Maoni ya Mnyika dhidi ya hotuba ya rais ya mwezi Juni

Ukisikia kudandia hoja ndio huko. Ulikuwa huna ubunifu wa kujuwa yote hayo mpaka umsikie Kikwete? hapo ndipo unapotudhihirishia kuwa wewe ni dhaifu wa hoja.

Uchukuwe hoja za mtu uzigeuzegeuze halafu uje humu na uende bungeni ukajidai hoja zako? Kijana naona umeishiwa kama Lema na Slaa.

Zomba (-a+e) = Zombe ni wale wale waliofunikwa kwa ghubighubi la kijani na njano. Ukipenda chongo huita kengeza. Mtabaki na chongo mkijua mna kengeza.
 
unaweza kuwa na hoja lakini si katika kila jambo,kukaa kimya usiwatetee watu au kukitetea kitu unachokiamini kwa kuogopa eti wananchi wataona umeside na madokta ni unafiki,na hii haiwezi kufanywa na mtu makini kama mnyika au any MP from cdm except shibuda.Naamini wananchi watataka hoja na si ni nani au nani anaside au hajaside na madokta au kundi lolote.............hakielimu eti?
True wananchi watataka kusikia hoja lakini si mradi hoja tu. Hapa watu sana sana kwa sasa hawataki tena kusikia maneno ya kisiasa watu wanataka kusikia huu mgomo unaisha vipi hili wapate matibabu yao serikali iliyowahidi itayadhamini.

Huo mgomo wa madaktari na vitendea kazi aikuwa malalamiko ya wananchi wanaopokea hizo huduma in the first place ni matakwa ya madokta. Wananchi kwa ujumla hapa hatasidhani wanaelewa ni vitu gani hasa vinavyohitajika ukitoa vitanda ambavyo wao wanajua havipo. Mpaka mwananchi aone kweli madaktari wanakesi inabidi um-convince aelewe ni nini hasa. Sasa basi ukikutana na jamaa ambae kazi yake ni propanganda ujue anaweza kukuamishia mpira maana kuna na madai ya kimaslahi makubwa tena. Kumbuka wengi katika jamii hawapati wala hata hawadhani kama watakuja lipwa hayo madai ya mishahara ya madokta.

Unless unakuja na kauli za kusema tungeweza hili kwa kufanya abc ndio unaweza kuingilia kati lakini we inakupa kuingilia kati kwa kupiga porojo tu. Si mwingine anaweza tumia maneno yako kuwambia wananchi unachochea wao kutopata matibabu. Narudi

Binafsi naona unajichanganya tu. Unataka kutuaminisha fikra zako kuwa ndo zinazotokea "kwingineko duniani" maana hata kama yanatokea haimaanishi kuwa ni sahihi, sababu umeielezea mwenyewe hapo pa zambarau.

Mnyika kaongea ulipo mzizi wa tatizo, UBABE na kutaka kuwaaminisha watu kuwa serikali IMEFANYA VYA KUTOSHA bila mjadala, kitu ambacho sio sahihi. Kwa nini wasiliachie bunge lijadili badala ya kutafuta huruma ya wananchi kama anavyofanya raisi kwenye hotuba zake!? kumbuka kuna kamati ilikua inafuatilia hili baada ya mgomo uliopita na hatujaona majibu yake na ni fedha za umma zilitumika hapo?!

Umesema hapo pa kijani, na hiyo ni wajibu wa kila mwananchi japo utekelezaji unafanywa na serikali iliyopo madarakani hivyo kuhoji utekelezaji sio ku'take sides'

Hakuna political suicide yeyote hapo, labda kama unaongea na wazee wa daresalama waliozoea ngonjera za JK, wengine wameamka na wanaelewa!

Mfa maji haishi kutapatapa. Wewe ndio uliyekurupuka. Wapinzani hawana akili iliyolala kama ninyi. Mbona hoja zao ndio mnazozifania kazi kila kukicha. Mmeishiwa, Rais wenu amelala usingizi wa kukororma, atakapoamka hayupo kwenye kiti cha enzi. Hilo la Madakatari litamtoa bila kutaraji. Anavaa kuficha kifua na tumbo, kichwa je?? avae bullet proof hadi kichwani! Aluta continua! mapambano bado yanaendelea. Hata Misri ilianza hivyohivyo na watu wachache. Wewe suburi timbwili lake. Ndugu zako utawatibu wewe Madaktari hawana mkataba na ndugu zako!
 
