Siasa chafu za CCM na usalama wa Waandishi wa Habari

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
3,886
9,186
Baada ya wapinzani, kundi jingine linaloonekana kuteswa na kutaabishwa na ccm, ni hili la waandishi wa habari.

1. Daudi Mwangosi aliuawa na polisi alipokuwa akiripoti maandamano ya chadema.

2. Azory Gwanda alipotezwa na hajulikani alipo sababu ikisemekana ni kuandika habari za uchunguzi kuhusu mauaji ya Kibiti.

3. Spensa Lameck
Huyu alifanyiwa figisu mbaya sana baada ya kuripoti kwa ufanisi mkubwa sana mikutano ya Lowasa alipokuwa akigombea urais kupitia chadema 2015. Mpaka leo hajulikani aliko

4. Mabere Makubi
Huyu aliachishwa kazi ITV kwa amri toka juu, baada ya kuripoti kwa ufanisi mkubwa sana migogoro ya wakulima na wafugaji. Hivi sasa anaishi kwa shida sana. Inasemekana serikali ya jiwe ilihusika.

5. George Maratu
Kapotea kabisa, kazi kaachishwa na duru zinasema serikali ya jiwe ndiyo sababu.

6. Pascal Mayalla
Huyu ni mwandishi nguli na mahiri kweli kweli. Ni mweledi na mwerevu wa kuandika na kuchambua habari za uchunguzi, pia ana uwezo wa kuuliza maswali yanayohitaji majibu mazito. Lakini hivi sasa kapoa kama maji mtungini inasemekana ni kwasababu wakati Ndugai akiwa spika aliitwa bungeni na kupigwa mkwara baada ya kuandika kuwa "bunge ni kibogoyo".

7. Erick Kabendera
Mwandishi wa gazeti la The Economist aliyeandika ukweli kuhusu udikteta wa utawala wa Magufuli. Inasemekana alisulubiwa nusura aage dunia akiwa selo.

8. Saed Kubenea
Huyu aliwahi kumwagiwa tindikali kwenye utawala wa Kikwete kwasabb ya kufichua habari za ufisadi katika serikali ya awamu ya nne.

Shime watanzania tushikamane kupigana na ccm, leo ni zamu ya wapinzani na waandishi wa habari kesho hatujui litafuata kundi gani.
 
6. Pascal Mayalla. Huyu ni mwandishi nguli na mahiri kweli kweli. Ni mweledi na mwerevu wa kuandika na kuchambua habari za uchunguzi, pia ana uwezo wa kuuliza maswali yanayohitaji majibu mazito. Lkn hivi sasa kapoa kama maji mtungini kwasabb wakati Ndugai akiwa spika aliitwa bungeni na kupigwa mkwara baada ya kuandika kuwa "bunge ni kibogoyo".
Mkuu G4N, umenikumbusha Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
Mimi bado nipo nipo na kipindi cha KMT
P
 
Baada ya wapinzani, kundi jingine linaloonekana kuteswa na kutaabishwa na ccm, ni hili la waandishi wa habari.

1. Daudi Mwangosi aliuawa na polisi alipokuwa akiripoti maandamano ya chadema.

2. Azory Gwanda alipotezwa na hajulikani alipo sababu ikisemekana ni kuandika habari za uchunguzi kuhusu mauaji ya Kibiti.

3. Spensa Lameck
Huyu alifanyiwa figisu mbaya sana baada ya kuripoti kwa ufanisi mkubwa sana mikutano ya Lowasa alipokuwa akigombea urais kupitia chadema 2015. Mpaka leo hajulikani aliko

4. Mabere Makubi
Huyu aliachishwa kazi ITV kwa amri toka juu, baada ya kuripoti kwa ufanisi mkubwa sana migogoro ya wakulima na wafugaji. Hivi sasa anaishi kwa shida sana. Inasemekana serikali ya jiwe ilihusika.

5. George Maratu
Kapotea kabisa, kazi kaachishwa na duru zinasema serikali ya jiwe ndiyo sababu.

6. Pascal Mayalla
Huyu ni mwandishi nguli na mahiri kweli kweli. Ni mweledi na mwerevu wa kuandika na kuchambua habari za uchunguzi, pia ana uwezo wa kuuliza maswali yanayohitaji majibu mazito. Lakini hivi sasa kapoa kama maji mtungini inasemekana ni kwasababu wakati Ndugai akiwa spika aliitwa bungeni na kupigwa mkwara baada ya kuandika kuwa "bunge ni kibogoyo".

7. Erick Kabendera
Mwandishi wa gazeti la The Economist aliyeandika ukweli kuhusu udikteta wa utawala wa Magufuli. Inasemekana alisulubiwa nusura aage dunia akiwa selo.

8. Saed Kubenea
Huyu aliwahi kumwagiwa tindikali kwenye utawala wa Kikwete kwasabb ya kufichua habari za ufisadi katika serikali ya awamu ya nne.

Shime watanzania tushikamane kupigana na ccm, leo ni zamu ya wapinzani na waandishi wa habari kesho hatujui litafuata kundi gani.
IMG-20241003-WA0088.jpg
 
Back
Top Bottom