Jana katika kipima joto cha ITV, yalitolewa mapendekezo au maoni kutoka kwa wanajopo wa kipindi hicho kwamba kutokana na usumbufu wa kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara au maandamano, yawe ya kisiasa au ya namna yoyote pamoja na mahakama kuruhusu, walipendekeza taarifa ya masaa 48 ambayo ilikuwa inatolewa kwa Polisi sasa itolewe kwa msajili wa vyama vya siasa na msajili atoe go ahead.
MAONI YANGU:
Bado naona urasimu waweza kuwa palepale hata kama msajili akifanya kazi hiyo, mimi napendekeza kazi hii ibaki kazi ya mahakama kama ilivyo sasa na kusiwe na kutoa taarifa Polisi na kama Polisi wana sababu yoyote ya kuzuia shughuli hiyo waende mahakamani.
Wewe una maoni gani?