Wewe rudi Shule ukajifunze kuandika kwanza! Kama umtanzania na lugha yako ya Taifa inakuchanganya, je ya nje ya Tz itakua vipi ?
> Salafu = Sarafu
> Mishaara = Mishahara
> Kai aribu = Kaiharibu
Cha kushangaza wewe tena unamwita Mkuu wa nchi "dhaifu" unawaita na Member wenzako vilaza !
Wakati wewe hata Kiswahili kukiandika mtihani .
Viazi.
Usiparamie mijadala ikiwa hata kuandika issue !


Kuhusu lugha humu ndani ya mtandao huu ni tatizo kubwa. Tunashangaa sana wanavyojiita great thinkers.

Aidha kuhusu Mnyika,Bwana mdogo huyu alaisha poteza mvuto wake pale Dodoma wakati anachangia pale bungeni.
Amekuwa ni mtu wa kuheshimika sana kabla katika upande wa upizani kutokana na maneno yake yaliyopimwa vizuri
yakapimika. Lakini kwa sasa yeye na tundu Lissu hawana tofauti ndani ya CHAMA CHA DEMOKRASIA YA MATUSI.
 
N
Ukisikia kudandia hoja ndio huko. Ulikuwa huna ubunifu wa kujuwa yote hayo mpaka umsikie Kikwete? hapo ndipo unapotudhihirishia kuwa wewe ni dhaifu wa hoja.

Uchukuwe hoja za mtu uzigeuzegeuze halafu uje humu na uende bungeni ukajidai hoja zako? Kijana naona umeishiwa kama Lema na Slaa.
.
Kweli wewe Zomba hasa. Hujasikia Mnyika alishaandika barua kwa spika kutaja hoja ya madaktari ijadiliwe bungeni? au wewe ndio wale weny kuangalia wasione, kusikia wasielewe na wanapapasa wasiitambue? pili hoja hapa ni kujadili hotuba ya rais sasa ulitaka ajadili ya kichwa chake tena? wewe vipi? au ndiyo uliyetumwa kumpiga Dk nini? Mmeishiwa nyie akili za kuku. Ndogo Mnyika yule mbele maili 300m mbele ya kilaza jk
 
Unajua mapenzi yakizidi yanaaharibu?

Zanta,

You got me wrong.

Hapa hatuzungumziii mapenzi ya chumbani baali tunazungumzia siasa na mstakabali wa nchi yetu Tanzania. Kama wewe una mapenzi kwa Rais wako Kiwete is up to you. Mimi nimesoma speech ya Kiwete na nimesoma maoni ya Mnyika na kuyapima who is talking what.

Nakumbuka story moja kule Kenya miaka ya 90s. Kwamba Rais Moi kwa wakti ule alifanya ziara nchini USA akifuatana na viongozi waandamizi akiwemo Foreign Minister Marehemu Robert Ouko. Katika ziara hiyo ujumbe wa Moi ulifanya Press conference na kukawa na maswali toka kwa wanahabari. Kila swali likulizwa Moi alikuwa anajibu kwa kubabaisha na hivyo Foreign Minister Robert Ouko akawa anamsaidia Rais wake kujibu maswali mengi.

Baada ya press conference media zikaweka hadharani kwamba kwa namna Ouko alivyokuwa akijibu maswali NDIYE ALIPASWA AWE RAIS WA KENYA. Habari hizo zilitibua hali ya hewa ndani ya msafara wa Rais na wakti wa kurudi Ouko ilibidi aachwe nyuma na apande ndege ya peke yake! Alipofika airport alipokelewa na kiongozi mmoja aliyekuwa close na Moi Bwana Nicholous Biwott na aliposhuka tu kwenye ndege Biwott alimsalimia Ouko kwa dhihaka,''Good morning Mr. President.''

Hapo ndipo lilianza sekeseke la uhasama kati ya Moi na Ouko na hatimaye kuuawa kwa Robert Ouko na mwili wake kuchomwa moto!

Ninachotaka kusema ni kwamba hapa MNYIKA AMEONGEA NA KUONYESHA UMAKINI WA HALI YA JUU KIASI CHA KUWEZA KUWASHAWISHI WATU KUWA HUYU JAMAA NDIYE ALITAKIWA KUWA RAIS WA TANZANIA NA SIYO KIWETE!
 
