Independent Prosecutor
Member
- Nov 14, 2015
- 9
- 19
Nimelelewa nikiaminishwa kwamba mimi ni bora kuliko kundi lingine la kidini (Nikiwa Mkirsto) nikaaminishwa kuwa jamii yetu ni jamii bora na nikaaminishwa kuwa hakuna la muhimu kwa wengine ila kwetu tu. Lakini nikawa ninajiuliza ni vipi Dini inafundisha utengano mkubwa kiasi hiki.
Niliishi na Mtazamo huu kwa mda wa miaka 24, nikimaanisha tangu nikiwa mdogo hadi nilipofika miaka 24.
Siku moja katika maongezi yangu na baba yangu tukazungumzia kidogo kuhusu dini, baba akaniambia tumeshakuwa na sasa tuna uhuru wa kuchagua njia yetu kama tubaki kuwa Wakristo ama waislam ama kuhasi dini, mimi sikusita kumjibu kuwa Kuanzia sasa sitaki dini yeyote, ila nitakuwa nikisali kwakua ninaamini Kuhusu Mungu Muumbaji, ninaamini katika Mungu wetu wa upatanifu na wa upendo..
Baba aliniambia niko sahihi kwa hilo kwakua ni maamuzi yangu, hakuniuliza kwanini nimeamua kuachana na dini, lakini siku moja baada ya kuja Marekani kusoma nilifanya tafiti za kidini zaidi, nilipata majibu mengi na hapo nilimtumia Baba email kumjulisha kwanini niliamua kuachana na dini.. Kwenye Email nikaandika sababu kuu ilikuwa ni kwamba Dini imekuja kuwa Ukuta mkubwa zaidi wa kutenganisha watu na siyo daraja la kuwaunganisha tena, haya niliyaona kupitia marafiki zangu wa hapa Marekani na wa Ulaya wanavyojiona wao (Wakristo) ni bora kuliko Waislam, nilichukia mtazamo wao na niliwasihi kuacha mitazamo yao ya utenganifu..
Nikaja nikatafiti kuhusu mauaji yaliyosababishwa na Dini tangu dini ya Paul, mnamo Karne ya kwanza kuna mauaji makubwa sana yalitokea Huko Korintho, Thesalonika, Roma (Ulaya) Galatia, Efeso na kwingine kwingi, hii ilikuwa ni kutetea dini, mauaji haya yalichukua miaka 235, mnamo karne ya tatu Wapagani walioanza vita na Paul walikuja na lengo la kuanzisha kanisa lao na kuondoa kanisa la Paul, wapagani hawa ni Catholic Church, hawa ni wapagani waliostaarabika, walipigana vita kubwa sana, watu walikufa wengi sana.
Vita kuhusu dini imeendelea kwa Karne na Karne, tumekuja miaka ya karibuni tumeona vita jinsi watu wanaojiita wa Itikadi kali wanavyouwa watu uko Afrika Mashariki Somalia huko, mashariki ya kati IS wanavyouwa watu, tutarudi kipindi cha Conspiracy ya September 11, 2001 jinsi Marekani ilivyotumia upenyo huo na kwenda kuharibu Mashariki ya Kati yote haya yamejificha katika Mwavuli wa Dini.
Kwa yale niliyojitafutia usahihi ni kwamba tangu kuumbwa kwa dunia watu waliokufa katika dini ndio wengi kuliko wale waliokufa katika magonjwa ya mlipuko, majanga ya asili, vita vya kikabila na kisiasa, watu waliokufa katika dini ni wengi na idadi yao haitakuja kuwa sawa hata kidogo na hao wengine niliotaja na wanaendelea kufa.
Sasa tujiulize hapa dini inaunganisha watu ama kuwatenga? inakuwa daraja ama ukuta?
Kibnafsi sipendi na sitashawishiwa kuunga dini mkono ila Kufanya yale ambayo Mungu wetu anatamani kuona sisi tunafanya..
Tuje katika mzozo wa sasa Papa Francis Kutetea suala la ushoga, tujiulize maoni ya Askofu mkuu wa Canterbury Justin Welby na Askofu mkuu wa Kanisa la Scotland Iain Greenshields juu ya ushoga, sasa hapa dini itakua inafundisha nini? Kibinafsi nimetokea kuichukia dini maana inataka kutumbukiza Dunia sehemu mbaya sana.