Maoni kuhusu Biashara E-Africa

Papa

New Member
Oct 10, 2007
2
0
Mimi ni mtanzania naishi South Africa nataka kujua kuna biashara gani naweza wekeza E-Africa

Nipe maoni na mifano ilio hai


Kula nao Papa
 
Mimi ni mtanzania naishi South Africa nataka kujua kuna biashara gani naweza wekeza E-Africa

Nipe maoni na mifano ilio hai

Kula nao Papa

Swali lako liko too general kiasi kwamba hakuna anayeweza kukujibu kirahisi. Biashara ziko za kila aina inategemea na mtaji wako. Ukiwa more specific kwa mfano type ya investment unayoangalia nafikiri wapo wengi tu kule bongo ambao wanaweza kukupa uzoefu wao. Vile vile unaweza kupitia TIC kuangalia jinsi wanavyowakaribisha WTZ na kuangalia pale ambapo wanaboronga au wanapatia.
 
Karibu mwekeza mzalendo, biashara nying tu hapo ni mtaji wako tu. Hata ukitaka mgodi utapata ni pochi tu!
 
Pia kazi ya udalali na serikali upo. hii taturahisiahia kuondoa ununuzi wa bidhaa feki kama rada huku vikiwa na commion kubwa sana kwa serikali. sasa hivi madalali wengi ni waasia.

ila itabidi na wewe ujiunge na chama cha kifisadi, vinginevyo watakuChifupa.
 
Papa,
Binafsi unaujuzi gani katika biashara?Experience,Skills,Qualifications?Jaribu kujikakamua iliuweze kufika mahala ambapo ungpenda kuanzisha biashara yako. Fanya uchunguzi iikujuwa kama kutakuwa na comptetitors kiasi gani na kama wapo wasikukatishe tamaa...watumie ilikuongeza ubunifu mwingi ambao utakongezea mapato!Man,there is more info za kukusaidi lakini jaribu kukusanya mawazo yako kwa ujumla na kuyapanga kwanza.
Kila la kheri.
Bhoey
 
Biashara nzuri ni ile unayoipenda wewe na kuweza kuifanya wewe mwenyewe. Je unataka ushauri wa kufanya biashara wewe mwenyewe au kuwekeza kwenye biashara nzuri. Kama unataka kuwekeza Tanzania kuna sekta za beer na sigara. Watu wanakunywa sana pombe na kuvuta sigara na kuhatarisha afya zao. hivyo wekeza kwenye biashara ya madawa ya kutibu magonjwa yanayotaka na kunywa sana beer na kuvuta sigara utapata pesa. Sekta zingine ni madni na utalii. Kuna madini ya kila namna Tanzania na kuna vivutio vingi vya asili. Kama unaweza kujenga Hotel au lodge nzuri huko mbugani utapa pesa. Pia kama utauza cell phone,mchicha na samaki utapata pesa. Fikiria unachoweza na mtaji ulio nao, ukijenga nyumba na kuziuza utapa pesa, ukizipangaisha utapata pesa. Biashara zipo nyingi jaribu ile unayoipenda angalia hasara na faida zake na kama hailipi anzisha ya aina ingine. Kikubwa ni kumake sure unaipenda hiyo biashara. Ukiuza mavazi au fanicha utapa pesa. Hakuna mteremko lazima uhangaike na ujionee mwenyewe. Ushauri ni kitu kizuri lakini nikikwambia kafanye biashara ya kujenga kiwanda cha sabuni utaweza?
Kuna watu wanauza viwanda vinawashinda wapo pia wanaouza biashara zinawashinda. Mazingira ni magumu kila mahali si ulaya si Marekani si Japan. Kwani huko South Africa unafanya biashara gani? anzia huko kwanza na biashara inayofaa kwa huko. Kisha uingie Bongo tayari ukiwa mfanyabiashara. Usisubiri mpaka uende Bongo. Anza hata kuuza maji kaisha unaingia China unanunua mashine za kutengeneza mitambo ya kuchuja maji na kuyaita Sauzi Water, utapata hela. Au anza kuuza chapati hukohuko South Africa kisha ingia Bongo na mashine za kutengeneza chapati, tafuta tenda utapata unaweza kutengeneza chapati 1,000,000 kwa wiki kila chapati shilingi 100 unapata milioni 100 za Tanzania kwa wiki taratibu namna hiyo. Baadae unatafuta soko huko South Africa, Chapatai zako zitapata soko ukijua kutengeneza chapati safi na nzuri. Biashara ni biashara hata ukiuza maji, kahawa, chai, biskuti, utapata fedha. Shindwa mwenyewe babu. Ndio maana nakwambia fanya ile unayoipenda wewe. BOngo sasa hivi jua kali unaweza kushusha air condition 50 au 100 kutoka huko South au nchi ingine? Kila biashara ina ushindani wake na utundu wake je wewe utundu wako nini? Usiibe usiue na usiseme uongo wala kutamani mali ya watu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom