WAKO WAPI WATU WAKO
JF-Expert Member
- Sep 26, 2017
- 2,359
- 3,115
Samatta afai kuwa Nahodha wa Stars,, apewe MTU mwenye kaliba ya uongozi uwanjani na kuwatia wachezaji wenzake hamasa.... Ili apigiwe kelele ajitume..Samatta hana la kupoteza ndio maana akija timu ya Taifa hajitumi anacheza hovyo tu kuogopa majeruhi.
Kuna mechi Taifa Stars walishinda bila yeye asituletee u-star wake, mtu ligi kubwa anafunga magoli, UEFA hadi Liverpool anafunga ila mechi ya timu ya Taifa anafunga penati tu, hata nusu ya Msuva hafikii hiyo namba 10 apewe hata hajibu.
Yupo Kaseja, Nyoni, Yondani kwa sasa wanaweza kazi ya uongozi ndani ya uwanja..
Ila nakubali pia Sammatta ni Mzigo kwa timu huu ndio ukweli...
Ana kiwango cha kawaida mno, sema anabebwa na mafanikio yake tu....aliyobahatika kuyapata.