Ninachotaka kusema ni kwamba hapa MNYIKA AMEONGEA NA KUONYESHA UMAKINI WA HALI YA JUU KIASI CHA KUWEZA KUWASHAWISHI WATU KUWA HUYU JAMAA NDIYE ALITAKIWA KUWA RAIS WA TANZANIA NA SIYO KIWETE!
Kwa mawazo yako lakini usitake kulazimisha kua kaongea kwa umakini wakati sie wengine tuanona hakuna jipya hapo alilosema
 
Umesomeka Kamanda Mnyika!

Niliisha wahi andika thread humu ndani kuhusu udhaifu wa mnyika nawashangaa humu jf members kumshadadia huyu dogo, jimboni ameshindwa na humu jf muda si mrefu atashindwa, dogo Yuko kisifa na kutafuta umaarufu zaidi
 
Kwa mawazo yako lakini usitake kulazimisha kua kaongea kwa umakini wakati sie wengine tuanona hakuna jipya hapo alilosema

Kama mapenzi yako yote yako kwa Magambas huwezi kuona jipya hata siku moja! Ndiyo maana hata CCM wakiongea pumba mijibunge na mifuasi ya magamba inashangilia tu.

Siku upinzani ukichukua madaraka ndipo utaona jipya linakuwaje.
 
Kama mapenzi yako yote yako kwa Magambas huwezi kuona jipya hata siku moja! Ndiyo maana hata CCM wakiongea pumba mijibunge na mifuasi ya magamba inashangilia tu.

Siku upinzani ukichukua madaraka ndipo utaona jipya linakuwaje.
Shida yaka ndio hii mtu asipokubaliana na hoja mnaleta ushabiki wa siasa. kwa mtazamo huu hamtafika kwa kweli. We ushaniona hapa nashabikia chama?
 
Mnyika naona unapimana ubavu na prezidenti wako....una mengi ya kufanya zaidi ya hicho unachong'ang'ana nacho, busara Fanya kazi zako za kibunge zaidi kwani 2015 haipo mbali na jimboni kuna mambo kibao hujayafanya. Mwenzako Jk ANAONDOKA zake Hvyo hana kugombea tena.
 
Eti serikali itoe maelezo kwa nini Rais hakuhutubia tarehe 30 june.yaani nilipofika hapo tu nimeamini HUYU MVULANA ANA AKILI FINYU SANA.
Hivi mnyika ni nani hadi utake kumpangia bosi wa nchi hii lini ahutubie?
We kijana huna nyimbo.ndo maana hata bungeni unahangaika kama kuku anayetaka kutaga.YOU SO FULL OF NOSENSE.HIVI WANAUBUNGO WALIKUCHAGUA ILI UWE UNATULETEA PUMBA ZAKO HAPA.
Sasa deal lenu la kuvuruga nchi limegonga mwamba.NCHI HAITATAWALIKA HUMU JF kwingine LIFE GOOSE ON.[/QUOTE

miaka 50 ya uhuru tuna watu kama hawa

hata mimi na shangaa miaka 50 ya uhuru tuna watu kama wewe ambao hawajui kinacho endelea nchini!

Jk nchi imemshinda mwenyewe na ana ivuruga mwenyewe kwa udhaifu wake.
Mnyika ana haki ya kuhoji kama wewe ulivyo na haki ya kuuliza mnyika ni nani( Mnyika ni muwakilishi wa wananchi)

kweli wewe umeshindwa kufikiri ni watanzania wangapi wenye huwezo wa kutumia internet mpaka hotuba ina sambazwa kwenye blog?

Lazima ukubali kuwa kurugenzi ya rais ni dhaifu kama yeye mwenyewe!

Mnyika ana msaidia rais kujirekebisha lakini hasikii!

Mwana nyinyiemu mwenzio alileta thread jana ya kutaka kurugenzi yenu iwajibike kwa kilichotokea, kwa hiyo na huyo mwenzio unampinga?

Pole sana kwa udhaifu wa mwenyekiti wako wa chama
 
Na Lingine kama kweli serikali haina hela kwanini isitangaze kupunguza mishara na malupulupu yote kwa asilimia hata ishirini tu kwa viongozi wote hasa wa kisiasa? kama yupo anayelipwa sh 18 miliion kwanini ishindikane kwa madaktari? Hata katika familia kama baba unalia hali kwamba hela hamna na ukashiriki kula kiporo asubuhi na kula dona kwa Maharage, watoto watakuelewa tu. Lakini kama unawambia watoto hela hamna na unarudi usiku umelewa baada ya kula sijui wapi huko watoto hawatakulewa. Au watoto wanadai daftari za kwendea shule unasema hela hamna lakini unazidi kushona suti tu hutaeleweka hata kidogo. Kwa hiyo kama serikali kweli inaamnini haina hela(siamini) ya kuwalipa madaktari na walimu haki zao itangaze wote wenye mishahara zaidi ya 3.5m wapunguzwe!
 
JK anasema amepandisha posho mpaka 25,000 kwa madaktari bingwa na 15,000 kwa madaktari wanaojifunza kwa vitendo mbona hajasema huko serikalini wanalipana posho kiasi gani kwa maafisa wao wakati wa kuandaa bajeti, safari, vikao, semina na makongamano?? anaejua wanavyolipana posho atuwekee hapa tulinganishe tafadhali.
 
MAONI YA MBUNGE WA UBUNGO KUHUSU HOTUBA YA MH. DKT. JAKAYA KIKWETE RAIS WA TANZANIA KWA WANANCHI TAREHE 30 JUNI 2012





Leo tarehe 1 Julai 2012 kumesambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari hotuba ya Mh. Dkt. Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi inayotajwa kutolewa tarehe 30 Juni 2012.

Kufuatia hotuba hiyo na kufuatia mwito kutoka wachangiaji wa mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kutaka maoni yangu kuhusu hotuba husika, naomba nichukue fursa hii kutoa maoni kwa nafasi yangu ya ubunge kuhusu hotuba tajwa kama ifuatavyo:

Hotuba hiyo ya Rais imeibua mjadala na masuala ambayo yanahitaji kujadiliwa bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge unaoendelea hivyo, serikali isiendelee tena kutumia kisingizio cha mahakama kulizua bunge kujadili masuala husika wakati yenyewe inayajadili na kuyatolea maelezo na maelekezo pamoja na kuchukua hatua hususani kuhusu suala la mgomo wa madaktari.

Hotuba hiyo ya Rais ukindoa suala la usafirishaji haramu wa watu nchini inaelekea kuwa ndiyo kauli ya Serikali ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kwamba ingetolewa bungeni lakini baadaye serikali ikasema haitatoa kauli. Uamuzi wa Serikali kuitoa kauli hiyo kupitia hotuba ya Rais una mwelekeo wa kukwepa wabunge wasijadili hotuba husika na pia wasitimize wajibu wa kikatiba wa ibara 63 (2) wa kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.

Hivyo, Ofisi ya Rais na Ikulu wanapaswa kutoa maelezo kwa umma sababu za Rais kutolihutubia taifa tarehe 30 Juni 2012 kama ilivyotangazwa katika baadhi ya vyombo vya habari vya kielectroniki na badala yake hotuba ya Rais kusambazwa tarehe 1 Julai 2012 kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari na iwapo masuala ya hotuba hiyo kuhusu mgomo wa madaktari ndiyo yale ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikusudia kuyaeleza bungeni.

Aidha, kwa kuwa bunge litajadili mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kuanzia kesho tarehe 2 Julai 2012 na kuendelea ni muhimu wabunge wakajadili pia masuala ambayo Rais ameyaeleza kwa taifa na kutimiza wajibu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 63 (2) wa kuishauri na kuisimamia serikali.

