Nani kumrithi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mwamunyange?

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,271
29,879
Rais John Magufuli alimuwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu January 30 Mwaka jana baada ya kutimiza umri kwa mujibu wa katiba na sheria.

Jenerali Mwamunyange alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini pamoja na Meja Jenerali wawili ambapo wote kwa pamoja walistaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

Sababu iliyomfanya Mamunyange Aongezewe Mwaka 1

Rais na Amri Jeshi mkuu waliamua kumbakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia tarehe 30 Januari, 2016 hadi tarehe 31 Januari 2017,”

Jeneral Mwamunyage alisema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea muda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo.

Je, Rais ameshampata mtu sahihi wa kuvivaa viatu vya Mkuu wa Majeshi ambaye muda wake unakaribia kuisha mwishoni mwa Januari 2017?

Je, ni nani aliyeandaliwa kuwa Mkuu wa Majeshi baada ya Mwamunyange?

Nawasilisha wadau.
 
Atateuliwa "Kaimu mkuu wa majeshi" kwanza
Nami nilifikiria kuwa asije akaweka mambo yake ya ajabu Kaimu Mkuu wa Majeshi!! Nadhani sasa ameshapata mtu wa kumrithi! Lazima awe wa kanda maarumu ingawa kw geshi huwa hawapendi hayo mambo ya undugu!!! Atafute miongoni kw Maj Gen ateue hapo.....either Land Force au Airforce au Navy!! Huyu aliepo ni Land Force lakini intelligence ndio anamaliza muda wake........au hata yule wa JKT naona amekimbizwa mbio mbio sanaaa
 
Rais John Magufuli alimuwongeza muda wa mwaka mmoja Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu January 30 Mwaka jana baada ya kutimiza umri kwa mujibu wa katiba na sheria.

Jenerali Mwamunyange alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi la ulinzi nchini pamoja na Meja Jenerali wawili ambapo wote kwa pamoja walistaafu ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo.

Sababu iliyomfanya Mamunyange Aongezewe Mwaka 1

Rais na Amri Jeshi mkuu waliamua kumbakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia tarehe 30 Januari, 2016 hadi tarehe 31 Januari 2017,”

Jeneral Mwamunyage alisema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea muda huo imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo.

Je, Rais ameshampata mtu sahihi wa kuvivaa viatu vya Mkuu wa Majeshi ambaye muda wake unakaribia kuisha mwishoni mwa Januari 2017?

Je, ni nani aliyeandaliwa kuwa Mkuu wa Majeshi baada ya Mwamunyange?

Nawasilisha wadau.

ampandishe kamanda Sirro.
 
Back
Top Bottom