Uchaguzi 2020 Maoni yangu juu ya mchakato wa mgombea urais CHADEMA

kali KENYATTA

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
288
166
Mpaka sasa CHADEMA ina watia nia watano kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwenye ushindani huu; namuona Tundu Lissu akishindana kwa ukaribu zaidi na Mwenyekiti wa chama ndungu Aikaeli Freeman Mbowe ukiachilia wagombea wengine watatu. Hii ni kwa sababu ya ushwawishi walionao ndani na nje ya chama chao.

Je, mchakato wa mwaka huu wa kumpata mpeperusha bendara ya CHADEMA unaharibiwa kwa Mwenyekiti kutia nia? Hasa ikizingatiwa kwamba wapenzi na wanachama wa CHADEMA walikuwa wameishafanya hitimisho juu ya uteuzi wa ndugu Tundu Lissu? Ambae kwa mtizamo na imani yao ndiye pekee anayeonekana anaweza kumkabili mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)?

La hasha, CHADEMA kama chama kinachojipambanua kuishi na kuienzi Demokrasia; kinapaswa kuwa mfano. Matendo yana kishindo kuliko maneno. Hivyo basi, CHADEMA inataka kuiambia jamii ya wapenda siasa zenye kufuata Demokrasia kwamba, kinaishi kwa matendo yale wanayoyahubiri. Hili ni jambo jema sana kama vyombo vinavyosimamia mchakato wa maamuzi vitatenda kazi yake kwa uwazi, bila upendeleo au msukumo wowote usiokua na dalili za kuienzi Demokrasia ndani ya CHADEMA . Historia itajengeka na heshima itatamalaki kwenye duru za siasa hizo. Vilevile, CHADEMA itakua inasahihisha makosa ya michakato kama hii ya huko nyuma. Kila mpenda Demokrasia ataimba mapambao ya ushindi kwamba DEMOKRASIA imeamua.

Kupata upinzani ndani ya mchakato wa CHADEMA kwa ndugu Tundu Lissu kuna faida nyingi. Mosi, kwa kawaida kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Pili, ushindi bila ushindani mgumu hauna hamasa. Watoto wa mjini wanasema, "atachukulia poa." Tatu, mchakato mgumu ndani ya CHADEMA unamuandaa mshindi vyema kwenda kukabiliana na hatua ya kushindana na CCM akiwa ameiva. Kwa mfano; wanamasumbwi hujiandaa sawa sawa na mpinzani atakayepambana nae. Hivyo basi, mchakato mgumu ndani ya CHADEMA ni maandalizi mazuri ya kumfanya mshindi awe ameiva kupambana na CCM.

Natambua hamu, matamanio na imani waliyonayo wale wanaosema Tundu Lissu apewe kijiti kwa kuwa anatosha. Hata hivyo, njia hii si sahihi sana. Inafanya uchaguzi kukosa hamasa. CCM mara nyingi wamefanya maajabu kwenye michakato yao ya kumsaka mgombea wa kiti cha Urais. Kwa mfano, hakuna aliyetegemea kwamba John Pombe Magufuli angelikua mgombea wa urais kupitia CCM mwaka 2015. Mchakato wao ndani ya chama uliitikisa nchi, macho yote yalihamia Dodoma. Kila mpenzi na mfuatiliaji wa siasa za Tanzania hakupenda kupitwa na tukio lolote. Hii ni nafasi nzuri ya CHADEMA kuboresha pale CCM wanapokosea, hasa pale wanapobaki makundi kinzani baada ya kuisha kwa mchakato wa ndani. Ni fursa kwa CHADEMA kuanzisha safari mpya ya matumaini na siasa zenye kulenga kujisahihisha na kuwa mfano wa kuigwa.


Mwisho, nawatakia CHADEMA mchakato mwema. Mchakato wenye uwazi, usiopendelea mtu kwa ubaguzi wowote ule, na wenye kuboresha umoja kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020.
 
Mungu ibariki Chadema
Chama la wana.. Tumaini la kizazi kipya..
IMG_20200531_072737_186.jpg
 
Je, mchakato wa mwaka huu wa kumpata mpeperusha bendara ya CDM unaharibiwa kwa Mwenyekiti kutia nia? Hasa ikizingatiwa kwamba wapenzi na wanachama wa CDM walikua wameishafanya hitimisho juu ya uteuzi wa ndugu Tundu Lissu? Ambae kwa mtizamo na imani yao ndiye pekee anayeonekana anaweza kumkabili mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)?

