Maoni Kuhusu Muswada Mpya PSSSF Hifadhi ya Jamii

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Awali ya yote natangaza nina maslahi na hifadhi ya jamii. Pili, mimi siyo mwanasheria. Kwa hiyo inawezekana nimeelewa isivyo. Na, tatu: haya ni maoni binafsi yenye lengo la kuboresha nia njema ya taifa kuwa na hifadhi ya jamii iliyo maridhawa.

Maoni haya yamegawanyika katika sehemu kuu mbili: maoni ya jumla, na, maoni mahususi.

A. Maoni ya Ujumla
(nyongeza 1):
*
7. Objectives of the Fund shall be to:
(a) ensure that every person who is an employee in the Public Service receives his retirement pension benefits as and when due;
(b) assist improvident individuals by ensuring that they save in order to cater for their livelihood during old age; and
(c) establish a uniform set of rules, regulations and standards for the administration and payments of retirement pension benefits for the Public Service.

*

Malengo ya mfuko yaliyoandikwa yanasigana vipengele vya muswada.

Kifalsafa, serikali ijitoe kwenye biashara ya hifadhi ya jamii. Kazi hiyo ibakie kwenye soko huria na maamuzi ya mtu binafsi. Kwa muswada huu itakuwa inajibebesha mzigo mzito itakayopata changamoto kuumudu na kusababisha watumishi wengi kutumbukia nyongo serikali yao inayowajali. Suala la pensheni lingeachwa liwe la mtu binafsi. Hata kama mifuko iliyoko ni mingi, na serikali ingependa ibakie mifuko miwili tu, basi hiyo mifuko iachwe ijiunge yenyewe kwa kufuata sheria zilizoko.

Muswada huu ni kama unabagua watumishi wa umma kwa mafungu mawili makuu: viongozi waandamizi na wananchi wa kawaida. Jambo hili linaweza kuleta athari mbaya sana pale wananchi wa kawaida watakapobaini kwamba michango yao inatumika kutoa mafao manono kwa viongozi waandamizi lakini wao hawana mafao yanayofanana na ya viongozi waandamizi. Kwa vile viongozi waandamizi wana mishahara mikubwa kuliko wasio viongozi, basi tofauti ibakie kwenye ukubwa wa mafao, na si masharti ya mafao. Marupurupu mengine ya viongozi waandamizi yatoke kwenye vyanzo vingine vya mapato, na siyo michango ya wanachama.

Kwa muswada huu ulivyo, serikali inakuwa ni kama imekwepa kulipa mafao watumishi waliyostahili na kukubaliana kwa mujibu wa sheria zilizoko. Wengine wanaweza kudai serikali imeshindwa kulipa na kulazimika kuacha kulipa ( _to default_ ).

Katika awamu za pili na tatu za uongozi Tanzania, serikali ilifanya jitihada nyingi kugatuka kutoka kwenye mambo mbalimbali. Moja ya mambo hayo ilikuwa ni masuala ya pensheni. Mifuko ya hifadhi ya jamii, japo kinadharia, ilikuwa ni sehemu tafauti na serikali. Muswada huu unarudisha hali ilivyokuwa miongo kadhaa iliyopita kwamba serikali ndio inatoa mafao. Yaani, kwa muswada huu serikali inarudi kulekule kwenye uchumi uliopangwa (" _central planning of economy_ ") kwenye masuala ya pensheni, uchumi ambao ulionwa una changamoto nyingi.

Moja ya madhara makubwa sana ya muswada huu itakuwa ni kukatisha tamaa watumishi. Angalau mategemeo ya kupata pensheni, na imani kwamba pensheni itakuwapo wakati mtu anastaafu, ni miongoni mwa vitu vinavyoleta matumaini kwa baadhi ya watumishi. Ukiondoa tumaini hilo, hali halisi haiwi ya kuvutia.


B. Maoni mahususi.

Muswada toleo la 19 Oktoba 2017 wahusika.

Nadhani baadhi ya vilivyomo kwenye muswada huo ni kama inavyoorodheshwa hapa chini. Nimeongeza maoni kwenye baadhi ya orodha ya vilivyomo.


1. Wanatumishi wa umma walioko NSSF kuhamishiwa PSSSF. Hao watumishi walioko wangeachwa hukohuko NSSF. Mfuko wa PSSSF uanze na wanachama wapya na wale wa mifuko iliyounganishwa.

2. Mfuko wa PSSSF utakuwa tu sawa na serikali: hauwezi kushitakiwa bila kufuata mlolongo maalum wa kisheria. Mfuko wa PSSSF usiwe kama serikali bali uwe chombo huru.

3. Michango ya mwanachama na mwajiri itakuwa ni mali ya mfuko wa PSSSF. Hili lingebadilishwa. Michango ya mwanachama na ya mwajiri iwe ni mali ya mwanachama.

4. Pesa yoyote kwenye akaunti ya mwanachama itatolewa kwa idhini ya bodi ya PSSSF. Mwanachama akitoa kiasi chochote hatahesabiwa tena kuwa mwanachama. Iwe ni pale mwanachama anapotoa kiasi chote.

5. Jinsia haijazingatiwa. Akifa mwanachama mwanamume watoto wanapata mafao. Akifa mwanamke hawapati. Sheria inatakiwa kutobagua kijinsia.

6. Mfuko wa pensheni unatengeneza madaraja. Wale wenye vyeo vikubwa wana mafao yenye masharti tofauti na watumishi wengine wa umma. Ikiwa wote ni wanachama kusiwe na tofauti ya masharti ya mafao miongoni mwa wanachama.

7. Mwanachama hatapewa mafao ya aina zaidi ya moja kwa wakati mmoja hata kama anastahili. Bodi ya PSSSF itamuuliza mwanachama achague fao moja au bodi itamchagulia. Hii haiko vizuri sana. Mwanachama apewe mafao yote anayostahili kupata.

8. Mwanachama akifungwa jela, hana maamuzi kabisa na namna gani mafao yake yatumike. Bodi ya PSSSF inaweza kuamua kumpa mtu yeyote pesa alizostahili mfungwa huyo. Hata ikitokea mfungwa huyo amesamehewa, hatorejeshewa pesa zilizotumika akiwa mfungwa.

9. Mwanachama anaweza kumuomba Mhe. Rais amsamehe kutumika vigezo na masharti ya lsheria hii. Yaani inaeleweka toka awali kwamba vigezo vilivyoko vitaumiza hadi kulazimu wengine kukimbilia kwa Rais.

10. Mwanachama kimsingi hawezi kutumia mafao yake kama dhamana ya mkopo au madai yoyote mengine au kuyahamisha mafao hayo nje ya mfuko. Akidaiwa na serikali, au amri ya mahakama kuhusu mkopo wa nyumba, labda.

11. Bodi ya PSSSF itakuwa ni kama vile inatunza pesa za wanachama. Bodi hiyo itakuwa huru kutumia pesa hizo inavyotaka ikizingatia mahitaji ya sheria hii.

12. Mfuko utapanga bajeti ya mwaka. Malipo yoyote yatahitajika kuwemo kwenye bajeti, hata kama ni mafao ya wanachama. Mfuko wenyewe utakuwa unaruhusiwa kutumia hadi 15% ya mapato. Mafao ya wanachama yatakuwa ni moja tu ya matumizi kwenye bajeti ya mfuko.

13. Bodi ya mfuko haitakuwa na mamlaka ya mwisho kwenye bajeti. Mamlaka hayo ni ya Mhe. Waziri.

14. Mfuko utakuwa kama vile serikali: huwezi kuishitaki bila kuipa taarifa miezi mitatu kabla.

15. Kanuni za kukokotoa mafao zilizopo hazitatumika. Badala yake mwanachama aliyekuwako kwenye mfuko mwingine, mafao yake yatakokotolewa kwa mujibu wa sheria hii.

16. Mwanachama akiacha kazi utumishi wa umma na kwenda sekta binafsi atahamisha uanachama wake kwenda NSSF. Michango yake ya PSSSF itabaki PSSSF. Miongozo inayoongoza namna ya kujumlisha mafao itafuatwa.

17. Wanachama watahamishwa toka mifuko walioko kwenda mifuko mingine kutegemea ni wapi walikoajiriwa. Hata wale wanaochukua mafao ya pensheni sasa, nao pia watahamishwa kutegemea ni wastaafu wa sekta ya umma au binafsi.
 
Sijui ni kwann swala la mifuko ya hifadhi ya jamii huwa haliwekwi wazi sana kwa wachangiaji.

Mifuko mara ikaanzishwa mingi kama utitiri kisha Sasa wanaiunganisha bila ruhusa ya wachangiaji.

Mm nikijiwekea akiba yangu, ins maana mm ndiye mwenye maamuzi ya niitumie lini na wapi. Sawa tulikubali kujiwekea kwa ajili ya uzee. Lkn je haionekani kama kuzitumia hizi fedha kadiri mfuko utakavyo na kuninyima mm mchangiaji haki ya umiliki wa zile fedha ni makosa?

Leo hii tukaunganishwe, je zile faida nilizokuwa nazipata kwenye mfuko wangu zitabaki ama zitakuwa hazipo huku niliko hamia?

Je kwann mifuko hii haitoi elimu kutujuza kwa undani nini kinaendelea?
 
Back
Top Bottom