Arusha: Political Base ya Lowassa inayosambaratika
Ili kutimiza ndoto yake ya kugombea urais, Lowassa bado anahitaji sana supremacy ya mkoa wa Arusha ili kuwaonyesha CCM kwamba ana nguvu kwenye base yake, charity begins at home. CHADEMA kwa sasa ni threat kubwa sana kwa Lowassa kuliko hata wana CCM wenzake. Pigo la juzi pale Arumeru Mashariki lilimuonyesha kwamba anaweza kuwashinda wana CCM wenzake within the party, lakini nje ya CCM kuna kiboko yake ambao ndio waliomgalagaza Siyoi. Hilo linaweza kuwa limefungua ukurasa mpya na kuanza kusuka mikakati mipya ya namna ya ku-neutralize nguvu ya CHADEMA mkoani Arusha.
[/QUOTE]Je, kuhamia kwake CHADEMA kutambadilisha utiifu aionao kwa Lowassa?
Je, Lowassa akiwa na nia fulani, mfano, kutaka kuchukua jimbo la Arusha Mjini au Arumeru Magharibi, hatamtumia kijana?
Je, CHADEMA watakapoendelea na kampeni za kumbomoa Lowassa, Millya atashiriki kikamilifu?
What if Jimbo mojawapo huko Arusha akiwekwa chaguo la Lowassa, je kijana atakuwa upande upi?
Je, Itikadi yake imebadilika ghafla? Siyo kwamba CHADEMA wanajiletea Shibuda mwingine? Maana ni juzi tu alikuwa anasema CCM safi, ubaya wa CCM umeanza lini? Kama CCM ni mbaya ilikuwaje wiki chache zilizopita akaomba kugombea ubunge wa EAC? Alikuwa kwenye kampeni za Arumeru Mashariki akipambana na CHADEMA lakini leo anasema CHADEMA safi!
Asante kwa uchambuzi makini na wa kina; uchambuzi huu umesaidia kuweka mawazo ya wana-mapinduzi wa kweli bayana. Huu ni unabii tosha, na Lowassa ni mtu wa mikakati wakati wote, ili kujiwekea mwelekeo haiwezi kuwa shida kumwandaa kijana na kuweka ngome ndani ya ngome ya upinzani. Mapokezi na vingine viwa kwa kupamba kisiasa, ila inapokuja kwenye kushughulika na mambo ya msingi ushabiki uwekwe pembeni. "Mtu aliyeongoka karibuni asipewe wajibu wa kuongoza kundi"