.
Hilo hitimisho la wanachadema la uteuzi wa Lisu kama mgombea lilifanyika tarehe ngapi mwezi gani mwaka gani na wapi?
 
Yeyote kati ya hao watano waliojitokeza kutia nia, anao uwezo mzuri sana wa kumkabiri mtesi wao bila ya shaka yoyote, hata kama kila mmoja wao anazo sifa zake zinazomtofautisha.

Kujitokeza kwa hao watano sioni sababu ya kuwepo wasiwasi ndani ya chama chao.

Kila mmoja ajinadi kadri awezavyo, na mwisho wa yote, mmoja wao apatikane kwa haki, kutokana na watakavyompima watakaohusika katika kumpitisha.

Na kama haya hayafanywi kwa sababu za 'mkakati' maalum waujuao wao CHADEMA, kujitokeza kwao ni ishara nzuri na kuonyesha ukomavu wa chama chao.

Wamejiwekea utaratibu wa jinsi mgombea atakavyopatikana; na kama kazi hiyo itafanyika kwa ufanisi, kwa nini pawepo na sintofahamu kati yao!

Acha hawa wapiga debe walioko nje ya chama wahangaike, lakini mwisho wa siku, heshima itakuwa kwa CHADEMA.
 
Je, wapenzi na wanachama wa Chadema ndio vyombo vya uteuzi wa wagombea?

Nimeandika kumaanisha kwamba kwa upande wao walikua wanasubiri Mh. Tundu Lissu apitishwe na vyombo husika tu.
 
Je, wapenzi na wanachama wa Chadema ndio vyombo vya uteuzi wa wagombea?

Nimeandika kumaanisha kwamba kwa upande wao walikua wanasubiri Mh. Tundu Lissu apitishwe na vyombo husika tu.
hizo takwimu za kusema wanachadema walikuwa wanasubiri ziweke hapa ni wa wapi ,walikaa wapi kufanya hayo maamuzi na minute za vikao vyao weka hapa
 
hizo takwimu za kusema wanachadema walikuwa wanasubiri ziweke hapa ni wa wapi ,walikaa wapi kufanya hayo maamuzi na minute za vikao vyao weka hapa
Huna mantiki kwenye inquiry yako. Hata nikisema wana-chadema 3,500,000 utabisha?

Unataka minutes za matamanio ya watu? Kwamba wewe ukimtamani binti fulani, wengine wataomba uwape minutes kuthibitisha matamanio yako?

Usipende kuusaka ukweli kwa njia za panya.
 
Huna mantiki kwenye inquiry yako. Hata nikisema wana-chadema 3,500,000 utabisha?

Unataka minutes za matamanio ya watu? Kwamba wewe ukimtamani binti fulani, wengine wataomba uwape minutes kuthibitisha matamanio yako?

Usipende kuusaka ukweli kwa njia za panya.
HUNA HOJA UMEANDIKA NDOTO ZAKO UNASINGIZIA OO WANACHADEMA WALISHAAMUA
 
HUNA HOJA UMEANDIKA NDOTO ZAKO UNASINGIZIA OO WANACHADEMA WALISHAAMUA
Mh. Tundu Lissu ni chaguo la wengi ndani ya CDM. Kama ilivyokua mwaka 2015 kwa "wengi" waliopenda Lowassa apitishwe kuwa mgombea wa CCM.

Tatizo lako unataka kuhesabu maji kwa kutumia tarakimu. Kwamba kuna maji 1,2 mpaka 10. Huwezi kupima upepo unavumaje kisiasa. Ndio maana unaomba nikupatie minutes. Kimsingi umekaririshwa.
 
Kutia Nia kwa Mbowe kumeitia nuksi safari ya TL. Kwa sasa makundi hayataepukika na utakuwa mwisho wa umaarufu wa Cdm
 
Kutia Nia kwa Mbowe kumeitia nuksi safari ya TL. Kwa sasa makundi hayataepukika na utakuwa mwisho wa umaarufu wa Cdm
Kama ni chama cha demokrasia watavuka, kama demokrasia IPO mdomoni tu hawatavuka.huu Ni wakati Wa viongozi Wa chadema kuonesha uongozi sahihi kwa chama chao.
 
Kutia Nia kwa Mbowe kumeitia nuksi safari ya TL. Kwa sasa makundi hayataepukika na utakuwa mwisho wa umaarufu wa Cdm
Ndio uzuri na ubaya wa Demokrasia. Lakini kama kweli wana nia, malengo na matamanio yanayofanana; basi watavuka salama.
 
Back
Top Bottom