Kuhusu Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini
Ni vizuri hotuba ya Rais imeeleza wazi kwamba tukio la Chitego, Dodoma la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea hapa Tanzania kwa kuwa kwa kipindi cha miaka kumi kumekuwa na ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu katika taifa letu kupitia mipaka ya mikoa mbalimbali hapa nchini. Kwa mbinu yoyote ile ambayo imetumika, matukio haya yanaashiria kwamba mipaka yetu haipo salama kwa kuwa kama malori na vyombo vingine vya usafiri vyenye watu wasio na hati za kuingilia nchini wanaweza kuingia kwa wingi kwa nyakati mbalimbali tafsiri yake ni kwamba nchi iko kwenye hatari ya kuingiziwa pia vitu vingine haramu ikiwemo madawa ya kulevya na silaha hali ambayo ni tishio kwa usalama wa nchi na maisha ya wananchi. Ni vizuri Rais amekutana tarehe 27 Juni 2012 na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzungumzia tukio hilo; hata hivyo, zaidi ya kuwapongeza vyombo vya dola kwa kazi nzuri ya kudhibiti shughuli za biashara haramu, nilitarajia kwamba Rais kwa mujibu wa mamlaka yake ya ibara ya 33 (2) ya mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu angeagiza uchunguzi ufanyike kuhusu udhaifu uliojitokeza na kuagiza hatua kuchukuliwa kwa walishindwa kudhibiti hali hiyo katika mipaka ambayo biashara haramu ya usafirishaji wa watu inapitia. Izingatiwe kwamba mianya hii katika mipaka yetu ina athari pana sio katika suala hili tu bali pia katika usalama wa maisha ya wananchi kama ilivyo katika mikoa ya Kigoma, Kagera na kwingineko ambapo uhai wa wananchi na mali zao uko mashakani kutokana na uvamizi toka kwa wahamiaji haramu. Aidha, athari za hali hiyo zimejitokeza katika usambazaji wa chakula toka kwenye hifadhi ya taifa ambapo pamoja na Serikali kutumia zaidi ya bilioni 27 kusambaza mahindi na nafaka nyinginezo bei za bidhaa hizo katika Soko la Dar es salaam ikiwemo katika Jimbo la Ubungo hazikushuka kutokana na vyakula hivyo kutoroshwa na kuuzwa nje ya nchi kutokana na udhaifu katika ulinzi kwenye mipaka.

Hivyo, ni muhimu wabunge wakati wa mjadala wa bajeti ya ofisi ya Rais wataka kuongezeka kwa uwajibikaji na usimamizi wa utawala wa sheria ili kudumisha amani nchini.

Hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa ni pamoja na bunge kuisimamia serikali kuhakikisha idara ya usalama wa taifa inafanya kazi kwa ufanisi zaidi katika kuvisaidia vyombo vingine vya dola kulinda mipaka ya nchi na pia matatizo ya maslahi katika vyombo vya ulinzi na usalama yanatatuliwa ili vyombo husika viweze kufanya kazi bila baadhi ya maofisa wake kujihusisha na vitendo vya ufisadi na kuruhusu biashara haramu za aina mbalimbali.

Kuhusu Mgomo wa Madaktari

Kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa; hotuba ya Rais imeendeleza kauli za upande mmoja ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kuhusu mgogoro huo bila taifa kupewa fursa ya kupata maelezo na vielezo vya upande wa pili; hivyo kuwa serikali imetoa kauli yake hadharani badala ya bungeni au mahakamani, ni muhimu pia taarifa ya kamati ya bunge ya huduma za jamii iliyoshughulia suala hilo na kukutana na pande zote mbili itoe taarifa yake bungeni na kwa umma.

Katika hotuba yake Rais amewaeleza kwa kiwango kikubwa wananchi namna ambavyo madaktari wanasababisha mahangaiko kwa wagonjwa wengi na kusababisha vifo kwa wengine lakini hakueleza kabisa mchango wa serikali katika kusababisha hali hiyo. Hivyo, kwa kuwa pande zote mbili zinachangia katika athari zinazoikumba nchi na wananchi kutokana na mgomo; ni muhimu chombo cha tatu kikaingilia kati kuwezesha ufumbuzi kupatikana na chombo hicho ni bunge ambalo ndilo lenye wajibu wa kuisimamia serikali. Jitihada za kuwalazimisha madaktari kurejea kazini bila majadiliano ya pande mbili mbele ya chombo cha kuisimamia serikali kushughulikia chanzo cha mgogoro huo zinaweza kuleta ufumbuzi wa muda mfupi na athari za muda mrefu.

Ieleweke kwamba hata madaktari wakisitisha mgomo wa wazi kutokana na amri ya mahakama na agizo la Rais, migogoro katika ya serikali na watumishi wa umma wenye kusababisha migomo baridi ya chinichini ina madhara ya muda mrefu kwa taifa.

Mathalani, kutokana na migomo baridi na huduma mbovu katika sekta ya afya wananchi wa kawaida wamekuwa wakifa kutokana na magonjwa yanayotibika.

