"skrepa"._
Kwa kifupi Kanali Lubinga ameongea mambo ya msingi lakini njia aliyotumia _sio sahihi_. Amefikisha ujumbe wake _kibabe_ sana na kwa kugha ya _vitisho._ Mbaya zaidi ametaja ukatili na kusema wanaweza kufanya ukatili ikitokea mazingira yanayohitaji kufanya hivyo. Amenukuliwa akisema *_"Sadism is inevitable when the situation is Alarming"._*
Mi nadhani hii kauli si sahihi. Katika nchi ya kidemokrasia jeshi halipaswi kushabikia ukatili. Na kama wanaotakiwa kufanyiwa huo ukatili ni hawa waandishi wasio na fimbo wala silaha yotote zaidi ya kalamu "itz very unfair".
Kama wamekosea wapelekwe mahakamani na wakikutwa na hatia washitakiwe sio kutishia kuwafanyia "ukatili". Nadhani kuna statement nyingine za kijeshi hazipaswi kufika kwa raia. Zinapaswa kuishia hukohuko jeshini.
*Kuhusu Gazeti*
Mwandishi na Mhariri wake wote wametuhumiwa kuandika habari ya uongo. Lakini Je walitunga hiyo habari? Je mahakama ya mwanzo Kibaha haikusikiliza kesi jiyo? Kama kesi ilisikilizwa kwanini mwandishi na Mhariri wake waitwe waongo?
Ukisoma hiyo habari vizuri mwandishi amedai kuwa iyekua mkuu wa polisi wa wilaya hiyo (OCD) ndiye aliyetoa ushahidi mahakamani kuhusu madai ya kuibiwa kifaru hicho. Lakini gazeti hilo linaandika kuwa OCD huyo alishindwa kudhibitisha mbele ya mahakama kuwa kifaru hicho kiliibwa na wananchi hao. Gazeti hilo linasema kuwa OCD alitoa ushahidi wa uongo. Na baada ya kuona ametoa ushahidi wa uongo akaomba ahamishiwe Songea ili kukwepa aibu ya kuwasingizia wananchi hao kuiba kifaru.
Kwa hiyo ukisoma habari hiyo utagundua kuwa Mwandishi alishajua kwamba wananchi hao hawakuiba kifaru bali walisingiziwa na OCD. Sasa kwanini hakuandika _"wananchi wasingiziwa kuiba kifaru??"_.. Kukosa weledi. Bila shaka hii ndio sababu iliyomfanya msemaji wa Jeshi kutaka waandishi wawe na weledi wanapoandika. Kama mwandishi angeandika hivyo basi kesi isingekuwa kwa mwandishi bali huyo OCD. Jeshi lingemuuliza OCD je ni Kifaru gani kimeibiwa? Lini? Wapi? Na nani? _"Burden of proof"_ ingekua juu ya OCD na sio gazeti.
*Kuhusu Kichwa Cha Habari*
Kwa kawaida katika taaluma ya habari kichwa cha habari huandikwa na Mhariri. Mwandishi hutuma story tu, au anaweza kutuma story na _"headline"_ lakini Mhariri akaitoa na kuweka anayoona inafaa. Kwahiyo kama Mhariri ndiye aliyeandika hiyo "headline" anaweza kuwa na kesi ya kujibu. Na kama iliandikwa na Mwandishi mwenyewe basi huyo mwandishi pia atakuwa na kesi ya kujibu.
Hii ni kwa sababu headline hiyo imehukumu kabla ya hukumu ya mahakama. Kitaalamu inaitwa _"judgemental headline"._ Yani headline ambayo imeshatoa hukumu kabla ya hukumu yenyewe. Headline inasema "Kifaru cha kivita cha JWTZ chaibwa" yani hapa mhariri ni kama vile alishaprove kuwa ni kweli kifaru hicho kimeibwa kabla hata mahakama haijatoa hukumu.
Kusema kifaru "kimeibwa" wakati haijadhibitika kama kweli au lah, ni kuripoti uongo. Na kuripoti uongo tena taarifa inayoleta taharuki kwa nchi ni kosa la jinai chini ya Sheria ya magazeti ya mwaka 1976 na sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 4 [Newspspers Act 1976 (CAP 229) &National Security Act (section 4)].
Mwandishi hapaswi kuwa hakimu. Kwahiyo alitakiwa kusema _"Kifaru cha JWTZ chadaiwa kuibwa"_ AU _"Wanakijiji wadaiwa kuiba kifaru cha jeshi"_ sio _"Kifaru cha kivita cha JWTZ chaibwa"._
Ukisema jambo linadaiwa kufanyika maana yake hujadhibitisha, lakini ukisema limefanyika maana yake umeshadhibitisha. Ukisema "fulani anadaiwa kufariki", na ukisema "fulani amefariki", ni statement mbili tofauti kbs.
Nirudie maneno ya msemaji wa JWTZ kuwa Waandishi tuwe makini, tupende kujifunza, tuwe na weledi, tutafute vyanzo vya kuaminika, tufuate maadili ya kazi. Kama Mhariri wa Dira ya Mtanzania angeweka tu headline yake vizuri isomeke _"Kifaru cha JWTZ chadaiwa kuibwa"_ pengine yasingemfika yaliyomfika.
*_Malisa G.J_*