Maoni yangu kuhusu Elimu yetu

HALANGA

New Member
Jan 21, 2021
2
2
Kuna suala ambalo linatakiwa lifanyike kwenye elimu ambapo lingemsaidia Mheshiwa Rais katika suala la kujenga nchi kwenye uchumi wa viwanda.

Tunapojenga uchumi wa viwanda mtaala wa elimu unatakiwa kuwaandaa watoto kuja kuingia kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Hii itafanyika kama mtaala utatambua kuwa shule ni kituo cha kukuza ubunifu. Mtaala wetu hautambui hivyo tutamsaidiaje Mheshimiwa Rais.

Kosa ni kwamba ubunifu wanadhani unatakiwa kufanyika katika ngazi ya elimu ya juu. Eneo la mtaala na namna ya kutekelezaji wake lazima lilenge kukuza ubunifu na zipo model mbalimbali wenzetu wanatumia.

Ndiyo maana kwa wenzetu ubunifu unafanywa na vijana wa shule miaka 14-25, huwezi kuamini lakini ni kwa sababu ya mtaala unatambua shule ni Innovation Centre. SIJUI kwa nini watafiti hawalioni hili.
 
Mwafrika na elimu wapi na wapi? Tupo busy kuanzisha historia ya Tanzania, tunaondoa masomo kama Computer science OLEVEL, Adv mathematics imeondolewa..ujinga ujinga tu kwenye elimu. Badala ya kusisitiza masomo ya sayansi wanaleta habari ya historia ya Tanzania, subiri aje mwingine uone kama halitaondolewa.

Kama una uwezo na vijisenti huu sio mtaala wa kumpeleka mwanao, mtaala unaoamuliwa na wanasiasa na sio wataalamu. ?
 
Mwenzako anataka Watanzania waijue Historia yao, ili eti wawe Wazalendo! Habari ya mitaala yenye mafungumano na teknolojia, elimu ya ufundi, viwanda, kilimo cha kisasa na chenye tija, huo ubunifu, michezo, nk. Wala hana hata habari nayo.
 
Bora umeliona hilo HALANGA. Kuna miss match kwenye maeneo mengi ya Elimu yetu. Kwa ujumla elimu yetu bado inapima uwezo wa mtoto kukumbuka, kuhifadhi kichwani na kuandika alichokiifadhi siku za mitihani basi. Natamani sana angalau kila wilaya iwe na chuo cha veta na kijikite kwenye uchumi wa natural resource za wilaya hiyo na baadaye waendeshe viwanda hivyo. Lkn pia vyuo hivyo vya Veta viwe na uwezo wa kushauri wangependa kupokea wanafunzi wenye foundation gani/zipi kutoka primary n secondary
 
Mwenzako anataka Watanzania waijue Historia yao, ili eti wawe Wazalendo! Habari ya mitaala yenye mafungumano na teknolojia, elimu ya ufundi, viwanda, kilimo cha kisasa na chenye tija, huo ubunifu, michezo, nk. Wala hana hata habari nayo.

Foundations ni muhimu sana kwa makuzi ya watoto. Huwezi kuwa na watu wasiojua history ya nchi yao then utegemee watakuwa wazalendo. Nimewahi kuongea na wajapan kadhaa na nilichogundua ni kwamba hakuna mjapan hata mmoja hasiyejua historia ya bomu la Hiroshima katika kisiwa cha Honshu wakati wa World War II na huwezi kuamini umoja wa wajapan unaanzia hapo
 
Umenena vema ndugu yangu. Hilo ndilo linalotakiwa kwa dunia ya sas na siyo hiyo Historia yake. Haisaidii. Kwa sasa dunia yote inazungumzia uchumi wa viwanda (Industrial economy) ambapo bidhaa zote kutoka kwenye sekta zote za kijamii na kiuchumi kama vile elimu, kilimo, afya, maliasili, n.k sharti zizalishe vitu na watu wanaoweza kuishi na kuendesha maisha kwa kutegemea soko la viwanda kama mazao, viatu,nguo, ndala, mikanda, simu, vipuri mbalimbali, n.k.

Sasa huyu mwenzetu anatataka twende kinyumenyume badala ya kwenda mbele. Nilivutiwa sana na ubunifu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ndugu Antony Mtaka ambaye mkoani kwake walianza kutebgeneza Chaki. Hivyo hata watoto wakimaliza shule wengine wangeingia kwenye shughuli hiyo na wengine shughuli nyingine. Sasa unakazania eti Historia ya kwamba fulani alikuwa Rais wa awamu ya tano na alijenga flyover ubungo. Baada ya hiyo Historia nini kinaendelea kwa huyu mwanafunzi?

Kwa kweli viapawa vya watoto huanza kutambuliwa, kukuzwa na kuendelezwa mapema kabisa katika umri wao mdogo na siyo kwenye utu uzima wa chuo Kikuu. Ndiyo maana tunakwama sana kuendelea kwa Sababu hata utafiti mtaala wetu unakazia zaidi kwa watu wa vyuo vikuu wakati hata ngazi za chini zingefanya kwa sehemu yao. Mtaalamu mmoja aitwaye Howard anasema binadamu wana vipawa tofauti tofauti (multiple Intelligences) kwa kufaidishana hivyo hata elimu itambue hivyo na isiwafundishe watoto wote kwa njia moja tu.

Wataalamu wa Elimu wapo wa kutosha kabisa na wanalijua hili ila wameamua kuwaachia na kwa kweli wamewazilia wanasiasa wafanye watakavyo. Na sisi jamii tukiendelea kuwasikiliza wanasiasa tunakipoteza kizazi hiki kabisa!
 
Foundations ni muhimu sana kwa makuzi ya watoto. Huwezi kuwa na watu wasiojua history ya nchi yao then utegemee watakuwa wazalendo. Nimewahi kuongea na wajapan kadhaa na nilichogundua ni kwamba hakuna mjapan hata mmoja hasiyejua historia ya bomu la Hiroshima katika kisiwa cha Honshu wakati wa World War II na huwezi kuamini umoja wa wajapan unaanzia hapo
Hivi ni Historia gani ya nchi yetu tusiyoijua? Mbona hamuweki wazi? Yaani wewe hadi leo hujui Tanzania ilitawaliwa nani? Hujui viongozi wa koo mbalimbali kama akina Mkwawa? Hujui Tanzania iliitwa Tanganyika kabla? Huji Rais wa kwanza wa nchi yetu aliitwa nani?

Naomba mtwambie yafuatayo:
1. Mmejuaje kwamba watanzania hawajui Historia yao?
2. Akina nani hao ambao hawajui Historia ya nchi yao?
3. Nani hasa atalisoma hilo somo laHistoria mnalotengeneza?
4. Je, huyo atakayesoma hilo somo ndiye mwenye tatizo?
5. Je, ni sisi watu wazima ndio tumeonyesha kutoijua Historia ya nchi yetu? Kama jibu ni ndiyo, je, tutarudishwa darasani?
6. Nani kafanya tathmini na utafiti wa ukubwa wa tatizo?

NB: Msije mkatuletea mihemko yenu ya kisiasa na ushamba/ ulimbukeni wa madaraka kuharibu kizazi chetu kwa kuwalisha matango pori yenu ya kijani.
 
Mimi nadhani siku tutakapoamua kuweka katiba ambayo itapiga marufuku wanasiasa kuchezea elimu yetu ndio utakaokuwa mwanzo wa kuwa na elimu bora. Haiwezwkani kila mwanasiasa anafanya mabadiliko kwenye elimu ilimradi atimize matakwa yake.
 
Mwenzako anataka Watanzania waijue Historia yao, ili eti wawe Wazalendo! Habari ya mitaala yenye mafungumano na teknolojia, elimu ya ufundi, viwanda, kilimo cha kisasa na chenye tija, huo ubunifu, michezo, nk. Wala hana hata habari nayo.
Amejuaje kwamba watanzania shida yao ya kukosa gloves na madawa hospitalini ni kwa sababu hawajui Historia ya nchi yao? Ni Historia ipi hiyo mbona hawaiweki wazi? Wanataka kutushitukiza tu na Historia yenye habari za Jiwe na Chato mwanzo mwisho?
 
Napiga picha ya kitabu cha Historia mpya chenye Sura Sita chenye Dibaji iliyoandikwa na Mtukufu mkuu:
1. Juu ya kanda la kitabu kutakuwa na picha ya Chato Airport.
2. Sura ya kwanza: Mbuga za Wanyama Chato
3. Sura ya Pili: Harakati za Kuhamia Dodoma kipindi cha utawala wa Awamu ya tano chini ya jemadari, mtukufu JEIPIEM
4. Sura ya Tatu: Uongozi wa Awamu ya Tano na Ujasiri wa Kiongozi Mkuu
S. Sura ya Nne: Ujenzi wa Ukuta wa Mererani awamu ya Tano
6. Sura ya Tano: Ujenzi wa barabara za juu na reli ya kisasa awamu ya Tano
7. Sura ya Sita: Usaliti wa Tundu Lissu.
Sura hii ya mwisho itaambatana na sahihi ya Jemadari wa awamu ya Tano.
 
Tuna rais ambaye anafikiri anajua kila kitu, mbaya zaidi maagizo anayatoa akiwa jukwaani. Kwa wale tuliosoma history na siasa ambayo baadae ilikuwa inaitwa civics mtaala ulikuwa umejitosheleza kabisa ila mafaraka ya katiba yanampa fursa mtu mmoja kuwa juu ya kila kitu haya ndio matokeo yake
 
Back
Top Bottom