Migomo ya chini kwa chini ya walimu na mazingira mabovu yamekuwa yakisababisha kudidimia kwa elimu katika shule za umma; mwanafunzi aliyehitimu masomo yake bila kujua kusoma na kuandika hana tofauti na mgonjwa anayekufa kwa kukosa huduma.

Hali hii ya kugoma kusiko kwa wazi imeenza kujipenyeza mpaka kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuachia mianya ufisadi na kushindwa kusimamia utawala wa sheria kama ivyodhihirika kwa kuongezeka kwa vitendo vya biashara haramu katika taifa letu.

Rais amewaeleza wananchi kuwa kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari na kwamba katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari yalizungumzwa na pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba. Hata hivyo, katika masuala matano yaliyobaki, Rais hakueleza kwa wananchi nini ambacho serikali ilikuwa tayari kutoa kwa kila madai na kwa kiasi gani badala yake ameonyesha tu kwa ujumla kwamba madai hayo hayatekelezi.

Aidha, kufuatia hotuba hii ya Rais Madaktari nao wana wajibu wa kuueleza umma msingi wa madai yao na kwa kiwango gani walikuwa tayari kushuka kutoka katika madai yao ya awali, kinyume na hayo itaonekana kwamba madaktari waliingia katika majadiliano wakiwa na msimamo wa kutaka madai yao pekee ndiyo yakubaliwe wakati ufumbuzi wa mgogoro wa pande mbili hupatikana kwa win win (give and take).

Ni vizuri ikafahamika kwamba katika majadiliano, pande zote mbili huwa na mapendekezo yake; hivyo upo uwezekano kwamba yapo madai ambayo madaktari wameyatoa ambayo serikali haina uwezo wa kuyatimiza kwa kiwango walivyopendekeza na yapo ambayo serikali imeyakataa wakati ambao ina uwezo wa kuyatekeleza hata ikiwa kwa kiwango pungufu ya kile kilichopendekezwa na madaktari.

Suluhu katika mgogoro kama huo ambao kila upande una mapendekezo yake linapaswa kufanywa na vyombo vya usuluhishi; hata hivyo kuwa suala hili linahusu mgawanyo wa rasilimali za nchi na bajeti ya serikali, chombo chenye mamlaka ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi ni bunge.

Na kwa kuwa kamati ya bunge ya huduma za jamii ilikutana na pande mbili, ilikuwa muhimu kwa serikali kabla ya kupeleka shauri mahakamani kurejesha kwamba suala husika bungeni ambalo ndilo lenye wajibu wa kupendekeza vipaumbele vya mpango wa serikali na ndilo lenye kuidhinisha bajeti ya matumizi ya serikali.

Uamuzi wa serikali kukimbilia mahakamani kabla ya majadiliano ya bunge umechangia katika kusababisha mgomo wa madaktari, hivyo ushauri wangu kwa Rais Kikwete ni kwa serikali kufuta kesi iliyoko mahakamani ili bunge lipewe fursa ya kujadili ripoti yake kamati yake na kupitisha maazimio ya kuwezesha suluhu kati ya serikali na madaktari.

Mahakama iwe ni hatua ya mwisho baada ya mihimili miwili muhimu ya serikali na bunge kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro unaoendelea wenye athari kwa nchi na maisha ya wananchi.

Rais Kikwete ameeleza taifa kwamba Serikali imeongeza sana bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka 2011/12; hata hivyo serikali inapaswa pia kulieleza taifa namna ambavyo kiwango hicho cha fedha kinapungua ukiweka kizio (factor) cha kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumumo wa bei ukilinganisha mwaka 2005 na 2012.

Ukweli ni kwamba bajeti ya Sekta ya Afya bado ni ndogo kwa kuwa serikali haijatimiza bado azimio la kutenga asilimia 15 kwa ajili ya bajeti ya afya pia, hata kiwango hicho cha ongezeko la fedha hakijaleta matokeo ya kutosha kutokana na matumizi kuelekezwa kwenye baadhi ya maeneo yasiyokuwa ya kipaumbele na kuwa na utegemezi wa kiwango kikubwa cha fedha za wahisani ambazo kwa mwaka huo wa 2011/2012 aliourejea Rais Kikwete hakikutolewa kwa kiwango kilichoahidiwa. Hivyo, Rais Kikwete awezeshe kuongezwa kwa fedha za ndani kwenye bajeti ya afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Katika madai mengine Rais Kikwete ameeleza kwamba pande mbili zilifikia makubaliano nusu nusu, hali ambayo inaashiria kwamba madaktari wana hoja ambazo zinahitaji majadiliano hivyo, ni muhimu bunge likapewa nafasi ya kujadili kuweza kuwakilisha pande zote mbili za serikali na madaktari kuhusu nini kinawezekana na nini hakiwezekani ili kulinusuru taifa na mgogoro unaoendelea.

Rais Kikwete ametumia kwa kiwango kikubwa madai ya madaktari ya ongezeko la mshahara kujaribu kuwachonganisha wananchi na madaktari kwa kuwa na madai yasiyotekelezeka. Hata hivyo, ni muhimu ikafahamika kwamba sio madaktari pekee ambao wana mgogoro na mwajiri wao yaani serikali kuhusu kiwango cha mshahara bali pia watumishi wengine wa umma ikiwemo walimu.

Nyongeza iliyotolewa na serikali ya kati ya asilimia 15 na 20 kwenye mwaka wa fedha 2012/2013 ni tofauti na ahadi ambazo serikali imekuwa ikitoa kwa wafanyakazi za kuongeza mishahara na kupunguza kodi katika mishahara. Rais Kikwete na serikali warejee maoni na mapendekezo ya kambi rasmi ya upinzani kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na 2012/2013 kuhusu nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma na vyanzo mbadala vya mapato vya kuongeza kwa ajili ya kuwa na uwezo wa kutimiza mahitaji. Uwiano wa sasa wa matumizi ya mishahara kuwa asilimia 48 ya bajeti badala ya uwiano mzuri wa asilimia 35 kuwa mishahara na na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa; ni matokeo ya udhaifu wa serikali katika kupanua vyanzo vya mapato, kupunguza matumizi ya kawaida yasiyo ya lazima na kuongeza fedha katika miradi ya maendeleo hali ambayo Rais Kikwete kuliwezesha bunge kuisimamia serikali na kuirekebisha.


Kuhusu Suala la Dkt. Steven Ulimboka

Rais Kikwete ameeleza wananchi kuwa ameelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane; hata hivyo kauli hii inaashiria kukubaliana na hatua iliyochukuliwa na jeshi la polisi kuunda jopo la kuchunguza.

Nilitarajia Rais Kikwete kwa kutambua uwepo wa madai ya polisi kutuhumiwa kuhusika katika jaribio la mauji ya Dr Ulimboka angetangaza kuunda tume huru ya uchunguzi au walau angeongeza nguvu katika jopo la uchunguzi lililoundwa kwa kuunda timu ya maafisa waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama na usalama pamoja na wadau wengine kutoka taasisi huru.

Rais Kikwete anapaswa kutumia madaraka yake kwa mujibu wa katiba kuunda tume huru ambayo inadhihirisha kwa vitendo kwamba watuhumiwa hawajichunguzi wenyewe na kuwezesha matokeo ya uchunguzi kuaminika.

Narudia kuwasihi madaktari kuendelea kuokoa maisha ya wananchi katika kipindi hiki kigumu lakini wakati huo huo Rais Kikwete aiongoze serikali kuepusha athari zaidi katika sekta ya afya ya kuwa na mgogoro na madaktari kwa kuliwezesha bunge kujadili suala hili na kulipatia ufumbuzi ikiwemo kupitia nyongeza ya bajeti ya Wizara ya Afya. Nimemwandikia barua Spika Anna Makinda akiwa ni mkuu bunge kama muhimili mmojawapo wa dola kuweza kuchukua hatua stahili, naomba pande zote zizingatie maoni yanayotolewa na wabunge kwa niaba ya wananchi kwa maslahi ya taifa.

Maoni haya yametolewa leo tarehe 1 Julai 2012 na:

John Mnyika (Mb)
Bungeni-Dodoma

COPIED FROM JOHN MNYIKA: MAONI YA MBUNGE WA UBUNGO KUHUSU HOTUBA YA MH. DKT. JAKAYA KIKWETE RAIS WA TANZANIA KWA WANANCHI TAREHE 30 JUNI 2012

MT TAKE:
Kweli ukitaka kupiga piga panapo huma zaidi,
Dogo amegundua dhaifu ni dhaifu, basi anaendelea kuonyesha udhaifu wa dhaifu kwa kuonyesha madhaifu ya dhaifu.




