Nicholas J Clinton
JF-Expert Member
- Mar 13, 2014
- 877
- 486
Pamoja na vyama vya upinzani kugomea uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji chama cha Mapinduzi kimeamua kufanya uchaguzi huo ambao wao wanasema ni halali na kwa namna hiyo wameshinda uchaguzi kwa 99.9% Chini ya mbabe wa chama chao Rsis Magufuli.
Sisi ambao hatuamini katika itikadi ya chama cha Mapinduzi tumebaguliwa kwa kunyimwa haki yetu ya kushiriki uchaguzi huu ambao ni wa umma wa Tanzania. Pamoja na Serikali ya Rais Magufuli kuvifunga vyama vya upinzani mikono na miguu kwa miaka minne na kuwa nunua viongozi kadhaa wa upinzani lakini bado CCM imekimbia kufanya uchaguzi wa haki na huru.
Hii ni aibu kwa CCM kinachoimba wimbo wa kukubalika miongoni mwa Watanzania wengi ila kwa hili imekimbia kufanya uchaguzi wa haki na huru.
Baada ya CCM legelege ya awamu ya tano kufanya uhuni, uzwazwa, ujinga na umbumbumbu , upuuzi na ushenzi huo wote, Balozi za Marekani na Uingereza wamelaani vikali namna ya uchaguzi ulivyokiuka haki za msingi. Na nimesikia Waziri wa OR - TAMISEMI Ndugu Jafo kawajibu hao Mabeberu sijui kajibu nini? Katibu mkuu wa CCM Dr Bashir Ally yuko Zanzibar akitangaza ushindi wa kishindo wa CCM na anasema vyama vya upinzani vitakufa moja baada ya kingine huu ni utapiamlo wa akili au kifadulo cha fikira!
Hivyo basi, Chini ya Mbabe Rais Magufuli CCM wamefanya uchaguzi tutake tusitake hiyo imepita tusubili 2020! Sasa najiuliza ni kweli Upinzani na asasi nyingine za kiraia tumekubali hali hii iende hivi hivi? Najiuliza ni kweli hatuna cha kufanya ili kulinda Demokrasia japo kwa kidogo hiki? Ni kweli sisi Upinzani tumeamua kutoa matamko na vitisho kwa CCM bila kuchukua atua zaidi?
Ni kweli sisi tulio wengi tumeufyata hatuna ubavu wa kupambana na CCM? Je kweli tumeamua kuendeshwa na CCM mputamputa bila kuchukua hatua za kulinda uhuru wetu na Demokrasia? Vipi CCM wanatuanaje kwa sasa bada ya kuwaogopa na kufanya uchaguzi peke yao na kujitangaza washindi?
Na je tutaogopa mpaka lini kuulinda uhuru na Demokrasia? tangu hapo nyuma siyo kuwa tulikuwa na Demokrasia komavu hapana ila tumeshindwa kuilinda hata kwa hiki kidogo!
NINI TUFANYE SASA?
Ni wazi Rais Magufuli ni Mbabe by Personality hii ndiyo ulka yake tutake tusitake ndivyo alivyo tu, mimi nafikiri anaitaji kudhibitiwa mapema kabla ya kipindi chake cha pili kama atafanikiwa kuwa Mkuu wa Nchi kwa mara nyingine. Nasema tumdhibiti Rais Magufuli, nasema tena tumdhibiti Rais Magufuli kwa kibri chake cha uzima ni vigumu sasa kusikia malalamiko dhidi ya upinzani kwa serikali yake kadamizi kwa upinzani na vyombo vya habari.
Rais Magufuli hatasikia kabisa wala hasikii kabisa kaziba masikio hasikii na hii ni hatari kwa kiongozi hasiyependa kusilikiliza wengine hasa wapinzani wake zaidi ya kutaka kuwaangamiza wasiwepo kabisa. Kwa Hulka ya Rais wetu hapendi Upinzani kabisa.
Nafikiri haya yafanyike ili kulinda uhuru na Demokrasia Nchini
Mosi: Upinzani tuombe malidhiano na Serikali ya CCM, ili Uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji urudiwe na Umma upate haki ya kuchagua kwa uhuru viongozi wanaowataka kutoka vyama mbalimbli vya siasa.
Pili: Ni njia ya moto, jasho, machozi na damu kutaka mabadiliko ya lazima ya Tume huru ya uchaguzi Tanzania kabla ya uchaguzi wa 2020 kama tukishindwa hapa tujue 2020 wabunge wa upinzani watanyanganywa viti vyao au ushindi wao kwa nguvu. Hatuna chaguo zaidi ya kuchagua hili kama njia ya amani ikishindikana. Rais wetu hapendi Upinzani nasema tena hapendi upinzani na wala hasikii malalamiko yetu kabisa.
Tatu: Na hii ni muhimu sana kwa Watanzania wote jasho, machozi na misukosuko na kwa lazima CCM na serikali yake watake wasitake tudai katiba mpya ya Umma Wa Tanzania, Rais Magufuli ni mbabe hatakubali hili kutokea kwenye utawala wake kwa kisingizio cha kuleta maendeleo, lakini ni lazima Watanzania tumlazimishe Rais Magufuli kuendeleza mchakato wa katiba mpya, kwa sababu yupo hapo halipo kwa kuajiriwa na Watanzania.
Haya yote yanahitaji mshikamano Wa Vyama vya siasa, Asasi za kiraia, viongozi wa dini na vyombo vya habari. Tuache tabia ya kuwategemea Mataifa ya wazungu kuwawekea vikazwo vya kiuchumi Viongozi wetu pale wanapokiuka haki za msingi za binadamu, tunyanyuke kwa miguu yetu na kupigania haki zetu ambazo zinaminywa makusudi na viongozi walevi wa madaraka.
Taifa litajengwa na sisi sote bili ya mtu kuachwa nyuma lazima tuamue kusonga mbele na kukataa dhuruma kutoka kwa viongozi wetu wanaojitwika mwanvuli wa maendeleo kwa kuwakandamiza wengine.
Ni wakati tuchukue hatua hili kulinda uhuru na Demokrasia Nchini.
Imeandaliwa na Nicolas Jovine Clinton
Kaimu M/Kiti wa Vijana NCCR - MAGEUZI Taifa.
Dar Es Salaam
"PAMOJA TUTASHINDA"