Maoni Binafsi: Ujio wa Bwana James Ole Millya ndani ya CHADEMA

Je Huyu Miliya si ndiyo yule aliyemshtaki Ole Sendeka eti amemtishia bastola? Au yule ni nani?

Ni vizuri kufahamu utendaji wake ndani ya magamba
 
sana kuwa makini na kuwasihi CHADEMA wawe na tahadhari. Kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa nayo pia imenifanya niwe na woga zaidi.

Sababu ambazo zimemuondoa Millya ndani ya CCM ni hizi hapa:
Kwanza, alikuwa kwenye mgogoro na chama chake katika ngazi ya mkoa na pia ndani ya UVCCM. Mgogoro huo ulikuwa umemuwekea doa baya ambapo ingekuwa ngumu sana kupata uongozi wa aina yoyote ile ndani na nje ya chama. Kwa taratibu za CCM uteuzi wa mgombea hufanywa na vikao vya juu, kwa utaratibu huo Millya asingeweza kukatiza kwenye hivyo vikao. Angeweza kupenya kwenye vikao vya wilaya na mkoa, lakini ndani ya CC ingekuwa ngumu kukatiza. Mfano mzuri ni hivi majuzi alipofyekwa kwenye wagombea wa EALA.

Nguvu ya Lowassa inaanza kupungua na pia Lowassa hana msaada tena kwa kijana kwa kuwa hata kama kambi ya Lowassa wanaweza ku-influence maamuzi ya vikao vya mkoa na wilaya, bado vikao vya juu ni ngumu sana. Kwa hiyo political "career" ya kijana ilikuwa imefikia ukingoni bila kupenda. Hakuwa na option nyingine zaidi ya kuondoka kwenye chama, maana chama hakimhitaji tena. Mara baada ya kumaliza muda wake wa uongozi ndani ya UVCCM mwaka huu angekuwa amefikia tamati. So, the best option ni kujitoa mapema ili "kuondoka kwa heshima".

Kwa hiyo hoja kwamba kuna watu wamezunguka nchi nzima wakimchafua, haina mashiko. Ila kuna watu ambao wanapeleka taarifa zake Lumumba kila anapotoa kauli zenye utata na ukakasi.

Kauli ya Mbowe
Ni kweli Bwana Millya hana kashfa ya moja kwa moja ya kuonyesha kwamba ni kijana mchafu. Tatizo lake ni kwamba alishachagua upande wa kundi la Lowassa na hivyo kumtenganisha na ufisadi wakati mwingine inaweza kuwa ngumu. Ni sawa na jinsi CCM inavyosema kwamba mafisadi wako wachache, lakini wameshindwa kujitenga nao. Same applies to Millya ambaye amekuwa mtetezi wa Lowassa siku zote, sasa leo CHADEMA watawezaje kumtenganisha na Lowassa mchafu?

Millya ni kijana mtiifu wa Lowassa. Kuna maswali mengi ambayo CHADEMA wanatakiwa kujiuliza kabla hawajamkumbatia na kumpa majukumu ya kukijenga chama au kuendeleza mapambano. Kukijenga chama ni pamoja na kumpa mtu responsibilities ambazo zitamsogeza karibu zaidi na mfumo mzima wa chama.

Je, kuhamia kwake CHADEMA kutambadilisha utiifu aionao kwa Lowassa?
Je, Lowassa akiwa na nia fulani, mfano, kutaka kuchukua jimbo la Arusha Mjini au Arumeru Magharibi, hatamtumia kijana?
Je, CHADEMA watakapoendelea na kampeni za kumbomoa Lowassa, Millya atashiriki kikamilifu?
What if Jimbo mojawapo huko Arusha akiwekwa chaguo la Lowassa, je kijana atakuwa upande upi?
Je, Itikadi yake imebadilika ghafla? Siyo kwamba CHADEMA wanajiletea Shibuda mwingine? Maana ni juzi tu alikuwa anasema CCM safi, ubaya wa CCM umeanza lini? Kama CCM ni mbaya ilikuwaje wiki chache zilizopita akaomba kugombea ubunge wa EAC? Alikuwa kwenye kampeni za Arumeru Mashariki akipambana na CHADEMA lakini leo anasema CHADEMA safi!

