Maoni Binafsi: Ujio wa Bwana James Ole Millya ndani ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni Binafsi: Ujio wa Bwana James Ole Millya ndani ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Keil, Apr 16, 2012.

 1. K

  Keil JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanza naomba niweke wazi kwamba mimi ni shabiki wa "mabadiliko" na nina amini kwamba mabadiliko yatakuja kwa kuiondoa CCM madarakani. Siamini kwamba hawa wanaojiita wana mabadiliko ndani ya CCM watakuja kutuletea mabadiliko kwa sababu yeyote atakayetaka mabadiliko ya kweli yenye kulenga kutendeka kwa haki basi kama ni mwana CCM atakuwa anakata tawi la mti ambalo yeye mwenyewe amekaa.

  Habari za Bwana James ole Millya kutangaza kwamba anaondoka CCM na kujiunga na CHADEMA, wengine wanaweza kuwa wamezipokea kwa furaha, mimi nimezipokea kwa hisia mchanganyiko na huku nikijitahidi sana kuwa makini na kuwasihi CHADEMA wawe na tahadhari. Kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa nayo pia imenifanya niwe na woga zaidi.

  Sababu ambazo zimemuondoa Millya ndani ya CCM ni hizi hapa:
  Kwanza, alikuwa kwenye mgogoro na chama chake katika ngazi ya mkoa na pia ndani ya UVCCM. Mgogoro huo ulikuwa umemuwekea doa baya ambapo ingekuwa ngumu sana kupata uongozi wa aina yoyote ile ndani na nje ya chama. Kwa taratibu za CCM uteuzi wa mgombea hufanywa na vikao vya juu, kwa utaratibu huo Millya asingeweza kukatiza kwenye hivyo vikao. Angeweza kupenya kwenye vikao vya wilaya na mkoa, lakini ndani ya CC ingekuwa ngumu kukatiza. Mfano mzuri ni hivi majuzi alipofyekwa kwenye wagombea wa EALA.

  Nguvu ya Lowassa inaanza kupungua na pia Lowassa hana msaada tena kwa kijana kwa kuwa hata kama kambi ya Lowassa wanaweza ku-influence maamuzi ya vikao vya mkoa na wilaya, bado vikao vya juu ni ngumu sana. Kwa hiyo political "career" ya kijana ilikuwa imefikia ukingoni bila kupenda. Hakuwa na option nyingine zaidi ya kuondoka kwenye chama, maana chama hakimhitaji tena. Mara baada ya kumaliza muda wake wa uongozi ndani ya UVCCM mwaka huu angekuwa amefikia tamati. So, the best option ni kujitoa mapema ili "kuondoka kwa heshima".

  Kwa hiyo hoja kwamba kuna watu wamezunguka nchi nzima wakimchafua, haina mashiko. Ila kuna watu ambao wanapeleka taarifa zake Lumumba kila anapotoa kauli zenye utata na ukakasi.

  Kauli ya Mbowe
  Ni kweli Bwana Millya hana kashfa ya moja kwa moja ya kuonyesha kwamba ni kijana mchafu. Tatizo lake ni kwamba alishachagua upande wa kundi la Lowassa na hivyo kumtenganisha na ufisadi wakati mwingine inaweza kuwa ngumu. Ni sawa na jinsi CCM inavyosema kwamba mafisadi wako wachache, lakini wameshindwa kujitenga nao. Same applies to Millya ambaye amekuwa mtetezi wa Lowassa siku zote, sasa leo CHADEMA watawezaje kumtenganisha na Lowassa mchafu?

  Millya ni kijana mtiifu wa Lowassa. Kuna maswali mengi ambayo CHADEMA wanatakiwa kujiuliza kabla hawajamkumbatia na kumpa majukumu ya kukijenga chama au kuendeleza mapambano. Kukijenga chama ni pamoja na kumpa mtu responsibilities ambazo zitamsogeza karibu zaidi na mfumo mzima wa chama.

  Je, kuhamia kwake CHADEMA kutambadilisha utiifu aionao kwa Lowassa?
  Je, Lowassa akiwa na nia fulani, mfano, kutaka kuchukua jimbo la Arusha Mjini au Arumeru Magharibi, hatamtumia kijana?
  Je, CHADEMA watakapoendelea na kampeni za kumbomoa Lowassa, Millya atashiriki kikamilifu?
  What if Jimbo mojawapo huko Arusha akiwekwa chaguo la Lowassa, je kijana atakuwa upande upi?
  Je, Itikadi yake imebadilika ghafla? Siyo kwamba CHADEMA wanajiletea Shibuda mwingine? Maana ni juzi tu alikuwa anasema CCM safi, ubaya wa CCM umeanza lini? Kama CCM ni mbaya ilikuwaje wiki chache zilizopita akaomba kugombea ubunge wa EAC? Alikuwa kwenye kampeni za Arumeru Mashariki akipambana na CHADEMA lakini leo anasema CHADEMA safi!

  Arusha: Political Base ya Lowassa inayosambaratika
  Ili kutimiza ndoto yake ya kugombea urais, Lowassa bado anahitaji sana supremacy ya mkoa wa Arusha ili kuwaonyesha CCM kwamba ana nguvu kwenye base yake, charity begins at home. CHADEMA kwa sasa ni threat kubwa sana kwa Lowassa kuliko hata wana CCM wenzake. Pigo la juzi pale Arumeru Mashariki lilimuonyesha kwamba anaweza kuwashinda wana CCM wenzake within the party, lakini nje ya CCM kuna kiboko yake ambao ndio waliomgalagaza Siyoi. Hilo linaweza kuwa limefungua ukurasa mpya na kuanza kusuka mikakati mipya ya namna ya ku-neutralize nguvu ya CHADEMA mkoani Arusha.

  Hapa ndipo ninapopata mashaka makubwa sana, CHADEMA wanatakiwa kuwa makini sana hawa watu wanao-cross vyama ghafla, wengi wao wanaishia kuwa mizigo kwenye vyama na hasa kama walishawahi kuwa na nyadhifa kubwa ndani ya CCM. Mifano mizuri tunayo, akina Shibuda na Mrema. Afadhali umpokee mtu ambaye hajanywa maji ya kijani kwa kuwa huna uhakika sana na Itikadi yake. Lakini kama mtu alishawahi kunywa maji ya kijani na alikuwa na ndoto ya kuchaguliwa kupitia CCM, wengi wao huwa wanakuja kuwa mizigo ndani upinzani. Watu wa papo kwa papo ni ngumu sana kuwabadilisha itikadi, huwa wana hama na itikadi zao. Leo hii Shibuda ni mbunge kupitia CHADEMA lakini msimamo wake kwa 100% ni sawa na mwana CCM tu.

  Wapinzani wajifunze kutoka CCM
  Mzee Makamba alikuwa anatuhumiwa kurubuni wapinzani, lakini wakifika huko hakuna walichokuwa wanaambua. Ni wachache sana ambao hubahatika kupenya kama akina Ngawaiya. Lakini wengine akina wengi wao sasa hivi hata hawajulikani wako wapi.

  Ushauri wangu
  Ningeshauri huyu kijana asipewe responsibilities kubwa au hata kama akipewa basi kuwe na mtu ambaye ana-monitor shughuli zake kwa ukaribu. Issue ya Millya iko more complicated kwa sababu ya connection yake na Lowassa ambaye bado yuko CCM na bado anataka kuonyesha ana nguvu Arusha, halafu CHADEMA wanamkabidhi kijana mtiifu wa Lowassa kazi ya kumbomoa Lowassa mkoani Arusha, total contradiction! Kama Lowassa angekuwa ame-give up ndoto yake ya kutaka kugombea urais, then ingekuwa rahisi kumwamini kijana kwa 100% kwamba amekuja kwa nia njema na uwezekano wa kukihujumu chama ni mdogo.

  Kuna wanachama wengi sana wa upinzani ambao ama wanatumiwa na CCM au individuals ambao wako CCM ili kuvihujumu vyama vya upinzani na hasa zinapokuja nyakati za uchaguzi. Mfano, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya, ametuhumiwa mara 2 kwamba ameuza ubunge wa Mbeya Vijijini . Mara ya kwanza Wakili mzima alikosea kujaza fomu za kugombea Ubunge, aliwekewa pingamizi na akatupwa nje. Mara ya pili na hii ndio ilileta kasheshe, jamaa akatuhumiwa kwamba kauza ubunge. Baada ya hapo Dr. Slaa alimtetea sana na jamaa akajifanya kususa kwamba amejitoa kwenye uongozi na hatimaye tukashangaa JK anamkabidhi kadi ya CCM. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, bila sababu za kueleweka hakurudisha fomu ya kugombea Jimbo la Isimani (kwa Lukuvi), matokeo yake Lukuvi akapita bila kupingwa.

  Haya mambo ya papo kwa papo, ni rahisi sana kuliwa. Hayana tofauti na chekundu au cheupe? Wewe unaona chekundu, jamaa akija kufungua unakuta cheupe na tayari umeishaliwa.

  Kama nitakuwa nimewakwaza wana CHADEMA, naomba mnisamehe.
   
 2. D

  DOMA JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Good ideas
   
 3. A

  Analytical Senior Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Well analyzed.
   
 4. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Yap yap yap
   
 5. c

  collezione JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  CHADEMA wawe makini hapo.
  Afu ndo hiki kitu nilikua nasema kila siku. CHADEMA, wanatakiwa wawe na kanuni au katiba madhubuti kwa ajili ya kupokea member wapya. Na pasiwe na upendeleo katika hili.

  Wasipokee watu tu, kama dampo. Wazingatie kanuni, katika mchakato wa kupokea watu (hasa waasi kutoka vyama vingie). La_sivyo inawezekana ikawa mtego, kwa chama kizima.

  CCM imekufa, kwa sababu ya kupokea mamluki bila kufuata taratibu. Hatimaye hayo mamluki yanaingia kwenye chama kwa nia ya ufisadi, na mwisho wake kuhujumu chama.

  Wahenga husema, "ngoma ikilia sana, mwisho wake itapasuka". CDM sasa hivi, ngoma yao inavuma kila kijiji hapa Tanzania. Na kila mTanzania sasa hivi anatamani kuingia ngomani kucheza. CDM wasipokuwa makini, watawapokea fisi ngomani. Badala ya binadamu.
   
 6. E

  Erasto..sichila Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We mwongo wanao jiunga upiozani ni binadam u huo unafiki unao usema upo lakini mi pia nafikiri umetumwa kuleta unafiki ili umuvuruge huyu tunasema time will tell ujue pia we ndugu yeye kaamua kujiunga wako watuchadema wengi ndio wenye chama ninacho shauri hatafisadi aje chadema apokewe ili tupa te siriza kuibomoa Ccm nasema unafiki ziiiiiii njo milya acha siasaza majitaka kom
   
 7. c

  collezione JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  My take:
  CDM waamini sasa chama kimekua. Wajitahidi kuwa na katiba "madhubuti" kwa ajili ya kuongoza chama Chenye idadi kubwa ya watu. La_sivyo wengine mafisi, wataingia kuhujumu chama..

  Kila raheli katika mchakato wa katiba mpya. Msisahau kuwa na katiba ya chama, yenye strong roots pia....

  Kupokea watu, sio tija. Hata kama awe Lowassa (fisadi). Ila katiba ya CHAMA izingatiwe kwanza..
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,966
  Likes Received: 1,858
  Trophy Points: 280
  Nionavyo mimi,

  Hoja yako mtoa mada ni nzuri na umejaribu kueleza kwa mtazamo ambao umeeleweka karibu kwa kila mwana jf atakayeusoma. pia umeonyesha moyo wako wa uzalendo juu ya chama chetu CDM na hofu ya mamluki abayo twaweza kuwaingiza ndani hali siyo wenzetu.

  Mimi nilianza kuingiwa na hofu hasa pale ambapo hawa watu wanajiunga na CDM baada y kukosa nafas uongozi ndani ya CCM. fano hai tuliona kwa Shibuda, Ngawaiya, Mwita nk nilipoangalia kwa mapana ya (akili yangu) nikagundua kuwa hawa watu bado hawaji na roho nyeupe CDM bali na nia ya madaraka tu. Anyway siyo vibaya kama anaouwezo wa kuongoza wakapewa madaraka lakini hofu inayokuwepo ni je! watakitumikia chama na taifa kwa ujumla wake kwa moyo wao wote? swali hili hakuna mwenye jibu nalo zaidi ya walengwa wenyewe ndani ya mioyo yao. kwani ajionavyo mtu naafsini mwake ndivyo alivyo. kwa kuwa sisi wengine hatuna uhakika wa msukumo wa ndani wa mtu basi ni vyema zaidi wakawekwa chini ya uangalizi maalum ili kutokuleta mkanganyiko wa fikra baadae.

  Pia nikirejea katika history wapelelezi walipotumwa Africa walikuja kwa njia nyingi sana sasa nasema haya kwa mawazo yangu wala nisieleweke vibaya yawezekana kabisa mtu kama James akawa amekuja kupeleleza CDM kwani najua ushindi wetu wa ARUMERU umewashtua sana na siyo hivyo tu, bali uwezo wetu umeshaonekana wazi kwahiyo wanataka wapate mbinu za kileo za kuhandle mambo. hivyo ukasukwa mpango kama huu ili kujakukidhoofisha chama baadae. sisemi kwamba ndivyo ilivyo ila naonyesha tu yale ambayo yanaweza kuwa ni matokeo.

  Pia kukua kwa CDM kumetikisa nchi kwa kiasi kikubwa na hii mi kweli kwakua ndicho chama kilichoweza kuwakumbatia vijana wale ambao Lowassa aliwaita ni bomu linalofugwa na CCM. CDM ilijijengea imani kwa vijana na wameonyesha nguvu ya dhati ya kumsaidia kijana na ndiyo sababu ndicho chama chenye wabunge wengi vijana ukilinganisha na chama chochote. Ninaamini kabisa hawajakosea kuwakumbatia vijana kwani mob psychology yao iko juu na wakiamua wanaweza thats why hata Arumeru kimepita kwa kishindo.

  Ushauri wangu kwa viongozi wetu wa CDM,MBOWE wewe ni kaka yangu, nakufaham kama mwanaharakati mpenda maendeleo, simameni kwa nguvu zote za ujana mlizo nazo kuijenga CDM yetu. Daima sisi tuko pamoja nanyi na kamwe msimbague mtu ila mumkague kwa umakini kabla ya kumuingiza kwenye nafasi za juu zenye kuhitaji maamuzi makubwa yenye nguvu. Wale wote wanao leta sifa mbaya ndani ya chama waelezwe na ikiwezekana basi wawekwe pembeni. Mtu asije akaingia leo kwa nia ya uongozi tu na sisi tukamuamini hata kidogo. Hao ndio watakao tubomolea chama. Tukumbuke kuwa 2015 siyo mbali kabisa na tunatakiwa tujiweke tayari. tuvae silaha za vita tayari kuingia kwenye uchaguzi.

  mwisho napenda kuchukua nafasi hii " KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015 KATIKA JIMBO LANGU"

  CDM People's power.

  nb haya ni mawazo tu jamani msinihukumu na kama nitakuwa nimekosea mnisamehe, ila nakubali kukosolewa na kusahihishwa.
   
 9. L

  Laptani Member

  #9
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu Keil nakuunga mkono kabisa, tahadhari kabla ya hatari. Uwezekano wa kupokea mamluki upo. Ila kama utakumbuka kauli ya Mwl. Nyerere kwamba upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM, rejea kilichoisambaratisha KANU ni wanachama potential akina Saitoti walipoamua kujoin Orange Movement; nasi hatuna budi kuwapokea kwenye M4C na kumonitor perfomance yao kama wataonyesha dalili ya usaliti tuwatie adabu itakayokuwa fundisho. Tunawahitaji hawa wapishi wa ng'ambo ya pili tupate mbinu za mapishi ya pande hizo.
  ALUTA CONTINUA!!! WE STILL INVITE ALL WHO FORESEEN AND REALISED THAT NEEDS TO BE BORN AGAIN!!
   
 10. s

  sanjo JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  WanaJF Lazima tukubaliane kuwa CDM ni chama ambacho kinaendelea kupendeka na hivyo kuwa kimbilio la kila mtu, mzuri na mbaya. Hivyo, lazima kichuje pumba, chuya na mchele.
   
 11. K

  Keil JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Zama za uwazi hizi ... taja tu Jimbo gani ili kama kuna makamanda huko msaidiane kujenga chama. Au unaogopa kuongeza ushindani?
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Laptan,

  Nakubaliana na hoja ... Mwalimu Nyerere aliposema upinzani utatoka CCM alimaanisha kwamba watakapotofautiana kiitikadi na mtazamo kuhusu approach ya maswala mbali mbali. Sasa wengi wa wanaoondoka CCM baada ya kukosa uongozi sio kwamba kinachowatofautisha ni Itikadi, NO, bali ni ulaji ndo unakuwa umeleta shida.

  Hapo kwenye mfano wa Kenya naomba tuweke rekodi sawa: KANU ilisambaratika baada ya Mzee Moi kumteua Kenyatta kuwa mgombea urais na kuwaruka wengine ambao walikuwa wanategemea. Waliondoka ni pamoja na huyo Mzee Saitoti (Prof) pamoja na akina Rutto na Odinga, wakaenda kuanzisha Rainbow Coalition (hii nayo ni mfano wa papo kwa papo) ambayo haikudumu kwa sababu hawa watu walikutana ghafla hakuna cha itikadi wala nini, wameona kwamba ulaji anapewa mwingine wakaamua kutimka.

  NARC ilipotwaa madaraka, ndoa ya hao wana siasa ilikuwa ya muda mfupi, ndipo akina Odinga, Kalonzo, Rutto, Balala na wengineo walipojitenga na kuanzisha ODM. Bado hao watu walikuwa na itikadi tofauti na wote wanataka ulaji tu na si vinginevyo. Kalonzo Musyoka alikuwa na matarajio makubwa sana, lakini alipoona kwamba hawezi kupata tiketi ya kugombea Urais akaamua kujitenga.

  Kwa hiyo hoja yangu iko pale pale kwamba haya mambo ya papo kwa papo ni hatari zaidi maana huwezi kujua hidden agenda ya mhusika.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Good analysis Keil

  One member said earlier today kwamba chadema hawawapi wageni funguo... lets wait and see

  Binafsi nimependa hii change kwasababu imeonyesha kwamba kuondoka CCM inawezekana; maana zamani walikua wanatishwa kwamba ukiondoka CCM umekwisha, siku hizi CCM ina maadui wengi kiasi kwamba haiwezi tena kupigana in all fronts na mfano mzuri ni chaguzi ndogo za mwezi April

  I think it is absolutely vital kumweka Millya nje ya majukumu yoyote ndani ya chama at least for the coming 12 months kupima seriousness yake
   
 14. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Mawazo mazuri,naushauri uongozi wa juu uyafanyie kazi.
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,573
  Likes Received: 1,939
  Trophy Points: 280
  Keil, nimekupata.

  However niko critical, vipimo ulivyotumia, ukivitumia hata humo ndani ya chama kuna watakao fail.

  Mbona kuna waliokuwa na alliances na viongozi wengine wa ccm toka kitambo na wamo kwenye uongozi chadema?Hata RA mwenyewe ali enjoy hiyo status, so i wonder inakuwaje kuhus EL.

  Pia, mbona kuna waliosapoti mgombea ubunge wa chama cha tofauti na chama chao cha chadema?Yule wa NCCR-Mageuzi aliyepata sapoti ya Zitto.
   
 16. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  safi sana mkuu
   
 17. J

  John W. Mlacha Verified User

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Keil nakukubali , na hapa ndio umeua bendi yote. mimi nina uhakika CHADEMA wasipofuata huu ushauri lazima waingie mkenge
   
 18. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mwalimu Julius nyerere aliwahi kusema
  upinzani bora utatoka ndani ya ccm. Sasa wewe unataje? Mkuu
   
 19. N

  Nyampedawa Member

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Safi sana mkuu Keil. Nakubaliana na wewe kwa 100%. Huyu jamaa lengo lake ni kacheo tu hana lolote.
   
 20. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,964
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  u r very bryt mkuu..mbowe hawezi kutuaminisha kile tunachofahamu..kuwa cdm si kuwa toy kwa kila kinachosemwa na viongozi..yeye kama anamuona msafi mi namuona si msafi..labda kama kuna ajenda.. cdm haihitaji watu kutoka ccm ili kukijenga..sababu hata tuliokuwa hatuna vyama sasa tunasapoti cdm..huyu ni askari mtiifu kwa lowasa..tunaichukia ccm yote sababu ya ufisadi wa wenzao..kwani nape ana hatia gani..?mbona huwa tunamsema vibaya..ni sababu yupo ccm..millya hata kama hana tuhuma anaem backup amejaa tuhuma ambazo cdm wamekuwa wakizisema..cdm don make us fools..pliz..millya hajawahi kusimamia kile cdm inachoamini.. Angalau samwel sitta au nape nnauye..cdm inalewa umaarufu
   
Loading...