Kwa ujula maoni ya mh. Mnyika kuhusiana na hotuba ya Raisi yana mambo mazuri yanayopaswa kuzingatiwa. Mwishoni mwa maoni yake anawasihi madaktari kurudi kazini na kutoa changamoto kwa serikali kutafuta suluhu ya kudumu ya matatizo yao ili kuepusha vifo vya wananchi. Katika sehemu nyingine ya maoni yake anatoa changamoto kwa chama cha madaktari kuweka wazi kwa wananchi wako tayari kupokei kipi kidogo kuliko walichoomba ili kama kanuni za usuluhishi patanishi zitafuatwa aliyepata apate nusu na kukosa nusu na kinyume chake. Amefafanua zaidi kwamba kama madaktari hawatakuwa tayari kupata nusu na kupoteza nusu watakuwa wanaweka maslahi yao kama ndio sharti la suluhu.

Kwamba Serikali haikupaswa kupeleka suala mahakamani kabla kamati ya Bunge haijatoa taarifa au ushauri wake kuhusiana na mgogoro yangeweza kuwa maoni muafaka kama madaktari wangekuwa tayari kukaa kimya kusubiri maoni au ushauri wa kamati ya Bunge. Bahati mbaya madaktari wetu wamekuwa na haraka sana kuhakikisha madai yao yanatekelezwa mara moja. Ndio maana walilazimisha kuwepo mgomo wenye athari kubwa katika maisha ya watu bila kujali kuwepo amri ya Mahakama Kuu ya kusitisha mgomo. Kwa utaratibu wa sheria zetu, panapokuwepo na mgogoro wa kisheria kati ya pande mbili mwenye dhamana na mamlaka kisheria ya kusuluhisha mgogoro huo ni Mahakama. Bunge halijapewa madaraka ya kutatua migogoro ya kisheria kati ya pande mbili. Lina mamlaka tu kama ulivyosema kwa usahihi mheshimiwa ya kuisimamia Serikali yenyewe lakini sio watumishi wa Serikali, kama madaktari. Chombo pekee chenye mamlaka juu ya Serikali na Bunge pamoja na watumishi wa umma kuhusiana na utatuzi wa migogoro niMahakama.


Kwamba mgogoro ulipaswa kupelekwa katika chombo cha usuluhishi ndivyo ilivyokuwa maana mgogoro ulikuwa mikononi mwa Kamati ya Usuluhishi na Uamuzi na iliposhindikana ilipelekwa Mahakama Kuu.
Suala la kuundwa kwa Tume huru kuchunguza mateso aliyofanyiwa daktari Ulimboka badala ya polisi ambao ni watuhumiwa linaweza kuwa na msingi kama polisi nao ni watuhumiwa.
 
Dingiswayo alifanya kazi nzuri sana jana. Jk anahutubia, huku mi nasoma kwenye mtandao Jf.
Sijui nani anamtengenezea hotuba feki namna ile, inawezekana ndiye anayempeleka Jk na ccm yake kwenye friji then kwenye coffin.
 
Last edited by a moderator:
JK anasema amepandisha posho mpaka 25,000 kwa madaktari bingwa na 15,000 kwa madaktari wanaojifunza kwa vitendo mbona hajasema huko serikalini wanalipana posho kiasi gani kwa maafisa wao wakati wa kuandaa bajeti, safari, vikao, semina na makongamano?? anaejua wanavyolipana posho atuwekee hapa tulinganishe tafadhali.

Mfano tu Wabunge! Mbunge kama Maji Marefu elimu yake darasa la nne anapokea posho 200,000 kwa siku!
 
Upinzani ktk siasa si kupinga kila kitakachotolewa na wengine,sina hakika kama mambo yote yanaweza kuwa mabaya siku zote...hivi ni wazi kuwa kila litakalotamkwa na serikali au chama tawala kina walakini??na hivi ni sahihi kuamini kuwa kila kitakachosemmwa na mtu wa upinzani hasa wa CDM ndiyo sahihi??nani kasema kuwa CDM ndio framework sahihi ndani ya nchi hii??
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom