Maoni: Katiba Mpya ndio msingi utakaoweza kuwapunguza spidi na kiburi watawala

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Hii ni mada fikirishi, Kuna wakati watu walitaka kukusanyika kwa ajili ya kumuombea Tundu lissu lakini wakaambiwa marufuku na ni uchochezi, Aliyesema haya bado yupo, Mbona kimya sana.

Akiwa Nairobi hospital, Hakuna Mbunge wa CCM aliyeweza kwenda hata kutuma Salamu za Pole, Wengi ya wabunge wa ccm walisema wanatishwa na wanaogopa kwenda kutokana na amri, Huyo Mtoa amri yupo wapi, Mbona kimya sana

Ni kitu gani kinamfanya huyo mtu akae kimya? Kwa huu ukimya na yupo wapi kwa sasa? Anafanya kitu gani huko aliko?

Kama ni nguvu kwanini anashindwa kutumia hiyo nguvu tena?

Yote haya aliyatenda kwa kuwa na katiba mbovu na isiyofuata msingi wa haki.

Katiba Mpya ni muhimu ili kuzuia haya yasitokee tena.

Kumpatia mtu mmoja Madaraka makubwa huyageuza mamlaka kuwa ya kifalme.

Katiba itakayoondoa Wanasiasa kama wakuu wa wilaya na Mkoa ndio suluhisho.

Ni wakati sasa wakuu wa Mikoa wakapigiwa kura na wananchi na wakawa na nguvu za kukataa au kupitisha sera mbovu kutoka Bungeni.

Bunge kufanya mambo yote pekee bila watu wa kupiga kura kilichopitishwa Bungeni ndio huzaa Bunge Butu.

Ni muhimu kila mkoa ukachagua mkuu wao wa Mkoa ambaye atakayeweza kupiga kura ya veto kwenye bajeti ya nchi, Hawa wakuu wa wilaya wa aina ya Sabaya ni tatizo.
 
Back
Top Bottom