Arusha: Political Base ya Lowassa inayosambaratika
Ili kutimiza ndoto yake ya kugombea urais, Lowassa bado anahitaji sana supremacy ya mkoa wa Arusha ili kuwaonyesha CCM kwamba ana nguvu kwenye base yake, charity begins at home. CHADEMA kwa sasa ni threat kubwa sana kwa Lowassa kuliko hata wana CCM wenzake. Pigo la juzi pale Arumeru Mashariki lilimuonyesha kwamba anaweza kuwashinda wana CCM wenzake within the party, lakini nje ya CCM kuna kiboko yake ambao ndio waliomgalagaza Siyoi. Hilo linaweza kuwa limefungua ukurasa mpya na kuanza kusuka mikakati mipya ya namna ya ku-neutralize nguvu ya CHADEMA mkoani Arusha.

Hapa ndipo ninapopata mashaka makubwa sana, CHADEMA wanatakiwa kuwa makini sana hawa watu wanao-cross vyama ghafla, wengi wao wanaishia kuwa mizigo kwenye vyama na hasa kama walishawahi kuwa na nyadhifa kubwa ndani ya CCM. Mifano mizuri tunayo, akina Shibuda na Mrema. Afadhali umpokee mtu ambaye hajanywa maji ya kijani kwa kuwa huna uhakika sana na Itikadi yake. Lakini kama mtu alishawahi kunywa maji ya kijani na alikuwa na ndoto ya kuchaguliwa kupitia CCM, wengi wao huwa wanakuja kuwa mizigo ndani upinzani. Watu wa papo kwa papo ni ngumu sana kuwabadilisha itikadi, huwa wana hama na itikadi zao. Leo hii Shibuda ni mbunge kupitia CHADEMA lakini msimamo wake kwa 100% ni sawa na mwana CCM tu.

Wapinzani wajifunze kutoka CCM
Mzee Makamba alikuwa anatuhumiwa kurubuni wapinzani, lakini wakifika huko hakuna walichokuwa wanaambua. Ni wachache sana ambao hubahatika kupenya kama akina Ngawaiya. Lakini wengine akina wengi wao sasa hivi hata hawajulikani wako wapi.

Ushauri wangu
Ningeshauri huyu kijana asipewe responsibilities kubwa au hata kama akipewa basi kuwe na mtu ambaye ana-monitor shughuli zake kwa ukaribu. Issue ya Millya iko more complicated kwa sababu ya connection yake na Lowassa ambaye bado yuko CCM na bado anataka kuonyesha ana nguvu Arusha, halafu CHADEMA wanamkabidhi kijana mtiifu wa Lowassa kazi ya kumbomoa Lowassa mkoani Arusha, total contradiction! Kama Lowassa angekuwa ame-give up ndoto yake ya kutaka kugombea urais, then ingekuwa rahisi kumwamini kijana kwa 100% kwamba amekuja kwa nia njema na uwezekano wa kukihujumu chama ni mdogo.

Kuna wanachama wengi sana wa upinzani ambao ama wanatumiwa na CCM au individuals ambao wako CCM ili kuvihujumu vyama vya upinzani na hasa zinapokuja nyakati za uchaguzi. Mfano, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya, ametuhumiwa mara 2 kwamba ameuza ubunge wa Mbeya Vijijini . Mara ya kwanza Wakili mzima alikosea kujaza fomu za kugombea Ubunge, aliwekewa pingamizi na akatupwa nje. Mara ya pili na hii ndio ilileta kasheshe, jamaa akatuhumiwa kwamba kauza ubunge. Baada ya hapo Dr. Slaa alimtetea sana na jamaa akajifanya kususa kwamba amejitoa kwenye uongozi na hatimaye tukashangaa JK anamkabidhi kadi ya CCM. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, bila sababu za kueleweka hakurudisha fomu ya kugombea Jimbo la Isimani (kwa Lukuvi), matokeo yake Lukuvi akapita bila kupingwa.

Haya mambo ya papo kwa papo, ni rahisi sana kuliwa. Hayana tofauti na chekundu au cheupe? Wewe unaona chekundu, jamaa akija kufungua unakuta cheupe na tayari umeishaliwa.

Kama nitakuwa nimewakwaza wana CHADEMA, naomba mnisamehe.[/QUOTE]
 
siasa ni ulingo mpana,wakati mwingine huwa naifananisha na taifa beberu la marekani kwa sera yake ya kutokuwa na rafiki au adui wa kudumu.huwa naenda mbali zaidi nikitafakari kwa mapana(kwa akili yangu) maana ni kama mchezo wa wapambe wa kumpa "bosi" sifa azitakazo.na tusubiri tuone
 
Ndugu Keil wataalamu wa falsafa wanasema ni vizuri kuwa na mashaka na kila kitu. "Doubt everything" ili uweze kuwa kwenye nafasi ya kuutafuta ukweli halisia.

Katika hili la Millya ni vizuri kwenda nae kimashaka mashaka ili kuweza kumuuna undani wake juu ya dhamira yake ndani ya CDM lakini haimaanishi kumzuia asiwe mwananchama.

Uzuri wa CDM ni kwamba mpaka sasa hakuna wimbi lililotokea kuiharibu limefanikiwa kwa sababu tuu ya umadhubuti wake katika kushughulikia jambo.

Shibuda kaja CDM kawa mbunge lakini mpaka sasa kajitahidi kuingia chumbani na matokeo yake kaendelea kubakia sebuleni na yawezekena hata hapo sebuleni akaondolewa. Misimamo yake aliyojitahidi kuonyesha dhidi ya CDM katu haijafua dafu kuiyumbisha CDM bali yeye mwenyewe kabakia kuyumba. Taasisi ni kubwa kuliko mtu mmoja .

Pia sio jukumu la CDM kumkataa Millya kwa sababu tu ya imani yake ndani ya CCM na kwa bwana Lowasa bali ni jukumu la CDM kumjenga na kumbadilisha kimawazo ili aweze kulandana na wengine ndani ya CDM. Maana yake ni kumuindoctrinate aweze kufikiri kinguvu ya umma na kimrengo wa kati. Yawezekana alikua blind mpaka kuwa mfuasi wa bwana lowasa sasa ni jukumu la CDM kunnarture ili awe na maono mapya.
 
Asante kwa uchambuzi makini na wa kina; uchambuzi huu umesaidia kuweka mawazo ya wana-mapinduzi wa kweli bayana. Huu ni unabii tosha, na Lowassa ni mtu wa mikakati wakati wote, ili kujiwekea mwelekeo haiwezi kuwa shida kumwandaa kijana na kuweka ngome ndani ya ngome ya upinzani. Mapokezi na vingine viwa kwa kupamba kisiasa, ila inapokuja kwenye kushughulika na mambo ya msingi ushabiki uwekwe pembeni. "Mtu aliyeongoka karibuni asipewe wajibu wa kuongoza kundi"
 
Mkuu Keil,

Nimependa uchambuzi wako, yaani kama vile uko kamati kuu ya chama CDM

Je viongozi wa CDM wanapitia humu na kusoma haya, JF ni taarifa za usalama wa taifa, kama unajua kusoma na kupembua.

Ninasema Millya anahitaji, muda ili afanywe upya utu wake wa ndani wa kuachana na CCM na kuifahamu CDM na kuyatumikia matakwa ya mageuzi kupitia CDM na vyama vingine wanaotaka mageuzi ya kweli.

Ushauri kwa uongozi wa CDM, wananchi wana matarajio makubwa sana na CDM kuleta, kusimamia mageuzi kuwaondoa CCM madarakani, hivyo wakati mnawapokea watu wanaohama vyama, msije mkapelekwa na utamu mkasahau jukumu la msingi.
 
Arusha: Political Base ya Lowassa inayosambaratika
Ili kutimiza ndoto yake ya kugombea urais, Lowassa bado anahitaji sana supremacy ya mkoa wa Arusha ili kuwaonyesha CCM kwamba ana nguvu kwenye base yake, charity begins at home. CHADEMA kwa sasa ni threat kubwa sana kwa Lowassa kuliko hata wana CCM wenzake. Pigo la juzi pale Arumeru Mashariki lilimuonyesha kwamba anaweza kuwashinda wana CCM wenzake within the party, lakini nje ya CCM kuna kiboko yake ambao ndio waliomgalagaza Siyoi. Hilo linaweza kuwa limefungua ukurasa mpya na kuanza kusuka mikakati mipya ya namna ya ku-neutralize nguvu ya CHADEMA mkoani Arusha.

Lakini, mkuu Keilo nasikia huyu jamaa EL ana mpango wa kuachana na siasa na hii ameambiwa na madaktari wake kwa usalama wa afya yake lakini EL anaona soo aache vipi maana akiachana na siasa atakuwa amewape credit Nape and his CO... ok lets wait and see

 
Nashukuru kwa analysis yako nzuri,,,, binafsi ni mmoja wa watu waliopata shida sana kuhusu milly kuhamia chadema... nilikuwa nina doubt na nia yake kuhama... je ana nia ya kweli kuhama ccm? je si pandikizi? lakini pia nilikuwa ninajiuliza kuwa influence ya lowasa ni ipi hasa katika swala hili....? binafsi ninatikiri itakuwa ni jambo la busara sana kama chama watatengeneza mtumo wa kuwajua na kuchukua tahadhari ya hawa jamaa wanao hamia ili baadae wasije kuwa bomu ndani ya chama... ninaunga mkono hoja
 
Tumewaona wengi wapo kina yule mzee wa maswa tunajua yeye alifuata ubunge tu,yupo mrema augustino na wapo cuf ambao leo ni kikwazo kule mjengoni
taf,viongozi wetu cdm kuweni macho anaweza akawa katumwa kuhalibu mbio zetu za ukombozi
 
Thank you for the well thought analysis Keil. Chadema lazima wakumbuke msemo "aisifiae mvua.........."
 
Je, kuhamia kwake CHADEMA kutambadilisha utiifu aionao kwa Lowassa?
Je, Lowassa akiwa na nia fulani, mfano, kutaka kuchukua jimbo la Arusha Mjini au Arumeru Magharibi, hatamtumia kijana?
Je, CHADEMA watakapoendelea na kampeni za kumbomoa Lowassa, Millya atashiriki kikamilifu?
What if Jimbo mojawapo huko Arusha akiwekwa chaguo la Lowassa, je kijana atakuwa upande upi?
Je, Itikadi yake imebadilika ghafla? Siyo kwamba CHADEMA wanajiletea Shibuda mwingine? Maana ni juzi tu alikuwa anasema CCM safi, ubaya wa CCM umeanza lini? Kama CCM ni mbaya ilikuwaje wiki chache zilizopita akaomba kugombea ubunge wa EAC? Alikuwa kwenye kampeni za Arumeru Mashariki akipambana na CHADEMA lakini leo anasema CHADEMA safi!
[/QUOTE]

Mkuu, hakika Millya hawezi akafanya upuuzi wa aina yoyote ndani ya CHADEMA haijalishi atakuwa amepewa majukumu ya aina gani na akiamua kufanya hujuma atakua amejimaliza kisiasa, halafu na sehemu anayotokea ni sehemu ambayo CHADEMA wameweka mizizi 100% ya kisiasa na imejenga imani kubwa sana kwa wana Arusha,
refer madiwani waliovuliwa uanachama wamebaki na ibu kubwa sana na kila sehemu wanayo pita wanazomewa, hata kutemewa mate( Diwani Rasta hili limeshamkuta)...
 
Asante kwa uchambuzi makini na wa kina; uchambuzi huu umesaidia kuweka mawazo ya wana-mapinduzi wa kweli bayana. Huu ni unabii tosha, na Lowassa ni mtu wa mikakati wakati wote, ili kujiwekea mwelekeo haiwezi kuwa shida kumwandaa kijana na kuweka ngome ndani ya ngome ya upinzani. Mapokezi na vingine viwa kwa kupamba kisiasa, ila inapokuja kwenye kushughulika na mambo ya msingi ushabiki uwekwe pembeni. "Mtu aliyeongoka karibuni asipewe wajibu wa kuongoza kundi"

Mkuu Lowassa sasa kwisha habari, ni sawa na simba wa kwenye mabanda ya sabasaba unaweza ukamsuka mabutu zile sharubu zake
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom